Kuna uhusiano gani wa Damu na masuala ya imani katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaisha?

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
May 4, 2016
218
297
Maisha ya hapa Duniani yana siri nyingi sana na yanaonekana kuwa na uhusiano wa Moja kwa moja au niseme Connection na ulimwengu mwingine ambao ni wa siri sana yaani ulimwengu usio wa hadharani.

Katika imani nyingi damu imekuwa ikitumika kama kichocheo cha matatizo au kitatuzi cha matatizo. Kwa maana ya kwamba ili umkomeshe adui yako kupitia ulimwengu wa siri damu ya kiumbe hutumika ili kummaliza au kama una tatizo unataka litatuliwe basi damu hiyohiyo ya kiumbe hutumika.

Mathalani, kuna watu hutoa kafara za wanyama ili kufanikiwa kimaisha na wengine huenda mbali zaidi kutoa binadamu kabisa ili kufanikiwa ama kutajirika. Kafara za wanyama au binadamu huhusisha Damu. Na hii hata kwenye Biblia kuna maandiko mengi tu yahusuyo kafara jina lingine zikijulikana kama sadaka za kuteketezwa.

Lakini pia imani ya Kikristo inaamini Damu ya Yesu nayo ni Kitatuzi cha matatizo ya binadamu na ndio damu yenye thamani zaidi kuliko ya kiumbe chochote, yaani ni damu ambayo haihitaji damu nyingine yoyote ili kutatua matatizo au kufanikiwa kimaisha kwa ufupi DAMU ya Yesu Kristo katika imani ya Kikristo ndio Kafara kuu ama Sadaka kuu.

Sasa hapa neno kafara ni Sadaka ya Kishetani kwa mujibu wa imani za kipagani na Sadaka ni ya Kimungu lakini vyote huashiria Sacrifice.

Sasa mimi nauliza kwani huwa kuna uhusiano gani wa kiimani kuhusu Damu na utatuzi wa matatizo ya kimaisha?
 
Damu ni uhai na ni roho. Unapofanya sacrifice ya damu, unanuia na kuweka mapatano nayo (maagano) hivyo hio roho itafanya kazi kwa niaba yako kulingana na maagano iloweka.

Kama uliweka agano la kulipa kisasi, itafanya hvo,
Kama n mambo ya mali, inafanya n.k

Thats all
 
Kitu kizuri kuhusu sisi (Waafrica) ni kwamba tuna Elimu pana zaidi ya haya Mambo kuliko Sayansi na Teknolojia...
Na bado tupo nyuma kwa kila kitu

Mi nahisi, ni kwa sababu Damu ina chembechembe za "oyoli" ambayo inaweza kufungua milango ya kuzimu na kukuwezesha wewe kufanya unalotaka na likafanikiwa

Matajiri wengi wanatumia damu ya vichanga kutoa kafara, mfano Bill Gate... Inasikitisha

(Sarcasm)
 
Swali lingine : hapo hapo kwenye kutoa makafara ya damu.. Kwa nin mara nyingi kwa viumbe kama kuku, mbuzi , kondoo huwa mara nyingi wanapendelea rangi nyeus au nyeupe au nyekundu wakat kinachohitajika ni damu tu?
 
Wale wa kaskazini wanakunywa damu alafu Jumapili wanajaa makanisani wakiimba mapambio..ni sbabu ya wao kuinywa..upagani??
Kuna tofauti Kati ya maagizo na kuyafuata. Kwan wazinzi na waongo hatuingii makanisani?
 
Kuna tofauti Kati ya maagizo na kuyafuata. Kwan wazinzi na waongo hatuingii makanisani?
Uzinzi una uhai?...hiyo ni roho unaipandikiza ndani ya nafsi..ndio maana Kuna madhehebu Hadi kuongezewa damu ya mtu hawaruhusu...Wazungu hawaongezwi damu ya mtu mweusi nk
 
Uzinzi una uhai?...hiyo ni roho unaipandikiza ndani ya nafsi..ndio maana Kuna madhehebu Hadi kuongezewa damu ya mtu hawaruhusu...Wazungu hawaongezwi damu ya mtu mweusi nk
Nimezungumzia maagizo na kufuata kiongozi sijajikita kwenye impact yake
 
Uzinzi una uhai?...hiyo ni roho unaipandikiza ndani ya nafsi..ndio maana Kuna madhehebu Hadi kuongezewa damu ya mtu hawaruhusu...Wazungu hawaongezwi damu ya mtu mweusi nk
Ni kweli kabisa Mimi ndugu zangu wapo kwenye Moja ya madhehebu hayo shangazi yangu amekubali kufa kuliko kuongezewa damu.
 
Back
Top Bottom