Ukweli kuhusu kauli ya vyombo vya ulinzi na usalama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu kauli ya vyombo vya ulinzi na usalama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kishongo, Oct 8, 2010.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot](Source: RAIA MWEMA NEWSPAPER)
  [/FONT]


  ONYO la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama limeibua mjadala mpana na mzito nchini. Ni mjadala unaohusu weledi wa mijeledi. Wengine katika vyombo vya habari wanapigia kelele wakisema si weledi kumbe wanaogopa mijeledi!

  Baada ya Luteni Jenerali Abdulraham Shimbo kutoa onyo, wapo waliostuka na wakidhani JWTZ imetangaza hali ya hatari, wengine wakidiriki kusema imedhamiria kuinusuru CCM huku wengine wakisema ilikuwa ni kazi ya jeshi la polisi.

  Niliposikia hayo wakati nikiwa katika ndege, niliogopa nikidhani wajomba wamechukua hatamu sasa. Hawataki upuuzi na wanataka Jakaya Kikwete aongoze nchi vyema hadi matokeo ya uchaguzi mkuu yatakapotangazwa.

  Lakini baada ya kukaa na kutulia, nilitafuta kauli sahihi iliyorekodiwa na kisha nilipata taarifa sahihi kwamba kumbe JWTZ haijatoka kambini kama ilivyokuwa imeripotiwa na wanasiasa na wadau wengine!

  Kumbe ilichokuwa imekifanya JWTZ ni kujaribu kuonya vyama (ikiwemo CCM) kwamba hakuna damu itakayomwagika; kwani uchaguzi utafanyika katika mazingira ya amani na utulivu.

  Ila, kilichonistua na kuonyesha watu hawajaelewa mantiki ya onyo la JWTZ ambalo ni jeshi lenye historia ya utiifu, ni pale wanasiasa wa Upinzani walipoibuka na nadharia kwamba jeshi limelenga kuinusuru CCM.

  Nilipaswa kurejea onyo la Luteni Jenerali Shimbo, lakini bado nilipata ukakasi kuoanisha na kile kilichozungumzwa na Upinzani asubuhi yake.
  Wapinzani ambao baadhi tunafikiri ni wanasiasa wasomi, wakajikuta katika lindi la ujinga.

  JWTZ ilisema, kwa niaba ya vyombo vya ulinzi na usalama: "Hakuna umwagaji damu utakaofanyika. Uchaguzi utafanyika kwa amani na kwamba vyombo hivyo viko tayari kupambana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani."

  Hapa ukifanya uchambuzi wa kimaduhui, huoni hata sehemu moja ambayo JWTZ inasema imepanga kuibebea mbereko CCM kama ilivyodaiwa na vyama vingine vya Upinzani.

  Jambo la ajabu kabisa ni kwamba, hata mwanangu wa chekechea alimwelewa Shimbo. Alichokisema ni kwamba, wao wa vyombo vya ulinzi na usalama watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuvuruga amani ya nchi.

  Lakini, nilistuka kusikia eti JWTZ imepanga kuinusuru CCM! JWTZ haikusema kwamba vyama vya Upinzani vikubali matokeo yoyote ambayo yatatangazwa kwamba CCM imeshinda. Ilichosema ni kwamba vyama vya siasa, ikiwemo CCM, vikubali matokeo yoyote.

  Sasa unaweza kuona jinsi uwezo wa kufikiri wa baadhi ya wanasiasa wetu ulivyo mdogo au kuchanganyikiwa na mambo mengi ya maisha. Ni wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia.

  Wanasiasa wenye migogoro ya kinafsia, kifamilia na jamii, ndiyo ambao huweza kutamka na kuropoka kile walichoota jana usiku kwamba, kuna njama za kutaka kumuua. Inawezekana jana usiku mwanasiasa aliota kakabwa na jinamizi la usingizini, basi, anaamka asubuhi na kuambia umma yuko tayari kuuawa!

  Huu ndiyo ujumbe tuliopata baada ya JWTZ kutoa onyo. Jeshi lina dhima ya kulinda nchi kutoka maadui wa ndani na nje, Jeshi lina intelejensi yake (Military Intelligence), kwa mantiki hiyo, linapozungumza kuna njama za watu kuvuruga amani, huwa halikurupuki.

  Nilitegemea wananchi walipongeze jeshi kwa kuonyesha msimamo mapema na kutoa onyo kwa watu wanaotaka kuivuruga nchi. Unashangaa unaona wanasiasa wenye kuangalia madaraka badala ya Tanzania wanakurupuka na kulihusisha jeshi na mbeleko kwa CCM.

  Wapo wanaosema JWTZ imeenda mbali zaidi kwani hilo lilikuwa jukumu la jeshi la polisi, lakini wamesahau kwamba hatua ya jeshi kuchelewa kuchukua hatua ndiko kunakofanya nchi kuvurugika na damu kumwagika.

  Leo hii, watu wanalalamika uzembe katika kudhibiti mauaji ya halaiki ya Rwanda, kwa sababu Dk. Kofi Annan akiwa mkuu wa Ulinzi na Usalama wa UN, alishindwa kushauri umoja huo haraka kuzuia mauaji nchini humo.

  Kwa mantiki hiyo, JWTZ iko sahihi kuhakikisha amani ya nchi haivurugwi na maadui wa ndani au nje. Jeshi limekuwa sahihi kutoa onyo mapema kwa sababu hatuwezi kuruhusu umwagaji damu wa kutisha ndipo tuombe nguvu za jeshi.

  Amani na usalama wa nchi haufanyiwi majaribio. Amani, uhuru na umoja wa kitaifa unalindwa kwa nguvu. JWTZ imekaa katika nafasi yake husika.

  Nimestushwa kusikia kauli ya JWTZ ikihusishwa na mbereko dhidi ya CCM. Hili ni jambo la kipumbavu. Kwa nini CCM ikae kando wakati nacho ni chama cha siasa kinachopaswa kutii matokeo kama kikishindwa?

  Uropokaji huu wa wapinzani umezidi kuifanya CCM ionekane kama ni chama makini, kilichobobea katika siasa na kisichokurupuka. Ndiyo maana, ingawa chenyewe ni chama cha siasa, hakikutaka kukurupuka na kuirukia JWTZ.

  Kwani kinajua jeshi letu lina nidhamu ya hali ya juu, halijihusishi na mambo ya siasa za majitaka, lina nidhamu, utiifu na uzalendo.

  Hivyo, kudhani kauli ya JWTZ ni mbereko kwa CCM ni mawazo yasiyosadikika, na ni dhana tu isiyo na mashiko. Ni vema vyama vikaiga ukimya wa CCM.
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot](Source: RAIA MWEMA NEWSPAPER)[/FONT]
  Uropokaji huu wa wapinzani umezidi kuifanya CCM ionekane kama ni chama makini, kilichobobea katika siasa na kisichokurupuka. Ndiyo maana, ingawa chenyewe ni chama cha siasa, hakikutaka kukurupuka na kuirukia JWTZ."


  Kwa uelewa wako unadhani JWTZ lilitamka hayo likiwa ndani ya majukumu yalivyoanishwa ktk katiba? au kwa kuwa tu wanavaa magwanda basi wanayo haki ya kuropoka? kumbuka jeshi likivunja katiba linaweza kushitakiwa pia maana nalo ni legal person liko kwa mujibu wa sheria
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  sio wana siasa tu wengi wetu hata tusiosoma tumeelewa mantiki ya Shimbo. Need no degree to understand such crap. Tunajua yeye sio msemaji wa majeshi. Alikuwa wapi Cdf, Igp? mnadhimu wa jeshi kazi yake ni nini? Stop this crap. powet tillet na maduka ya jeshi ndio force behind
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  kama angetaka aeleweke ulivyotaka angepaswa kuwa clear zaidi na aseme hawajali hata ingekuwa ccm fisadis watashughuliikwa . Hakuthubutu na hiyo ndio taswira tulioipata mkuu
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  nchi hii amani itatawala na adhabu yenu iko tarehe 31 wananchi watakapoamua kwa kishindo kuwa ndio mwisho wenu

  tuungane kujikwamua sio kujikwamisha
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,135
  Trophy Points: 280
  ..kama Jeshi halikukurupuka, na kwamba military intelligence imebaini kuna watu wanapanga kufanya fujo, basi kilichopaswa kufanyika ni kuwakamata wahaini hao. sikuona mantiki ya Mnadhimu Mkuu Lt.Gen.Shimbo kutoa some vague statements.

  ..CCM imekuwa na ka-mchezo ka kuvitumia kisiasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. kama hamuamini waulizeni chama cha CUF. Lt.Gen.Shimbo alipaswa kuelewa ukweli huo, na kujiepusha kujiingiza ktk kusemea masuala ya kisiasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Inategemea kama kweli huyu mtu ana akili au la, maana siku hizi si siasa za majitaka tu hata uandishi pia upo wa majitaka. Wakuu naomba kujua kama kweli mtu unaweza kusikiliza matangazo ya radio kwenye ndege, nikiwa na maana matangazo ya Radio zetu hapa bongo na kwenye ndege zetu.

  Pia ningependa kujua kama kweli huyu mwenzetu ni mtanzania wa level gani, mwenye mtoto anayesoma chekechea mwenye uwezo wa kumsikilizo Shimbo na kujua hasa Shimbo anasema nini.

  Watanzania wengi wanajua kuwa Jeshi lilianzishwa lini na kwa malengo gani, na wengine wanajua wazi ni jinsi gani vyombo vyetu vya usalama vilivyowekwa mikononi mwa CCM. Kwa hiyo wengi pia wanafahamu Shimbo alikuwa anasema nini, na anajua anachokiona hapa Tanzania. Kama alaivyosema mdau mmoja hapa huhitaji digrii kujua Shimbo alikuwa anasema nini, kwa hiyo inawezekana mtoto wa chekechea wa mwandishi ana akili zaidi kuliko baba yake japo hana digrii wala elimu ya msingi.

  Mwandishi anazungumzia UZALENDO, anaweza kueleza Meremeta ina connection gani na jeshi? na uzalendo ulikuwa wapi wakati wa issue hiyo, au ndio uandishi wenyewe wa maji taka?

  Anazungumzia nidhamu, anajua kazi ya mtu kama Shimbo ni nini? mipaka yake ni ipi? na anajua kuwa watu walio kwenye magwanda Tanzania hawatakiwi kuingilia mambo ya siasa? Nidhamu gani anayoizungumzia??
   
 8. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umetumwa kutuletea hii thread yako mkuu? Naona kama hujaelewa pia kile kilichozungumzwa na wanasiasa majukwaani. Hata humu ndani tumepeana habari moto moto kuhusu Gr Shimbo kuhusu kashfa zake na uhusiano wa karibu na JK. Anyway unapiga kampeni kumsafisha huyo jamaa naona.
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mtu anayeleta vitisho majukwaani ni Kikwete. Bado nakumbuka aliyosema Dodoma wakati akizungumza na wana sisi m wenzake.
   
 10. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hehehe eti nilisikia nilipokuwa kwenye ndege, ndege hizi hizi tunazoambiwa tuzime simu za mkononi ili zisiingiliane na mawasiliano kati ya marubani na waongozaji au anazungumzia ndege za aina gani?
   
 11. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MKUU, Mwandishi hajabainisha kuwa alikuwa akisikiliza redio kwenye ndege, pengine alisikia kwa abiria mwenzake au kupitia gazeti alilolikuta kwenye ndege. Tusimhukumu kwa hisia zetu.
   
 12. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MKUU, Mwandishi hajabainisha kuwa alikuwa akisikiliza redio kwenye ndege, pengine alisikia kwa abiria mwenzake au kupitia gazeti alilolikuta kwenye ndege. Tusimhukumu kwa hisia zetu.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nilkuwa na mzee mmoja wa miaka kama 70 ivi tulikuwa twaijadili kauli ya Shimbo akasema toka azaliwe hajawai sikia JESHI/JWTZ kutoa tamko kama ilo kwa wananchi.
  Akangaka na kusema kuna walakini apo
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wewe Kishongo kweli umefulia, kwa nini unaleta habari kutoka Raiamwema na humtaji aliyeandika habari hiyo ? Unataka ionekane kama vile huo ndio msimamo wa gazeti tunaloliheshimu la Raiamwema kumbe ni mawazo tu ya mwandishi moja aliyechanganyikiwa. Huko wako wengi tu kama akina Maggid, acheni hizo.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu, Gen Shimbo hakupaswa kabisa kutoa kauli kama ile kwa waandishi wa habari. Pengine kuna taarifa za kijasusi zinazoonyesha uwezekana wa kufanywa kwa fujo baada ya uchaguzi, lakini busara ingekuwa kufanya maandalizi kimya kimya kutoa msaada kwa polisi pindi itakabidi. Jeshi lina heshima yake kubwa sana. Kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa kwa sababu ya uchaguzi kutaanza kulivunjia heshima. Tukumbuke mpaka sasa heshima ya taasisi nyingi nyeti imepungua kutokana na mitazamo finyu yabaadhi ya viongozi wake.
  Bado naamini kabisa jeshi letu lina kila sababu ya kuhakikisha hakuna umwagaji wa damu. Ila sikubaliani na dhana ya generals kwenda kwenye vipaza sauti na kuanza kuhutubia. They expose themselves unnecessarily.
   
 16. p

  p53 JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Mwandishi ameanza kwa kuzungukazunguka na kujifanya yuko neutral lakini katika umaliziaji ameshindwa kuficha hisia zake na hivyo kuonyesha rangi yake halisi.Mwanzoni ulinivuta kidogo na hoja yako,lakini baada ya kukusoma mpaka mwisho(hasa hapo nilipokoleza wino) nikagundua kumbe na wewe ni walewale tu.
   
 17. Bollo Yang

  Bollo Yang JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 440
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  JF bana, watu hawafichi hisia zako za kichama..ila mkumbuke kupiga kura sasa sio mnalalamika tu
   
Loading...