Ukweli kuhusu laana (Curse)

Ukweli kuhusu laana (Curse)

Katika hali ya kawaida watu wa kale waliaminishwa vitu hivi yaani baraka na neema kuwa vipo alihali kiuhalisia ni kitu ambacho hakipo.. hii ni kwa upande wangu.
Umewahi kujiuliza kwann wanaotoa laana na baraka weng wao husemekana ni wazazi au wazee/walezi kuliko mtoto kutoa laana kwa mzazi?
Je hii laana ilipangwa kwa wakubwa tu wao ndo watoaji wa laana na baraka?

Jibu ni kwamba enzi za mababu zetu maneno haya laana na baraka yalitumika kujenga watoto kukaa katika malezi mazur yaan wasifanye vitu vibaya vya kuweza kuikwaza jamiii lasivyo walitishia watapata laana and vice vesa kwa baraka maneno haya yalitumika kama silaha tu na sikweli.
Na kama kuna ukweli uliwahi kumuona mtu kapata laana papo kwa papo? Hii imejengwa akilini mwa watu kuwa laana huja baadae...hakuna ukweli wowote na ili jambo ni imani tu tumejengewa kama ilivyo imani zingne.
mkuu vitu vingine sio vya hadithi za sungura na fisi.hii kitu acha kbsa ndugu na iogope.usitegemee ukiwa na laana unajijua sahau hyo watu ndo wanajua ww umelaanika
 
subir ulaaniwe ndio utajua laana ipo.na uzr ukipata laana ww km ww huwezi kujijua ila wengine.hii ipo kiimani na nikwl ipo
Mkuu achana na hiyo imani, itakutesa sana. Ndiyo hii "fear of the unknown". Utatambika sana kwenye makabuli ya mababu zako kwa lengo hili la kuondoa "laana". Na kila utakapofeli kimkakati akili yako itakuelekeza kwenye "laana". Umeshindwa kulipa deni wanataka kuuza nyumba akili itakutuma kutambika kwenye kaburi la baba, mjomba, shangazi, mama, bibi, nk. Ili laana itoke wasiuze nyumba yako! Achana na hiyo dhana.!
 
mkuu vitu vingine sio vya hadithi za sungura na fisi.hii kitu acha kbsa ndugu na iogope.usitegemee ukiwa na laana unajijua sahau hyo watu ndo wanajua ww umelaanika
Wao wanajuaje kama nimepata laanawanakipimo cha laana?
ulimwona mtu kalaniwa?
je iyo laana uwa inampataje muhusika kutoka kwa mtoa laana na anayelaniwa?
je unajua kutoa laana?
Ulimpa laana nani?
Maneno yapi unatumia kutoa laana?
Inachukua siku ngapi laana kumpata muhusika?
Naomba leo unipe laana nitoe ushuhuda jf.

Sipendagi ujinga mimi...
 
Kwanza tujiulize neno laana latoka kwenye lugha gani? halafu ndio ulete huo ushahidi wako wa uongo latoka kwenye lugha ya kiarabu maana yake nikuwa mbali na kukubalika na Allah (Mwenyezimuungu) Hilo neno sisi wa swahili sio letu halafu hakuna dini itwayo sayansi kama hujui maana ya sayansi maana yake ni jitaahidi za uvumbuzi upo mkuu sio dini alio Kuja nayo Muhammad na Yesu isibitishe na sayansi hapana sayansi isibitishwe na vitabu vikatifu upo mzee cc waislamu na wakiristo hatuna dini itwayo sayansi upo
umeanza kufafanua vizuri ila mwishoni umeharibu kwa sababu umejitungia swali lako na kujijibu, maana yake uko nje ya maada! sijasema popote pale kwenye huu uzi kwamba ati sayansi ni dini wala dhehebu, leta mchango mkuu
 
Wao wanajuaje kama nimepata laanawanakipimo cha laana?
ulimwona mtu kalaniwa?
je iyo laana uwa inampataje muhusika kutoka kwa mtoa laana na anayelaniwa?
je unajua kutoa laana?
Ulimpa laana nani?
Maneno yapi unatumia kutoa laana?
Inachukua siku ngapi laana kumpata muhusika?
Naomba leo unipe laana nitoe ushuhuda jf.

Sipendagi ujinga mimi...
tehetehe taratibu mkuu
 
watu wakishiba ugali wana matatizo sana, eti hakuna laana! nyie mnaishi jamii ipi? acheni kujifanya hamjui haya mambo, tumieni akili ya kawaida sio sigara bwege
Punguza jaziba ili busara zipate nafasi! Hebu tusaidie: umewahi kukutana na mtu aliyealaaniwa? Yukoje? Au nini kilikutuma kuona kuwa huyu ni mtu aliyelaaniwa?! Si kweli kwamba mpaka mtu anayemfahamu alipokwambia kuwa huyo unayemuona amelaaniwa ndipo nawewe akili yako ikaelekea huko?
 
Laana na Baraka zipo na sio suala la kufikirika kama wengine wanavyosema humu. Hebu tuanzie na vitabu vitakatifu tuone namna Baraka na laana zilivyo.
  1. Someni ktk biblia kitabu cha mwanzo laana aliyotoa Mungu kwa 'nyoka', Hawa na Adamu baada ya uovu wa kwanza.
  2. Someni pia kitabu hicho hicho laana ya Mungu kwa Kaini baada ya kumuua nduguye Abeli
  3. Someni Baraka kwa watoto wa Ibrahim Isihaka na Ishmael.
  4. Someni Baraka na laana za Nuhu (kama sikosei) kwa wanae kwa aliyemcheka na wale waliomfunika akiwa amelewa.
  5. Someni Baraka za Israel (Yakobo) kwa wanawe
Ni Mengi ya kusoma ila LAANA na BARAKA zipo, mfano hai zaidi ni Amri ya 4 Ya Mungu ;waheshimu baba na mama upate heri na miaka mingi duniani. hebu angalieni wale ambao waliheshimu wazazi DHIDI ya wale waliowadharau upate mifano.
 
Hakuna kitu kama hicho.Ni suala la kisaikolojia tu. Linamuathiri yule anayeliamini.
Laana ipo mzee kama unabisha jaribu uone.Laana ni adhabu apeyo mtu baada ya kudhulumu nafsi ya mwenzie yaani kumfanyia ubaya au kumkosea Allah.

Kuna laana itokayo moja kwa moja kwa Allah kama vile laana aliyopewa ibilisi na kuna laana ambayo unakuta mja fulani amemdhulumu mja mwenzake,sasa yule aliyedhulumiwa akamshitakia Mola na kumkabidhi Mola amfanye lolote yule aliyedhulumu.

Na sio laana atakayoomba binadamu imfikie mtu fulani itamfikia lazima iwe ya kweli na huyo awe kweli amedhulumu(amekufanyia jambo baya) la sivyo inakurudia mwenyewe.

Kutokana na uwepo wa jambo hilo yaani laana na jinsi lilivyokuwa zito tumehimizwa sana tujizuie kupeana laana.

Dawa ya laana ni mtu kufanya toba na kukiri makosa yake na anatakiwa kwanza kurudi kwa yule aliyemkosea kama anamjua kisha amtake Mola msamaha na Mola ni mwingi wa kusamehe.

Halafu tuwe na desturi ya kuuliza kama kitu hukijui mzee.
 
Ndiyo hivyo. Hiyo ni dini kama zilivyo imani za dini. Ni METAPHYSICAL. Na halina logic yoyote. Ingekuwa ipo kweli ni kwa nini itoke kwa wazazi ama watu wa karibu tu wakati maovu umewatendea watu mbali mbali?! Kwa nini ukikosa adabu kwa wengine usilaaniwe?! Hata hilo neno "baraka" ni upuuzi mtupu! Hakuna kitu kama hicho.! Na ndiyo maana hata ukisali kabla ya kula, yaani kukibaliki chakula, kama kina sumu itakuathiri tu na kama kina kipindupindu utaugua tu.
Nani amekwambia laana inatoka kwa baba na mama au watu wa karibu tu ?
 
Laana ipo mzee kama unabisha jaribu uone.Laana ni adhabu apeyo mtu baada ya kudhulumu nafsi ya mwenzie yaani kumfanyia ubaya au kumkosea Allah.

Kuna laana itokayo moja kwa moja kwa Allah kama vile laana aliyopewa ibilisi na kuna laana ambayo unakuta mja fulani amemdhulumu mja mwenzake,sasa yule aliyedhulumiwa akamshitakia Mola na kumkabidhi Mola amfanye lolote yule aliyedhulumu.

Na sio laana atakayoomba binadamu imfikie mtu fulani itamfikia lazima iwe ya kweli na huyo awe kweli amedhulumu(amekufanyia jambo baya) la sivyo inakurudia mwenyewe.

Kutokana na uwepo wa jambo hilo yaani laana na jinsi lilivyokuwa zito tumehimizwa sana tujizuie kupeana laana.

Dawa ya laana ni mtu kufanya toba na kukiri makosa yake na anatakiwa kwanza kurudi kwa yule aliyemkosea kama anamjua kisha amtake Mola msamaha na Mola ni mwingi wa kusamehe.

Hkama kitu hukijui mzee.
Kiongozi umewahi kukutana barabarani au mtaani na mtu aliyelaaniwa?! Ulimtambuaje?!
 
Hakuna kitu kama hicho ni Upuuzi uliopitiliza.Laana ndio nini huyo aliokulaani yeye hajakosea watu
 
Kiongozi umewahi kukutana barabarani au mtaani na mtu aliyelaaniwa?! Ulimtambuaje?!
Sasa mbona unachanganya mada mzee ? Suala ni uwepo wa laana au mpaka nimuone ? Kwa akili ya kawaida mwenyewe jijibu mzee.Sasa utamtambuaje ? Kwa macho huwezi kumtambua suali ni sawa sawa na kuuliza je unaweza kumjua mwanamke aliyeachika kwa kumtazama ? Jibu ni huwezi.

Haya,unataka kusema nini baada ya hapo ?
 
Niliwahi kushuhudia....tukio la kijana akimtwanga mangumi mama yake mzazi...na kumdhalilisha vibaya sana......mbele ya kadamnasi....

Yule mama kuna maneno aliyoyaongea ambayo sikuwa nayatilia maanani lakini baada ya muda tukaja kuona maana yake na madhara yake.....

Namnukuu...

" Wewe Charles( sio jina halisi) kama hujawahi kunyonya ziwa hili ( huku akionyesha ziwa lake) na kama hujakaa tumboni hapa( huku akionyesha tumbo lake)..........tutaona yatakayo kupata......

Baada ya muda kidogo
yule bwana maisha yake yalibadilika haraka sana.......aliacha kazi yeye mwenyewe kwa hiyari yake.....akaanza kuvaa nguo za mkewe....na matukio mengine yakiyotuwacha mdomo wazi......

Mpaka ninavyoandika hapa yule jamaa ni kichaa kabisaa....tena huwa namuonaga hata pale maeneo ya jangwani.....hata tukipishana hanifahamu tena.......

Haya mambo sio ya mchezo....kabisa.....
 
Sasa mbona unachanganya mada mzee ? Suala ni uwepo wa laana au mpaka nimuone ? Kwa akili ya kawaida mwenyewe jijibu mzee.Sasa utamtambuaje ? Kwa macho huwezi kumtambua suali ni sawa sawa na kuuliza je unaweza kumjua mwanamke aliyeachika kwa kumtazama ? Jibu ni huwezi.

Haya,unataka kusema nini baada ya hapo ?
Maana yangu ni kwamba ili umuone mtu kuwa kalaaniwa, ni lazima watu waseme ndipo nawewe akili yako ielekee huko. Kwani nikilaaniwa napatwa na nini specifically?!
 
Back
Top Bottom