Ukweli kuhusu CHADEMA Iringa na uongo wa TUNTEMEKE

Ukweli kuhusu CHADEMA Iringa na uongo wa TUNTEMEKE

CDM ukweli ni mchungu kwenu???? Muige tabia ya wanaCCM kuwa wavumilivu

CCM sio wavumilivu ni waoga wa kufanya maamuzi. Na mnafaa mshukuru CDM maana bila mashinikizo yao msingefanya maamuzi kabisa mgeendelea kulala usingizi wa pono kama kawaida.
 
Mkuu tunashukuru kwa ufafanuzi wako ambao naamini TUNTEMEKE na timu yake utawapa ajira mpya ili kuukanusha. Ushauri: Angalia usalama wako maana mabosi wa TUNTEMEKE siku hizi wanaua kwa kutumia shoka. just be careful mkuu.
 
Mkuu heshima mbele!!
Tunashukuru kwa ufafanuzi uliokamilika na kwa wakati, tunawahakikishia tu kwamba tuko macho na tunaelewa mchezo unaofanyika hapa..

Wengine kwenye post zao wamekiri kwamba 'watawaaminisha watu kuwa Slaa si yule watu wamdhaniaye'- Waberoya.

Huu upuuzi unaoletwa hapa sisi wenye macho tanauona, na hapa tunafahamu kuana watu wanajiita hawana chama ambao literally ni vuguvugu na sisi wengine tulishawatapika siku nyingi!!

Tunangoja taarifa rasm ya CC toka mamlaka husika!!
:yo:

Sisi watu wa-Iringa tunamsemo huu "Na Ye Yaifwa yaigopa" maana yake ni. Hata inayokufa hutapatapa. So mpuuzeni maana ameshachinjiwa baharini kilichobaki ni kutapatapa.
 
CDM ukweli ni mchungu kwenu???? Muige tabia ya wanaCCM kuwa wavumilivu

Hakuna mtu mwerevu atakayeweza kuwa mvumilivu wakati wananchi wakipata taabu na mali za umma zinaibiwa. kama ndivyo unavyomaanisha, basi siku moja ukikuta ndani mwako kuna mwanaume tena kalala chumbani kwako ujitahidi hivyo hivyo kuvumilia mpaka jamaa amalize kazi yake na akiondoka nawe uingie. ikiwa utaweza kuvumilia kwa jambo hilo basi na mimi rasmi nitajifunza kuvumilia kama walivyo wanachama wa JIJINJEMU. Ahsante sana MAFILILI.
 
Allen anawezaje kuhoji maamzi ya kamati kuu huu ni utovu Wa nidhamu,Taratibuzi hazikufuatwa chiku badala ya kuwa msimazi Wa uchaguzi akageuka kushawishi wajumbe yeye awe mgombea aibu gani hii ,na allen baada ya kapwani shogaa yake Ameamua kuside na chiku ,Wanairinga msidanganywe na uhuni Wa Allen .Aleni urafiki wako na chiku umeanza lini?
Acha unafiki wako wanachama tunajivunia Katibu wetu na makini katika utendaji wake wa kazi.Wewew kama una dukuduku njoo kenye vikao vya nadani uje utueleze sio kupiga majungu kwenye mitandao.Chiku tofauti sana na warembo wengine,yeye yuko mageuzi mda mrefu ameonja shubiri nyingi za kupamabana na vyombo kandamizi vya dola.Halaafu wewe unatumia jina la bandia hiyo ni dalili ya uoga dhidi ya vyombo vya dola wache makamanda wafanye kazi.
 
Mkuu heshima mbele!!
Tunashukuru kwa ufafanuzi uliokamilika na kwa wakati, tunawahakikishia tu kwamba tuko macho na tunaelewa mchezo unaofanyika hapa..

Wengine kwenye post zao wamekiri kwamba 'watawaaminisha watu kuwa Slaa si yule watu wamdhaniaye'- Waberoya.

Huu upuuzi unaoletwa hapa sisi wenye macho tanauona, na hapa tunafahamu kuana watu wanajiita hawana chama ambao literally ni vuguvugu na sisi wengine tulishawatapika siku nyingi!!

Tunangoja taarifa rasm ya CC toka mamlaka husika!!
:yo:

Vip ritz na rejao ile thread ya waberoya anayeingia na id ya tuntemeke haikuwa na mshiko kwi! Kwi kwi kwi!!!!!!!

Hakuna raha dunia hii kama kumuwaza na kumuogopa mtu usiyemjua!! sasa mm hata majina yenu hayako kwenye database yangu!

Pangolin na Bukanga nataka nione u-great thinker wenu...maana inaonekana mnameza kila kitu!

nawauliza swali na ninataka jibu sasa hivi, ....kati ya yai na kuku kipi kilianza??
 
Haihitaji digrii au kusoma human saikoloj kujua kwamba huyu anayejiita kamandamakini ndie msigwa.. Kama huamini soma vizuri koments zake zote halaf konect tha dots.. Mkuu huo ni utoto na unafki.. Angalau Allen tumemjua kwa I'd halisi.. Why u hide ur tru id if u wanna pose allegations to the knwn one. If u spik facts and nt fictions disclose urself.. Athawaiz una lako jambo, na hufai hata kuwa baba wa familia huo unafki kwa kivuli cha kutojulikana
Mkuu taratibu Msigwa ni mchungaji.
 
Ni uvivu Wa kufikiri kuwa eti Mimi ni Msigwa kwa sababu nimemkosoa Allen ,Allen Jibu joja wewe ni mzigo ndani ya chadema Iringa .unachuki na Msigwa .nimekuuliza lini umeonekana hadharani ,kiongozi gani wewe kuwepo au kutokuwepo hakuleti tofaouti yoyote.upngozi ni impact ,wewe Huna hilo zaidi ya wivu na husuda dhidi ya Msigwa
 
Kweli leo nimestushwa sana na habari kuhusu kile kinachoitwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa. Ingawa habari yenyewe imeondolewa lakini madhara yake yatakuwa ni makubwa sana kama Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nikikaa kimya. Sijui kama huyo anayejiita TUNTEMEKE kama hata anajua ni kwa jinsi gani watu wanapambana kuuondoa mfumo mbovu uliopo.Tangu mwaka 2010 CHADEMA Iringa tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa MKoa kutokana na yule aliyekuwepo Benny Kapwani kujiuzulu Uenyekiti hapo tarehe 21/08/2010. Tangu wakati huo mpaka tulipofanya kikao cha baraza la Mashauriano Mkoa wa Iringa tarehe 25/02/2012 tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa Mkoa. Kwenye kikao hicho hatukuwa na uchaguzi kama inavyoelezwa bali wanachama walifanya uteuzi kwa mujibu wa Katiba kwani kikao hicho ndicho chenye mamlaka ya kuchagua viongozi wa ngazi ya mkoa. Wajumbe wa Baraza la mashauriano walipendekeza majina ya watu watatu kukaimu nafasi ya Mwenyekiti nao ni: Otmar .O. Haule, Chiku .A. Abwao na Thomas .S. Nyimbo.Isingekuwa rahisi kwa wote watatu kukaimu nafasi hiyo kwa hiyo wajumbe walipiga kura si kuchagua mwenyekiti bali kuteua miongoni mwa hao watatu nani anafaa zaidi kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi 2013 tutakapofanya uchaguzi wa nafasi hiyo kikatiba. Baada kura kupigwa Chiku Abwao alipata kura 59 na Thomas Nyimbo alipata kura 30 na Otmar Haule alijitoa kabla ya kura kupigwa.Kwa hiyo hoja ya TUNTEMEKE kwamba kulikuwa na fomu za kugombea nafasi hiyo si za kweli kwani si Chiku Abwao wala Thomas Nyimbo walioingia kwenye kikao kile wakiwa ni wagombea wala wanachama hawakuja kwenye kikao wakijua kuwa Abwao na Nyimbo ni wagombea.Na kikao kile cha Baraza la Mashauriano cha mkoa wa Iringa hakikufanyikia Makao Makuu ya Mkoa kama TUNTEMEKE anavyotaka tuamini bali kikao kile kilifanyikia Makambako kwenye Mkoa Mpya wa Njombe ambao kichama bado ni sehehmu ya Mkoa wa Iringa.Uchaguzi ule niliusimamia mimi mwenyewe kutokana na sababu za kiufundi wala si kwa utashi wangu mimi binafsi, CHADEMA hatuna kamati tendaji ngazi ya Mkoa badala yake tuna Baraza la Uongozi la Mkoa ambalo wakati huo lilikuwa halina Mwenyekiti. Kwenye kikao cha Baraza hilo ambalo Chiku na Msigwa ni wajumbe na wote walihudhuria (24/02/2012) ilikubaliwa kwamba niendeshe mchakato wa kuteua kaimu Mwenyekiti wa Mkoa ili kikao kiendeshwe na Mwenyekiti anayekubalika na wajumbe wa Kikao badala ya Baraza la Uongozi kuteua Mwenyekiti wa kuongoza kikao hicho.TUNTEMEKE ana chuki binafsi na DR. Slaa lakini ukweli utabaki kuwa hakukuwa na fomu za kugombea kwa hiyo kusema kwamba Dr. Slaa alimshawishi Chiku Abwao kuchukua fomu ni uongo uliopindukia na wala si kweli kwamba Peter Msigwa amewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa. Huu nao ni uzushi unaotakiwa kupuuzwa kwa nguvu zote. Labda TUNTEMEKE anaweza kutuambia ni lini Msigwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa na kikao kilichomchagua kilifanyikia wapi na uchaguzi ulisimamiwa na nani?Nawasilisha!!Allen Kilewella Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa
Mkuu ,Heshima kwako nashukuru sana kwaufafanuzi wako.Nakusihi sana utumie sana vikao vya ndani kwa kushirikisha wanachama wako.Nafasi hiyo inaweza kutumika vyema kujipanga kichama na kutengeneza uwezo wa kuendesha chama makini kama hiki.Mfano mzuri ni wa Mkoa wa Arusha wenzetu waliitisha harambee kubwa ambayo ni mfano wa kuigwa mikoa mingine.Tubone Kasaba
 
Ni uvivu Wa kufikiri kuwa eti Mimi ni Msigwa kwa sababu nimemkosoa Allen ,Allen Jibu joja wewe ni mzigo ndani ya chadema Iringa .unachuki na Msigwa .nimekuuliza lini umeonekana hadharani ,kiongozi gani wewe kuwepo au kutokuwepo hakuleti tofaouti yoyote.upngozi ni impact ,wewe Huna hilo zaidi ya wivu na husuda dhidi ya Msigwa

Mkuu pole sana na punguza hasira Ikiwa Allen afit kiongozi kunataratibu za kuondoa au kusubiri uchaguzi lakini hili la kumsema mwanachama mwenzako kwa maneneo ya dharau unakosa utashi wa uvumilivu, Rev Msigwa ni mchamungu na sifa ya kuwa mcha Mungu ni jinsi ya kufanyakazi na kuishi na wengine bila kwa amani na uvumilivu anakumbuka hata wakati wa Yesu wale mitume aliyowachagua baadhi walikuwa na mapungufu mengi tu ilifikia wakati wakwa wanabishana na kufokeana waokwa waolakini yesu aliwatumaini na kuwapa kazi ya kueneza evanjeli so na sisi tujufunze kuishi na wengine hata kama wanamapungufu wakati wake ukifika hakuna ovu ambalo halitakuwa wazi machoni.
 
Ni uvivu Wa kufikiri kuwa eti Mimi ni Msigwa kwa sababu nimemkosoa Allen ,Allen Jibu joja wewe ni mzigo ndani ya chadema Iringa .unachuki na Msigwa .nimekuuliza lini umeonekana hadharani ,kiongozi gani wewe kuwepo au kutokuwepo hakuleti tofaouti yoyote.upngozi ni impact ,wewe Huna hilo zaidi ya wivu na husuda dhidi ya Msigwa
Mkuu don't take it personal!!
 
Wale wanaosema kwamba mimi nina chuki na Msigwa wasome hili Bandiko langu na mengine yafuatayo ambayo niliandika tarehe 11/10/2011 kujibu hoja iliyoanzishwa na Member aitwaye Alexism kwenye thread yake yenye kichwa "Mbunge wa CHADEMA (Msigwa) atalipoteza Jimbo Kwa mwendo huu". Bandiko hilo litatoa picha kati yangu mim na kamandamakini nani Mkweli.

Mimi kama Kiongozi wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nataka kuweka wazi kwamba ni mapema mno kumpima Msigwa utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi kumi na moja tu.

Kwanza yeye alipoingia madarakani alikuta Mbunge aliyemtangulia kachukua mafaili yote ya Ofisi na kuondoka nayo nyumbani kwake.Ikumbukwe kwamba mbunge huyo, Monika Mbega (CCM) alikuwa ni Mbunge wa Iringa mjini tangu mwaka 2000 hadi 2010. Kwa maana nyingine ni kwamba Mbega ameondoka na taarifa rasmi za Ofisi ya mbunge wa Iringa Mjini za kipindi cha miaka 10.

Hivi Msigwa anaweza kujua ni miradi mingapi ilikuwa inasimamiwa na Ofisi ya Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita bila ya kuwa na kumbukumbu za kiofisi ambazo Monica Mbega ameondoka nazo? Kwa mfano ni vikundi vingapi vya uzalishaji mali vilifadhiliwa na ofisi ya mbunge na vilifadhiliwa kwa kiasi gani cha fedha.

Watoto na watu wengine walio kwenye mazingira magumu wamesaidiwaje na Mbunge aliyepita na wako kwenye hatua ipi. Mbega aliwasiliana na ofisi ngapi kwa niaba ya watu wa Iringa na aliwasiliana na ofisi hizo kwa lengo lipi. Hoja yangu hapa ni kwamba kabla ya kumbebesha mzigo mkubwa Msigwa ni lazima kwanza tumsaidie kupata nyaraka hizo muhimu za kiofisi ili aweze kuchapa kazi kiufanisi.

Ni kweli kwamba Msigwa ni mwenyekiti wa Iringa Mjini, lakini swala la Uchaguzi wa kata hizi za Gangilonga na Kitanzini ambazo tulipoteza tulifanya mkosa ya kiufundi kwenye kuchagua wagombea na jinsi tulivyoendesha kampeni zetu. Hakuna wa kumlaumu katika hili, kwani wote kwa pamoja tuliipoanza kampeni tuliamini kwamba tutashinda lakini hali ya mambo baadaye haikuwa upande wetu.

kushindwa kwetu kulitokana na makosa ya kiufundi ambayo hatudhani kama huko tuendako tutayarudia tena. Kitu pekee ninachokiona ni kwamba watu wengi wanafikiri kwa kupambana na Msigwa itakuwa ni rahisi kwao kuwa wagombea wa CHADEMA kwenye nafasi ya Ubunge hapa Iringa Mjini mwaka 2015.

Ushauri wangu kwao badala ya kuanzisha kampeni za kupakana matope na kujifagilia basi tumsaidie Msigwa ili ikifika mwaka 2015 wana Iringa Mjini waone tofauti kati ya mbunge wa CCM na wa CHADEMA. Tunaye diwani mmoja Bwana Nyalusi yeye naye aonyeshe kwenye kata yake ya Mvinjeni jinsi ya kuendesha utawala bora ili mwaka 2015 tuwe na cha kuwaonyesha wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Na hili pia ni ushahidi tosha kwamba mimi sina tatizo na Msigwa labda kama kamandamakini kaambiwa na Msigwa mwenyewe kwamba mimi nina Husuda na chuki naye.

Hizi dhana mbili kwa ukweli siziamini sana kwani zinawafanya wengine waonekane bora kwa wengine. Kusema kwamba kwa "beef" za CCM ndiyo maana Msigwa akashinda siyo kweli na ni kutaka kuwafanya wana Iringa Mjini hawajui ni nini maana ya mabadiliko. Bifu zao ni kichocheo kilicho wafanya wana Iringa waone kwa urahisi kwamba CCM hawako kwa maslahi yao na hivyo kuigeukia CHADEMA na Msigwa.

Duniani kote wananchi hubadilisha uongozi kutokana na makosa ya uongozi wenyewe. kama siyo sera za CCM kutofautiana na zile za CHADEMA unafikiri wana Iringa wangeichagua CHADEMA? Kulikuwa na mgombea mwingine wa nafasi hiyo hiyo ya Ubunge kutoka NCCR-Mageuzi, Mariam Mwakingwe. Mbona yeye hilo Bifu la wana CCM halikumsaidia kushinda? Ili uweze kumshinda mpinzani wako kisiasa ni lazima uka-pitalize kwenye makosa yake na ndivyo CHADEMA na Msigwa tulivyo fanya na wala si dhambi kisiasa.

Na hii dhana ya kuamini wana Iringa waliichagua CHADEMA kwa sababu ya wanachuo siyo ya kweli hata kidogo ingawa ki ukweli na wao wana mchango wao. Mwaka 1995 hapa Iringa kulikuwa hakuna CHuo Kikuu chochote kile lakini wana Iringa waliichagua NCCR-Mageuzi na Mbunge wake Mfwala Magoha Kibaassa. Hata wananchi wa kawaida ambao si wanachuo wanao uwezo wa kuchambua mambo na kufanya maamuzi sahihi ya kubadili viongozi. Sijui takwimu zinakuonyesha wasomi walikuwa wangapi kwenye uchaguzi wa Mwaka 2010 au ni asilimia ngapi ya wana Iringa Mjini wote.

Naujua na kuuthamini sana mchango wa wasomi katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yoyote ile, lakini sitaki mchango wao huo uwe ni kifungo kwa wengine. Kwa nini tusimhamasishe Msigwa kutembelea watu wake wote badala yake tuna specify kwa wasomi wa kwenye Contena la RUCO ambayo ni sehemu ya kunywea Pombe?

Wasomi waje na vitu Creative na Tangible kwa ajili ya manufaa ya watu wa Iringa halafu hapo ndipo tutaona mchango wao na tofauti yao na wananchi wasio wasomi ,na siyo kumshinikiza Mbunge awafuate kwenye Grocery zinazouza Pombe.
Iringa Mjini kuna Kata 16 na kote huko kuna watu na wanashawishiana wenyewe kwa wenyewe kufanya mabadiliko.
 
Last edited by a moderator:
Na hili pia ni ushahidi tosha kwamba mimi sina tatizo na Msigwa labda kama kamandamakini kaambiwa na Msigwa mwenyewe kwamba mimi nina Husuda na chuki naye.

Mkuu nimesoma post zako umeonyesha kwamba huna husuda wala chuki na Msigwa. Hapa ulikuwa unajibizana na Kamandamakini ila sasa unapoweka shaka kwamba labda kama kamandamakini kaambiwa na msigwa mwenyewe kwamba una husuda na chuki naye unakuwa humtendei Msigwa haki. Kama huma husuda wala vhuki naye huna sababu ya kufikiri kuwa MSigwa anaweza kumuambia Kamandamakini kwamba una husuda naye. Kauli zingine mkuu zinasababisha watu tujiulize ulize.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nawapongezeni viongozi kwa utekelezaji wa dhamana mliyopewa.haya ya tuntemeke ni upopombo na uhabithi ambao unamfanya aote kutokana na kivuli chake ambacho kitammaliza hatimaye.tuntemeke shame on you.
 
Mkuu nimesoma post zako umeonyesha kwamba huna husuda wala chuki na Msigwa. Hapa ulikuwa unajibizana na Kamandamakini ila sasa unapoweka shaka kwamba labda kama kamandamakini kaambiwa na msigwa mwenyewe kwamba una husuda na chuki naye unakuwa humtendei Msigwa haki. Kama huma husuda wala vhuki naye huna sababu ya kufikiri kuwa MSigwa anaweza kumuambia Kamandamakini kwamba una husuda naye. Kauli zingine mkuu zinasababisha watu tujiulize ulize.
Mkuu Kimbunga tatizo kamandamakini anaongea kama vile yeye ana authority ya kumsemea Msigwa na amesisitiza sana hiyo hoja yake kwamba mimi nina chuki na Husuda na Msigwa, ndiyo maana nikasema kwa uhalisia mimi sina kabisa chuki wala husuda na Msigwa labda yeye ambaye ameonyesha kama vile ni msemaji wa Msigwa atuambie siye wengine kwamba kama kuna siku Msigwa amemwambia kwamba mimi nina chuki naye. Ni ufafanuzi tu ndugu yangu.

Hii ndiyo Post yangu ya Mwisho kwenye mjadala huu. Nawashukuruni wote.
 
Last edited by a moderator:
Nilimfahamu Bw. TUNTEMEKE SANGA tulipokuwa Tabora High School miaka ya 1951/52 na alikuwa mtu mwema kweli kweli, mcha Mungu.

Inavyofahamika huyu Tuntemeke alikwenda America alipojizolea madegree na alirudi nyumbani mwanzo mwanzo wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere akatukuta tumeshapata nyadhifa za juu kidogo katika Serikali, na tumekwishaoa. Yeye alirudi na mke wa Kimerikani.

Tuntemeke aliingia katika siasa, nadhani; wakati huo wa TANU. Kwa bahati mbaya alifariki mapema (Mungu aiweke mahala pema roho yake).

Jina hili lililokuwa likiheshimika linatumiwa na huyu Mkinga muongo. Hata hajui taratibu zinazotumika ktk CHADEMA kupata viongozi wa muda.

Afadhali angeungana na huyu aliyetangulia kutumia jina "Tuntemeke" na kuwaacha wazalendo makini na jasiri kama Slaa, Msigwa na Chiku, kuongoza M4C kwa manufaa ya WaTz.

tumeshamjua aliyekuwa ana2mia hilo jina isivyo
 
Back
Top Bottom