Ukweli kuhusu kununua Views YouTube na VEVO

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
1,758
6,087
Kutokana na Wimbo wa DiamondPlatnumz - Hallelujah kufikisha views 1M ndani ya Saa 15 tu, Imeleta minong'ono mingi ya kwamba jamaa ananunua Views na ndio maana Msanii mkubwa kama yeye hayupo VEVO.

UKWELI ni kwamba, ni kweli Kuna watu wananunua views YouTube. Lakini hii haiwezi kukupa uhakika wa kupata views wa kudumu sababu YouTube Team huwa inang'amua fake Views na kuwafuta.

Na si kweli kwamba ukiwa VEVO huwezi kununua Views. Unaweza kununua pia maana VEVO's Views inatokana na YouTube viewers.
Na kuna site nyingi za kununua Views, lakini inabidi umakini sababu scammers ni wengi zaidi.

Faida ya Msanii kuwa na akaunti ya VEVO ni malipo mazuri yanayotokana na matangazo yanayotoka VEVO, pamoja na Wimbo kuonekana kwa Viewers wapya ambao ni subscribers wa VEVO.

Nakumbuka Diamond alisema amejitoa VEVO sababu hakutaka kupoteza Subscribers wake. Na ni ajabu Msanii mwenye Subscribers 700k anunue Views.

Hizi hapo chini ni bei ya kunua views.
15b1f88740adf8dc65bb7ac21b7898ce.jpg


Video yenye maelezo zaidi Tofauti ya VEVO na YouTube.
 
Pole yao wanaonunua... Ila ukweli ni kuwa kuna uwezekano wa kufika hata views 2m ndani ya siku pia ikiwa kutakuwa na ushirikiano mzuri.
 
Wanabwabwaja sana aseee ngoja wanyooshwe asee sio kwa mkimbize huu.Kama anabisha VEVO wana nyimbo ya MARRY YOU akatazame ina viewers wangapi....
 
Kwa jirani hakukaliki hata kidogo wanaweweseka tu wakiongozwa na dada yetu Mange, hawaamini record yao haijakaa hata mwezi imetolewa kwenye reli na mwenye record zake....
Yani ni sawa na kiduku arushe rocket yake kuelekea Newyork ni mshike mshike kwa kweli.
 
Taratibu nawaona watu wa kodi wanakuja chukua 18% zao . Mi naona mnawachongea kwa mamlaka za kodi
 
Mange anataka kuongezwa Mke mwingine kwa Diamond au anahitaj mtoto tu!?? Maaan naona hamuishi Mdomoni
 
Back
Top Bottom