Ukweli kuhusu kafara ya kumwaga damu

1.Mungu anatakasa ili kumfurahisha nani wakati moto ni wake na mbingu ni yake ?
2.Nje ya damu huwezo wa Mungu kutakasa haupo ?
1.Ni utaratibu aliojiwekea yeye mwenyewe Mungu mwenyewe kwa watu woote aliowaumba kawawekea namna ya kuwa na uhusiano naye ndio kwa njia hiyo ya utakaso,Hafanyi kumfurahisha mtu yoyote anafanya apendavyo yeye
2.Ngoja tuone biblia inasemaje kama tunaweza kutakasika nje na damu ya Yesu,Efeso 1:7("Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake") 1Yohana 1:7 (bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote)
Wagalatia 3:13,Waefeso 1:7,wakolosai 2:15 ....
Vitabu vyoote hapo juu vinasema tunatakasika kwa damu ya yesu hakuna hata mahali kwenye biblia panasema tunaweza kutakasika nje ya damu ya yesu,kama wewe una andiko lolote ndani ya biblia linalosema tunaweza kutakasika nje ya damu ya Yesu liweke hapa,kama huna Basi amini katika utakaso wa damu ya Yesu
 
1. Kama Mungu ndio mpangaji mwenyewe anaamua atakavyo nakuuliza swali kama Mungu alipanga toka mwanzo kabla sijazaliwa mimi niende jahanamu nani anaweza kupangua ?
2.sawa nje ya damu ya Yesu , kumbe Mungu wenu hawezi kufanya utakaso , hili nimelichukua
 
Samahani mkuu, Sijaona yesu akisema kuwa damu yangu ni kafara ya hivyo unavyosema, na kama yy hakusema ni nani huyo mwingine mwenye mamlaka na nguvu ya kusema damu ya yesu ilikuwa kama ulivyosema? Mafundisho ya kumkadilia na kumzania yesu siyaelewagi. Yy hajasema na watu wanasema alifanya vile kwa sababu ya kitu fulani yaani kwa tafsiri ya utashi wa watu.
 
Kiongozi huwa ipo hivi.
HAKUNA kitu ambacho kina Nguvu kama Sadaka. japo sadaka yaweza kuwa ya Aina Tofauti kutokana na Dhumuni la Mtoaji.
lakini Moja ya sadaka zenye Nguvu ni hiyo Sadaka Ya kuchinja (Sadaka ya Damu).

lakini unapaswa kutambua,Sadaka huwa zinaweza kwenda sehemu kuu mbili inategemea na mtoa sadaka,Kwa jinsi ya Imani Yake na Misimamo Yake/Nia ya hiyo Sadaka na Manuizi.

1)Kuna sadaka ambayo huwa inatolewa na kwenda kwa Mungu Mkuu.

Hii Ni Aina ya sadaka ambayo,Watu Huitoa na kuipeleka, kwa Mungu Mkuu au wengine huwa wanasema Mungu mwenyezi/Wa Mbinguni.

Kwa kuwa umezungumzia sadaka ya Damu/kuchinja nitaigusia hiyo.

Sadaka ya Damu Ni Aina ya sadaka ambayo hupatikani kwa njia ya kuchinja na kumwaga damu or kukatisha uhai wa kitu chenye uhai na damu.
Ni Moja Ya Sadaka Ambayo huwa INAWEZA kutolewa kwa minajili Kama
-Sadaka Ya Ukumbusho au Alama.
hapa yaweza kuwa Ni ukumbusho wa jambo Kati yako na Mungu .
hapa tunaona jinsi Mungu alivyomuambia mussa wachinje wanyama na damu ya wale wanyama waweke kwenye milango yao Kama alama,pindi atakapotokea malaika wa kifo Basi nyumba zao zisipitiwe na Umauti.

-Sadaka ya Ma Agano/Agano
Hapa tunaona jinsi,Ambavyo Ibrahim baada ya kuweka agano na kuongea na Mungu aliweza kumtolea sadaka za kutekezwa na kuchinjwa Kama ishara ya Agano lake na Mungu.

-Sadaka ya Kujitakasa na Maombi
Hapa tunaangalia jinsi,wakati Taifa la Israel lilipokuwa limekosea au kukosa chakula walikuwa wanatumia Aina Hii kama ishara ya kuomba Toba na Kuomba kitu ambacho walikuwa wanakosa..Hapa tunaona story ya Eliya na wale manabii wa bahari kuhusu Toba na swala la KUOMBEA mvua iliyokata

- LAKINI Pia Ni Moja ya sadaka
Ambayo huwez kutolewa kwa minajili ya manuizo/Manuizi.Au Msaada
Hapa tunaona jinsi Ambavyo Mfalme baada ya kuzidiwa kwenye mapambano alinuizia na kusema kwa Mungu endapo atamshindia Vita,Kitu Cha kwanza kukutana nacho Basi atakitolea sadaka na bahati nzuri Vita Alishinda lakini too badly Mtoto wake alijitokeza wa kwanza so ikamlazimu kumchinja (kumwaga damu Yake).

Nakadhalika.

Lakini nifupishe Habari
Kupitia Gharama na mengineyo. coz hii sadaka ilikuwa ina hatarisha maisha ya watu lakini pia ilikuwa Ina gharimu Sana maisha ya watu.
Ndipo Mungu mwenyezi ikamlazimu amtume Yesu Kristo kwa ajili ya kufanyika kafara na kupitia kafara ya Damu yake pale msalabani Basi kila ambaye ataliita Jina lake atapata nehema na wokovu.kama ilivyo leo hii

Kuna sadaka ambayo hutolewa na kwenda kwa Lucifer na miungu mengine.
Hii inahitaji Umakini na uziada wa kuielewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ya Lucifer hujaeleza mzee ikoje
 
Kama Yesu alitolewa kafara basi iwe kwa wakristu tu. Hao wengine waendelee na kafara zao. Kafara ya damu (uhai) hasa binadamu ni siri kubwa ya mafanikio.
 
Ni.moja ya mawazo na maoni yako.

Japo hujasema wapi,nimedanganya

ila navyojua mimi.kupitia mauti ya msalaba hatuna hatia na haja tena ya kuchinja na kutoa sadaka.

isipokuwa kwa upande wa pili wale wanaotumia mali au wenye maagano na mashetani
mf.majini,waganga etc huwa wanatoa damu.
kupitia ajali, vifo fake etc

Sent using Jamii Forums mobile app
Truth
 
1.Ni utaratibu aliojiwekea yeye mwenyewe Mungu mwenyewe kwa watu woote aliowaumba kawawekea namna ya kuwa na uhusiano naye ndio kwa njia hiyo ya utakaso,Hafanyi kumfurahisha mtu yoyote anafanya apendavyo yeye
2.Ngoja tuone biblia inasemaje kama tunaweza kutakasika nje na damu ya Yesu,Efeso 1:7("Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake") 1Yohana 1:7 (bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote)
Wagalatia 3:13,Waefeso 1:7,wakolosai 2:15 ....
Vitabu vyoote hapo juu vinasema tunatakasika kwa damu ya yesu hakuna hata mahali kwenye biblia panasema tunaweza kutakasika nje ya damu ya yesu,kama wewe una andiko lolote ndani ya biblia linalosema tunaweza kutakasika nje ya damu ya Yesu liweke hapa,kama huna Basi amini katika utakaso wa damu ya Yesu
True
 
Sadaka hii inahitaji mwendelezo yaan ifanywe kila baada ya muda fulani tatizo linakuja babu yako. Kafanya na kafanikiwa na pia baba yako naye kafuata mkondo ule ule SASA tatizo linakuja kwa vijana wa sasa wamekuliaijini na hawajui na hapo ndo Damu inahitajika na huleta shida isipofanyika!
Dini za sasa zinakataza ila. Ule ni utamaduni toka enzi na enzi na isipofanyika huja na mabalaa mikosi kama vifo kufilisika na kutofanikiwa.
Fake
 
Tunaposoma kwenye biblia, kafara inatafsiriwa kama ishara ya utakaso na msamaha wa dhambi au kufanya mambo ambayo kwa hali ya kawaida haiwezekani isipokua kwa kumwaga damu .

Yesu alitolewa kafara, damu yake ikamwagika hili sisi tupone na tuondolewe dhambi na tutakaswe kwa roho mtakatifu, na ndio maana wakristo wengi wanaithamini damu ya Yesu .

Kinachonishangaza why Leo hii kafara zikitolewa kwa ajili ya kitu flani inaonekana ni dhambi kubwa sana na Jambo la kuogofya ilihali miaka iliyopita watu walikua wanatoa kafara kibao , za mbuzi ng'ombe kama sadaka za kuteketezwa?

Mungu mwenyewe alimwambia abraham amtoe mwanae wa pekee isaka kama Sadaka ya kuteketezwa ingawaje baadae aliingilia kati na kumkataza asimchinje mwanae na badala yake achinje kondoo

Swali ninalojiuliza, kuna siri gani iliyojificha nyuma ya kafara ya kumwaga damu ? Iwe ya mbuzi, kuku ,ng'ombe au binadamu. Kwa nini watu wengi wanapotoa kafara ya damu wanafanikiwa sana ? , kuna Siri gan iliyojificha nyuma ya kafara? Maana tu naona hata kwenye biblia miaka hiyo kafara zilikua zikitolewa na lilikua Jambo la kawaida lakini Sasa hivi ni haramu

Sent from my iPhone using JamiiForums
Swali zuri sana na kubwa sana. Kuna level mbalimbali za kujibu, ila level ya juu kabisa ni jambo la ajabu kujua na linahitaji ukomavu mkubwa mno wa akili na roho kuelewa, la sivyo sitapenda kabisa kumkwaza mtu. Kwa ajili ya watoto: kafara za damu hazihitajiki na Mungu na ni chukizo sasa, Yesu Kristo tayari alishafanywa "kafara" kwa ajili ya wote. Ukijua namna ya kuitumia kafara hii utaokoa maisha yako na ya wengi.
 
Samahani mkuu, Sijaona yesu akisema kuwa damu yangu ni kafara ya hivyo unavyosema, na kama yy hakusema ni nani huyo mwingine mwenye mamlaka na nguvu ya kusema damu ya yesu ilikuwa kama ulivyosema? Mafundisho ya kumkadilia na kumzania yesu siyaelewagi. Yy hajasema na watu wanasema alifanya vile kwa sababu ya kitu fulani yaani kwa tafsiri ya utashi wa watu.
Kuna sehemu Yesu anasema "Mimi ndimi njia kweli na uzima hakuna ajaye kwa baba..."
Hiyo nguvu Yesu anaitoa wapi, the whole future ya humankind iwe destined kupitia kwake.
The power of blood.
 
Kama YESU alishakufa msalaban hakuna haja ya kuwa na sadaka za kafara

Kwa maana kwa mtu mmoja (Adamu) dhambi na mauti vilipata kibali, lakini kwa mtu mmoja (Yesu Kristo) alifuta mauti na dhambi.

Tumekombolewa kwa damu ya Yesu ( Waefeso 1:7; Wakol.1:20; 1 Petro 1:19; Ufunuo 5:19), na si kwa vitu vihabikavyo kama fedha, dhahabu nk ( 1 PETRO 1:18 ). Hivyo, baada ya ujio wa Yesu tumepata ondoleo la dhambi kupitia damu yake, na ktk toba tunapata uponyaji (Zaburi 103:3).

Hivyo, itoshe kusema kwamba haikupasi kutoa sadaka yeyote kupata ukombozi. Kuna baadhi ya watumishi wanadai sadaka za ukombozi, ama sadaka za kuwatenga na laana au mabaya...hakuna kitu kama hicho.

Toa sadaka za kumshukuru Mungu, timiza nadhiri zako, toa mafungu ya kumi, malimbuko au sadaka za hiyari na mbegu...lakini sio kwenda kinyume na Isaya 53 hasa mstari 5 "kwa kupigwa kwake sisi tumepona", na 1 Petro 1:18 inayotueleza thamani ya damu ya Yesu.
 
Back
Top Bottom