kinachokufanya uihisi speed ya gari ni vitu vingi kwanza speed yenyew ya gari haipo costant, kuna wakati inaongezeka na kuna wakati inapungua so lazima utaihisi hiyo hali, pia gari inapita kwenye bara bara ambayo sio tulivu kwanza uwepo wa kona kona lazima wewe utazihisi, pia mashimo shimo barabarani yatakufanya uhisi kuwa upo kweny chumba kinachotembea.
Jiulize watu wanasafiri na ndege au meli wanawezaje kutembea ndani ya vyombo hivyo hali ya kuwa vipo kwenye mwendo? ni kwa kuwa vyombo hivyo vinakuwa vimetulia tofauti na magari....
sasa fikiria ukubwa hii dunia, wewe ni kajidude kadogo sana juu ya uso wa dunia yaan kadogo sana so huwez ukahis chochote kutokana na mwendo wa dunia, maana dunia ipo katika constant speed, na hakuna vizuiz vyoyote....