safi sana mkuu Mungu akubariki, ni sahihi kuwa laana inaweza kuletwa na Mungu lakini hapo kwa binadam bado nna dukuduku kwa maana siamini kama mwadam anaweza kuachia laana kwa nguvu zake tu( physical power) bila nguvu ya kiroho ( spiritual power) kuhusika, hiyo imekaaje mkuu
Mungu wetu ni wa huruma na rehema,Mungu halaani bali matokeo ya dhambi ndo huleta laana,tunapofanya dhambi hututenga na Mungu tunafungua mlango wa mabaya juu yetu maana tunakuwa hatuna Ulinzi tena wa Mungu juu yetu,na ndiyo maana pale ambapo utagundua kwamba umekosea ukatubu ukarudi kwa muumba wako Unapata rehema.
Yes binadamu naye anauwezo wa kutoa laana na baraka,tumeumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo tunauwezo wa kuyashiriki Yale ya kimungu,kuna nguvu fulani ya kiasili ipo katika mwanadamu katika kutamka,kuna mstari katika Biblia unaosema ninyi ni miungu .
Achilia mbali katika maisha ya kiroho Hata kikawaida tu tunaambiwa angalia sana maneno Yale unayoyatamka maana yana matokeo makubwa maishani mwako,"Wanasayansi wa maswala ya kisaikolojia wanasema badili unavyofikiri ili ubadili unavyosema" kwanini wanasisitiza Hilo wanajua ipo nguvu katika ukiri/maneno , ukiwa na mtazamo Chanya utaongea chanya na utaleta matokeo chanya. Na ndiyo maana wataalam hao wanatushauri sana ile asubuhi unapoamka waza na ukitamke kitu kizuri kwaajili ya siku yako hiyo,panga mipango yako kisha kuwa na mtazamo chanya kwamba utafanikiwa,na Hata kama umeshindwa Jioni angalia wapi ulikosea sahihisha waza na kiri kufanikiwa tena. Wakati mwingine sisi wenyewe pasipo kutamkiwa na mtu mwingine tumejilaani wenyewe,mtu unatamka yaani Mimi ni wa hivi hivi tu,ndiyo utabaki wa hivyo hivyo, au Mimi nitakufa na umaskini wangu kweli utakufa maskini, au wanawake wote pasua kichwa ndiyo Hata wakija wazuri kwako utawaona ni pasua tu na utaendelea kupata pasua kichwa tu.
Tujifunze Hata katika watu waliofanikiwa maishani katika dunia ya Leo wengi wao ukiwasoma historia zao walitembea na usemi fulani,walikubali kutoshindwa pamoja na vikwazo vingi walivyokutana navyo walikiri ushindi wakatimiza ndoto zao.
Pia ipo laana ambayo mtu huambatanisha na nguvu ya giza,ndo maana Hata wachawi na waganga wanalitambua hilo la nguvu ya maneno, pamoja na mauchawi yote wafanyayo lakini lazima atamke maneno fulani ya kumlenga yule aliyemkusudia,sasa kwa Yule ambaye amekusudiwa kama ana nguvu ya Mungu ndani yake uchawi huo haufanikiwi lakini kama hana ni rahisi kuchukuliwa na kusudio Hilo.
Ila hakuna kulaani kupitia nguvu ya Mungu tumeagizwa kutoa Baraka tu,Yesu alisema waombeeni wanaowaudhi maana kwa kufanya hivyo unapalia makaa juu ya kichwa chake,na akasema ukipigwa shavu la kushoto geuza na la pili,mtu akitamka maneno mabaya juu yako Wewe muombee tamka baraka juu yake, kisha yafute yote kataa maneno hayo,mwachie Mungu ndo atashughulika naye.
Pia tujue tu kikawaida apandacho mtu ndicho avunacho,ukimtendea mwenziyo ubaya jua yapo matokeo ya hayo mabaya Hata kama siyo Wewe wapo katika wanaokuhusu watapata,ukitenda wema utalipwa wema Hata kama siyo Wewe wapo watakaolipwa kwaajili yako ndo maana Hata waswahili wanasema Wema hauozi.