Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

BTW: Wanafunzi wale walikuwa na sababu legitimate kabisa. hata katika chuo ninakofanyia kazi, tulifanya curriculum review tukaagiza Mathematics department inavyofundisha math kwa engineering ikumbuke kuwa sisi tunataka applications za mathematics, siyo abstract content ya mathematical theories. Kwa hiyo tumeweka guiedlines za kuhakikisha kuwa Math inawapa wanafunzi wetu tools za kusolve engineering problems, siyo tools za kuwa theoreticians tu. Wakati huo Engineering Math iliyokuwa inafundishwa kwa wanafunzi wetu FoE ilikuwa inaelekea kutayarisha mathematical theorists wa aina ya DEFINITION+THEOREM+PROOF; hata vitu basic kabisa katika vector analysis, differential equations, real analysis na compex analysis ambayo ndiyo ilikuwa core ya engineering math, vilikuwa vinatoweka. Kuna wakati walikuwa wakifundishwa Topology mahala pa Real Analysis, bila wao kujua kutokana na kuwa mathematicians wanaona Real Analysis kama sehemu laini ya Topology. Ila wanafunzi walipokosa msimamo basi waalimu tukawaachia wajijue wenyewe.
 
Nimekuambia kuwa sijui mliohusika katika mgogoro ule, ile post yako ya kwanza inaonyesha kabisa kuwa mligawanyika, na mgawanyo huo ulisababsihwa na watu wa aina yako, kwani kama kweli ulikiri kuwa test ile ilikuwa ngumu sana, nafikri ilikuwa ni kwenye complex analysis, na ukasema kuwa mwalimu alifundisha bila kuelekwa na akatoa mtihani mgumu sana katika muda mfupi sana kiasi kuwa hadi dakika ya mwisho hakuna aliejua la kufanya, hiyo ilikuwa ni sababu tosha kabisa wanafunzi wote muwe na masimamo mmoja. Lakini nyinyi mligawanyika. Bila kujali iwapo mgawanyo ulitokea dakika ya mwisho au dakika ya kwanza, ukweli kuwa mligawanyika, na kundi ulilokuwamo wewe baada ya katika mgawanyiko huo ndilo lilikuwa kundi la uvurugaji. Mambo yaliyokuja kutokea mwishoni baada ya kesi ni matokeo ya mgawanyiko mliouanza akina nyie.

Kichuguu,

Nashindwa kukuelewa unaposema tuligawanyika baada ya kutoka test. Mtihani wowote duniani una atakayeuona ni rahisi na mwingine atauona mgumu.

Siamini kwamba mimi nimekuwa wa kukufundisha hili kana kwamba ulikuwa hulijua. Mkimaliza mtihani aliyeuona mgumu na aliyeuona mrahisi kila mmoja anachukua ratiba yake binafsi.

Sijui utaelewa lini kwamba wote sisi ns G211 tumeonyesha kwamba hakukuwahi kuwa hata na dalili za kikao kuujadili ugumu wa test ile. Kama kungeitishwa kikao, basi tungegawanyika wakati wa debate, jambo ambalo ni la kawaid a duniani kote, na mwisho binafsi sijui tungetoka na resolution gani.

Hivyo point yako ya mgawanyiko si hivyo. Huwezi kusema leo form six wamefanya paper halafu mwanao kaiona ngumu halafu mtoto wa rafiki yako kaiona rahisi, eti sasa uka-conclude kwambaForm Six wamegawanyika na motto wa rafiki yako kachagua upande mbovu wa mgawanyiko.

Au labda hizi ndizo definition zilizofanya mjiite SPIRIT OF ENGINEERING. Maana kuna mwenzako kasema Wanachuo wengine ingekuwa vigumu kuielewa SPIRIT hiyo!

Kuhusu uliyoongezea kuhusu Prof Materu sina cha kueleza sana maadam chronologically umethibitisha kwamba nilisema sahihi kuhusu akina Prof. Materu kwangu sina maneno.
 
mimi wa kizazi hiki cha digital ingawa sijapitia chuo kukuu cha UDSM mpaka sasa naweza kujivunia mafanikio mawili matatu ya elimu yangu.haya nyie ma-G211 na ma-TRAITORS wa UDSM ya 1994 mnajivunia nini?i mean is there any positive impact alongside to what you have narrated before us?

Aisee,

Nyinyi mnaokuja na kusoma post mbili au tatu ndiyo mnasababisha turudie thread iwe ndefu. Narudia kwa kifupi kwamba sisi G72 au tulivyoitwa TRAITOR, binafsi na wala si kwa niaba yao ninajivunia kwamba tulii-shape Engineering kuachana na mtindo wao wa kupitisha matakwa yao kwa kuchapa wenzao mabuti au makonde au kwa kuwatupia viti au kuwakataza wenzao wasisome night study!

Engineering wenzetu hawa, hawakuacha kuleta matakwa yao miaka iliyofuata. Lakini sasa, walijifunza kujenga hoja zao vikaoni na zipo walizoleta zikapita na zipo zilizokataliwa.

Zamani kabla yetu haikuwa rahisi kuwakatalia, kwa sababu mkikataa basi mjue buti zitatembea Chuo kizima na eti hiyo wakaita ndiyo Spirit of Engineering!

Lakini tatizo ni kwamba wakitoka kule Chuoni mtaani wanakuwa peke yao na hakuna anayeogopa mabuti yao kwa sababu mtaani hakuna anayewajua na hata makazini.

Wale waliozama kwenye ugonjwa wa kutandaza buti, basi wanaishia kunyong'onyea na hoja zao kifuani maana hawakujifunza kujenga hoja bali walijifunza ubondia kupitisha matakwa yao.

Lakini waliojrekebisha na kuanza kujifunza kujenga hoja, eeh bwana wanajenga hoja utadhani wana PhD ya kujieleza.
 
Hebu soma tena historia uliyoandika hapo kuhusu matukio yalivyokwenda. Nilikueleza kuwa post hiyo ya kwanza, na ndiyo niliyosma tu, inakuwaka upande mbaya wa mgawanyiko huo. Wewe mwenyewe umekiri kuwapo kwa makundi mawili ambapo wewe unaangukia katika kundi ninalosema kuwa lilikuwa potofu. iwapo uliona mtihani ni rahisi lakini sehemu kubwa inalalamika na wewe umekiri kabisa katika mojawapo ya statements zao kuwa mtihani huo ulikuwa wa kuua, basi ni lazima utulie kidogo uangalie wengi wako wapi. Ingekuwa kuwa kila waliofanikiwa wangekuwa wanaendeleza interest zao; akina Nyerere (aliyekuwa na nafasi nzuri seriklini), mandela (aliyekuwa na biashara nzuri ya uanasheria) na wengineo wasingefanya waliyofanya. kama wewe ulikuwa ni kipanga ukawa umejihakikishia A, ni dhahiri kuwa iwapo mtihani fair ungetungwa bado ungepata A.

Anyway, mimi nilishiriki kwenye student politics za miaka ya themanini, ninajua hali ilivyokuwa wakati huo. Wakati Mwinyi anafunga chuo mwaka 1990 tayari nilikuwa ni Assistant Lecturer. Kwa vile wewe ulilaia the wrong side kwenye mgogor ule, ni afadhali ungeliacha hilo huko huko ukaangalia mengine ya maana kuliko kutumia muda mwingi kusimulia jambo ambalo linakufanya uwachukie class mates kwa mambo ambayo hana faida katika dunia ya leo. Nyinyi mliofanya mtihani na wale ambao hawakufanya mtihani huo mliishia kupata digrii sawa.
 
Japokuwa miaka hiyo nilikuwa bado kindergarten but nimeisoma hii story na kuielewa kiasi chake na ku conclude. SUBIRI JIBU ni traitor japokuwa mtu mzima, kitendo cha kuandika wenzako wafukuzwe chuo ni usaliti na umeonesha ulivyo selfish wa kiwango cha juu na sitoshangaa ukimuuza hata mkeo hali ikiwa tete, yaani kupata kaka au baba traitor hatari sana, wanaume huwa wanasimamia misimamo yao hata iweje...

kila mtu kaenda na begi lake chuoni, usipotoshe wenzio, alichofanya jamaa yeye kama yeye na wewe unamwita binafsi was right!
 
Wewe mwenyewe umekiri kuwapo kwa makundi mawili ambapo wewe unaangukia katika kundi ninalosema kuwa lilikuwa potofu. iwapo uliona mtihani ni rahisi lakini sehemu kubwa inalalamika na wewe umekiri kabisa katika mojawapo ya statements zao kuwa mtihani huo ulikuwa wa kuua, basi ni lazima utulie kidogo uangalie wengi wako wapi.

Kichuguu,

Kama Engineering tunge-apologise kwa kitendo cha kumtwanga makonde yule lecturer kwa ile spiriti yenu basi mithani ungekuwepo kama kawaida na hayo ya test itukutanishe yasingekuwepo.

Wingi ungejulikana kama kungekuwa na kikao cha kujadili test ambacho hakuna aliyekuwa na wazo nacho iwe unaowatetea au sisi.


Ingekuwa kuwa kila waliofanikiwa wangekuwa wanaendeleza interest zao

Wote hadi siku ya UE interest yetu ilikuwa moja tu, kufanya Unversity Exam, ya test wote tulishayasahau ila Maths waliokuwa wanataka kuombwa radhi.


ni afadhali ungeliacha hilo huko huko ukaangalia mengine ya maana kuliko kutumia muda mwingi kusimulia jambo ambalo linakufanya uwachukie class mates kwa mambo ambayo hana faida katika dunia ya leo.

Niliacha na jambo hili nilipotuma post ya kwanz. Post zilizobaki hadi kufikia hapo ni reply kuwajibu nyinyi mnaojitokeza wakati post zimeshafika zaidi ya 90.

Ungeosoma post zote ungeona kuna mwenzako nilimjibu kuwa kama hii thread si ya maana kuna redio nyingi, TV nyingi, magazeti mengi na vyote hivyo vina mambo mengi aachane na wanaoiona hii ni ya maana kwao aende huko aone kama tutamfuata.
 
Njooni,



Watoto hawa wanasoma JF na huwezi kuwazuia. Ni afadhali wasome wakaja kunieleza "Baba, kuna mtu mmoja kwenye JF anaitwa SubiriJibu nimeona anajibizana na classmates wenzako".

Ndiyo sababu tunaweka history sawa ili tusionekane wote tulikuwa wehu.

Maana unaendele kuweka kapuni ID yako ili watoto Wako wasitambue dingi Lao ni liTRAITOR.
Wewe ni traitor mkubwa kwani umejielezea vizuri kuwa barua yako ilijadiliwa kwa kirefu na hapana Dhaka ndio ilosababisha utawala wawasimamishe wenzako! Shame on you.
Hao wenzako wanakujua sana kwani walikuwinda mpaka ilesiku unaenda Posta kuchukua barua ya intimidation, na wakakupiga mkwara, ukaishia kupigilia msumari wa utraitor kwenye response yako chuo, sielewi mantiki ya kuufufua huu mjadala zaidi ya revelations, kwa kumalizia bora uweke jina lako wazi ili tukutambue kikweli.
 
Subirijibu: Sikutamani kuuendelea na thread hii kwakua kuendelea ni sawa na kumkimbiza kichaa aliyekuibia taulo wakati unaoga.... wengi watashindwa kugundua nani ni kichaa kati yenu... lakini kwa kuwa kichaa yule akuishia kuiba taulo tu alianza na kurusha mawe ... nimelazimika kutoka na kuwaalika watu ili kumfukuza na kumfunga kamba kichaa huyo ili asilete madhara mengi zaidi...

kwanza nasikitika kwamba umeamua kwa makusudi kukataa ukweli ulio dhahiri [ hali inayowezwa kufanywa na kichaa peke yake] kwamba ulikuwa na makosa kusaliti wenzako na kuwekt masilahi yako mbele hata pale tulipokubaliana kwamba tususie mtihani... si kweli hata kidogo kama unavyotaka JF ifahamu kwamba hakukuwa na makubaliano...ukweli ni kwamba baada ya mtihani kuchelewa bila sababu... wote tulikusanyika chini pale kwenye canteen na kujadiliana... msimamo ukiwa kuwa kwa kuwa tulikuwa na kila sababu za kususia mtihani basi tusifanye mtihani na kuwataka ma class reps wetu wakawaambie watu wa math dept na uongozi wa FOE kwamba hatatukuwa tayari kufanya mtihani huokwani umechelewa beyond time...
kama unavyodai kwamba hatukuwa na maamuzi yoyote kitu ambacho ni uongo mbona ukuchukuwa initiative za kufanya hivyo ama wewe ukuwa miongoni mwa watu waliona kuwa tuna hoja ya msingi... kama ulivyokiri na kujichanganya hapo juu kwamba mpaka dk 25 wewe bado uliamini kwamba tuwe na msimamo wa pamoja mbona ukuupigania....

Nakushauri acha kupindisha maneno kubali kwamba ulikosea nao ni uungwana...usianze ku justify tatizo kama ulivyofanya kwa kuendeleza league na walio wengi kwa kuanza kuwataja kwamba wali ku intimidate ... kweli wewe kwa umri ule ulikuwa mtu wa kulazimishwa nini cha kufanya... kumbuka kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu kwa hiyo baada ya kuona kwamba wengi wameridhia kutokufanya mtihani ulitakiwa ku base nao hata kama utaki hoja yao ndio demokrsia.... au wewe hapo unaponya kazi unalazimisha kila ulitakalo....

Pili: naomba uache mara moja kuwadanganya wana JF kwamba FOE walikuwa si watu wa kujenga HOJA na kwamba tulikuwa tunatumia mabavu kuliko hoja... kwa umri ule wa chuo ni nani angelubali kuacha kutetea hoja yake kwa kuogopa kupigwa na je ni wangapi walipigwa kwa kufanya hivyo.... huo ni upotoshaji wa hali ya juu... FOE tulisifika kwa kuwa na kauli ya pamoja na msimamo wa pamoja na hii ilitokana na tabia yetu nzuri ya kujadili jambo kwa manufaa yetu kabla hatujaenda Rev square... dept nyingine zilikuwa na wanachuo wachache na hawakuwa na umoja.. sisi tulijivunia wingi na msimamo wa pamoja na ndi maana tulionekana threat kwa wengine...

Katu umoja wetu na msimamo wetu usiubadilishe na kuwa tulitumia mabavu na nguvu ... mbona sheria za chuo zilikuwa wazi kama ni hivyo... basi wana FOE wengi wangekuwa wamefukuzwa kwa kupiga watu... kitu ambacho hakikutokea ... bali watu walifukuzwa kwa maandiko ya kinafiki ya watu kama nyinyi pale mliposhindwa kutetea hoja yenu ya woga na kuandika kwamba engineering ndio waliowaladhiumisha kugoma au kushiriki uovu....

sihitaji kuundelea sana na mada hii lakini ukinilazimisha nitakuletea mada nyngine nyingi unazopotosha ....

JARIBU KUJIREKEBISHA UTRAITOR HAUTAKUSAIDIA MAISHANI... KUMBUKA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU...
 
Ndugu Muonamambo; nakubaliana nawe kuwa mada hii haikuwa hata inahitaji kujadiliwa hapa JF, tena kwenye jukwaa la siasa. Ila kutokujibu baadhi ya madai ya mleta mada ilikuwa ni kama kukubaliana naye; nashangaa sana engineer mzima wa leo kuja kupiga propaganda za student politics hapa karibia miaka ishirini tangu tukio hilo la chuoni litokeee. Inaonekana atakuwa bado ana kinyongo na graduates wenzake; ni kama vile alitaka wao wasipate digrii kabisa, na kitendo cha kukuta kuwa wote waliishia kupata digrii sawa huenda bado kinamsumbua sana akilini hadi leo.

fact moja obvious ni kuwa wanafunzi wa engineering walikuwa na backing ya waalimu wao kue direction ya engineering math haikuwa sahihi; somo lilikuea linapoteza applied nature yake likawa ni more theoretical, na waalimu tulikuwa tumeshakubaliana kukutana na head wa math department kushauriana namna ya ufundishaji wa engineering math. Mgogoro na mgawanyiko wenu ulisababisha mashauriano hayo yasifanyike kwa ufanisi wakati huo ingwa tulifikia kuwa na waalimu wa engineering wakiendesha tutorials.
 
Sikutamani kuuendelea na thread hii kwakua kuendelea ni sawa na kumkimbiza kichaa aliyekuibia taulo wakati unaoga

Hata mimi sikutuamani kuendelea zaidi y aile post yangu ya kwanza. Lakini pia mkionekana mna uwezo wa kuleta post zaidi basi na mimi ninao.
Kama ni kuanzisha hoja nyingine wewe anzisha na hiyo ndiyo kazi ya JF na unaweza kupata wasomajo wengi kuzidi hii.


si kweli hata kidogo kama unavyotaka JF ifahamu kwamba hakukuwa na makubaliano...ukweli ni kwamba baada ya mtihani kuchelewa bila sababu... wote tulikusanyika chini pale kwenye canteen na kujadiliana...

Hebu panga uongo wako vizuri. Kama mlikusanyika ilikuwaje wengine wakutwe darasani. Kumbuka hata mimi kutoka nje si kwamba mlikuwa mmeita tukusanyike pale Canteen na wala mimi sikuja kuelekea Canteen. Nilitoka kwa sababu nione watu wanasemaje baada ya kuona Prof. Masenge na kina class rep hawatoki ofisini kwa Nzali maana exam room yetu ilikuwa moja kwa moja inatizamana na Dr. Nzali Room na kama ungesogea karibu ungeweza hata kusikia mazungumzo.

Tungekuwa vichaa kama tungeondoka wakati mazungmzo hayajaisha. Kama mlikutana Canteen basi kalikuwa ni ka-kikudni kamoja kati ya vijikundi vingi mlivyoamua kukaa siku hiyo wakati kuna kundi halikutoka kabisa darasani wakati wa sakata zima.

Kama mlifanya kwa niaba ya wote basi kwa nini hamkuzunguka madarasani na kote kuwaambia watu kwamba kuna msimamo fulani umetoka. Uongo mkavu.

msimamo ukiwa kuwa kwa kuwa tulikuwa na kila sababu za kususia mtihani basi tusifanye mtihani na kuwataka ma class reps wetu wakawaambie watu wa math dept na uongozi wa FOE kwamba hatatukuwa tayari kufanya mtihani huokwani umechelewa beyond time

Case iliyokuwepo mbele hadi wakati huo ni kitendo cha wanafunzi wa FOE kumfanyia vurugu yule lecture baada ya ile test. Usingeweza kumtuma class rep aende kujadili kuchelewa kuja kwa mtihani wakati wote tulijua sababu ya kuchelewa ni kwa sababu wahuni walimtwanga makonde lecturer na huo uhuni ndivho kilichokuwa item ya mazungumzo kati ya Dr. Nzali na Prof. Masenge.

kama ulivyokiri na kujichanganya hapo juu kwamba mpaka dk 25 wewe bado uliamini kwamba tuwe na msimamo wa pamoja mbona ukuupigania

Ni kweli nilikuwa nje kwa dakika 25. Lakini kwa sababu bado una ugonjwa wa kutosoma vizuri basi hata wanaJF wenzako wanakumbuka kuwa nimesema sababu yangu ya kutoka nje haikuwa kuwa na msimamo na nyinyi. Ilikuwa ni kutaka kujua nini kinaendelea.

Wakati napita kikundi hadi kikundi ili kujua ndipo ghafla Sweke, Karungubare na Kitilinga (Class reps) wakaja huku kauli yao ya kwanza ikiwa ni kwamba invigilators tayari wamo kwenye exam room na wanasubiri only 30 minute na hivyo wanatuasa twende.

Kauli ya pili ikatoka kwa wengine iksema "MBONA WENGINE HAWAPO" na mimi nikauliza kwa wameenda wapi wakati kila mmoja anajua mazungumzo yalikuwa mbioni na hayajaisha tena mazungumzo yanaongelea kuhusu uhuni wa kumtwanga makonde yule lecturer.

Uhuni wa kumtwanga lecturer makonde, na uhuni wa kuondoka wengine wakati dialogue inaendelea nisingeweza kuwa pamoja. Ukweli ni kwamba lecturer alifanyiwa vurugu na mimi nisingekubali kuwa kundi hilo hata kama kungekuwa na kikao. Na nyinyi wote mlijua yote hayo. Agenda yenu msingeweza kushawishi maana mngeita kikao huenda wapo ambao wangewapa live kwamba mlimtwanga makonde lecturer.

Hivyo, kila nilichofanya siku ile kilikuwa ni msukumo wangu binafsi na sijawahi kuujutia na badala yake hadi kifo changu nitausifia, na kila nikikutana na nyinyi ana kwa ana nitausifia.

... kweli wewe kwa umri ule ulikuwa mtu wa kulazimishwa nini cha kufanya...
Kwani kuwavamia watu wasifanye mtihani kwa kuchanachana mitihani yao si kuwalazmisha wasiyotaka. Kumvuta tai Mutungirehi na alipoanguka akatwangwa na viti siyo kulazimisha. Si hiyo ndiyo mnayoitw FOE SPIRIT kana kwamba mlienda University kuonyesha ufundia wa kupigana ubondia.

Pili: naomba uache mara moja kuwadanganya wana JF kwamba FOE walikuwa si watu wa kujenga HOJA na kwamba tulikuwa tunatumia mabavu kuliko hoja... kwa umri ule wa chuo ni nani angelubali kuacha kutetea hoja yake kwa kuogopa kupigwa na je ni wangapi walipigwa kwa kufanya hivyo.... huo ni upotoshaji wa hali ya juu

Je, mlijenga hoja gani kwa slogan yenu kwamba TRAITOR ASISOME MADARSA MNAYOSOMEA USIKU.
Hoja yenu ni ufundi wak kutwanga watu makonde na viti vikiwa karibu basi vinageuka kuwa silaha yenu ya kuwatupia mnaowachukia kama Benedict Mutungirehi.

Katu umoja wetu na msimamo wetu usiubadilishe na kuwa tulitumia mabavu na nguvu ... mbona sheria za chuo zilikuwa wazi kama ni hivyo... basi wana FOE wengi wangekuwa wamefukuzwa kwa kupiga watu... kitu ambacho hakikutokea

Ni sheria gani iliwaruhusu kuchanachana mitihani. Ni sheria gani iliwaruhusu kumvamia Benedict Mutungirehi.

Humu wametajwa Harold Mushi na wengine kadhaa ambao hatuhitaji ushahidi lakini Harold ndiye aliyetupa konde la pili kwa Mutungirehi.

Lakini ajabu Harold na yule wa kwanza kumvamia Mutungirehi hawakusimamishwa kama nyinyi. Yule wa kwanza simkumbuki ila tuliishe naye block moja pale Hall 1. Harold niliwahi kumsikia live akisimulia jinsi alivyojitetea alipoitwa kwenye Commitee ya akina Prof. Masenge na jinsi alivyoweza kukwepa na kukana kwamba hakupanda jukwaani kumchapa makonde Mutungirehi.

Kweli Harold Mushi hakupatikana na hatia! Na akamalizia hiyo 4[SUP]th[/SUP] year yake japo kuna mmoja humu amedai kuwa alikuwa 3[SUP]rd[/SUP] year.

Kwa nini ushidhangae hilo.

sihitaji kuundelea sana na mada hii lakini ukinilazimisha nitakuletea mada nyngine nyingi

Mimi binafsi sihitaji kuendelea na mada hii, maadamu tu msiendelee na juhudi za kupindisha hoja. Kama mtaleta hoja na tayari zimeshajibiwa humu basi sintakuwa na sababu ya kuzirudia kujibu bali nitajibu kama mtaleta uongo mpya.

Na kama hii itakuwa post yangu ya mwisho kuhusu hili basi ninashukuru kuwa sikutarajia thread ifike page hii na kupata watu 2,361 waliokwisha kuisoma hadi sasa.
 
Ndugu Muonamambo; nakubaliana nawe kuwa mada hii haikuwa hata inahitaji kujadiliwa hapa JF, tena kwenye jukwaa la siasa. Ila kutokujibu baadhi ya madai ya mleta mada ilikuwa ni kama kukubaliana naye; nashangaa sana engineer mzima wa leo kuja kupiga propaganda za student politics hapa karibia miaka ishirini tangu tukio hilo la chuoni litokeee. Inaonekana atakuwa bado ana kinyongo na graduates wenzake; ni kama vile alitaka wao wasipate digrii kabisa, na kitendo cha kukuta kuwa wote waliishia kupata digrii sawa huenda bado kinamsumbua sana akilini hadi leo.

fact moja obvious ni kuwa wanafunzi wa engineering walikuwa na backing ya waalimu wao kue direction ya engineering math haikuwa sahihi; somo lilikuea linapoteza applied nature yake likawa ni more theoretical, na waalimu tulikuwa tumeshakubaliana kukutana na head wa math department kushauriana namna ya ufundishaji wa engineering math. Mgogoro na mgawanyiko wenu ulisababisha mashauriano hayo yasifanyike kwa ufanisi wakati huo ingwa tulifikia kuwa na waalimu wa engineering wakiendesha tutorials.

Kichuguu,

Thread inapokuwa ndefu na inapata wasomaji wengi basi walaumu wasomaji na wanao-reply kama wewe.

hata wewe concern yako si sawa na wenzako. Wewe unaongelea ufundishaji wa Mathematics wenzako hakuna aliyeongelea hilo maana hakuna aliyelalamikia ufundishaji. Na hata ugumu wa test haukuwahi kuwa mjadala wa jumla. Hayo ni yako.

Hawakuchanachana mitihani kwa sbaabu ya ugumu wa test bali kila jambo tumeeleza humu. Tatizo lako umejieleza mwenyewe kuwa unasoma post chache tu za mwanzo ambazo wewe unaziita institutional.

Kama ni kunyamaza basi labda mimi ndiyo nianze maana mnarudia yaleyale niliyoeleza huku nyuma.

Ila acheni ubabe wenu wa pale FOE. Mkileta huku mtaani ubabe wenu wa kibondia kama pale FOE msidhani watu wataogopa kuwataja kwa polisi au mahakamani eti tu kwa sababu midomo yenu inajua kupindisha neno UCHOKOZI mkaliita UJASIRI na neno KUJIHAMI eti mkaliita TRAITOR.
 
Usipoteze muda wako kujaribu kuhalalisha mliyofanya kama wanafunzi wa engineering zaidi ya miaka kumi sita iliyopita. Let bygones be as they should be; haikusaidii lolote kujaribu kurudisha chuki mliyojenga baina yenu kama wanafunzi wakati huo. Kwa vyovyote ambavyo ungependa watu wajue, wewe ulihappen kuwa upande mbaya wa mgogoro ule, ingawa ndio upande uliokubalika na uongozi. Iwapo uliopingana nao wangekuwa upande mbaya wa mgogoro huo, mahakama isingeaumuru warudishwe chuoni, na wasipeta digrii zao pamoja na wewe. Tunafahamu kuwa kuna wanafunzi wenye filosofi imara sana kuamini kuwa yupo chuoni kwa sababu yake tu, na atafanya lile ambalo anaona lina faida kwake tu. Hiyo ddiyo filosofi uliyofuata wewe, na ilikuwa inatosha ubaki nayo moyoni mwako.
 
Usipoteze muda wako kujaribu kuhalalisha mliyofanya kama wanafunzi wa engineering zaidi ya miaka kumi sita iliyopita. Let bygones be as they should be; haikusaidii lolote kujaribu kurudisha chuki mliyojenga baina yenu kama wanafunzi wakati huo. Kwa vyovyote ambavyo ungependa watu wajue, wewe ulihappen kuwa upande mbaya wa mgogoro ule, ingawa ndio upande uliokubalika na uongozi. Iwapo uliopingana nao wangekuwa upande mbaya wa mgogoro huo, mahakama isingeaumuru warudishwe chuoni, na wasipeta digrii zao pamoja na wewe. Tunafahamu kuwa kuna wanafunzi wenye filosofi imara sana kuamini kuwa yupo chuoni kwa sababu yake tu, na atafanya lile ambalo anaona lina faida kwake tu. Hiyo ddiyo filosofi uliyofuata wewe, na ilikuwa inatosha ubaki nayo moyoni mwako.

Ubondia wenu mwisho wake ilikuwa ni pale mwisho wa geti za FOE? Tuliukomesha na sasa umebaki kuwa history. Tuliweka history ya kuwaadabisha na mkaadabika. Mlikuwa meshashindikana na mabuti yenu kama wanamgambo.
 
Kichuguu na Muonambali, huyu jamaa amejitambulisha mwenyewe. Ni traitor, Msaliti mkubwa. Kizuri ni kwamba nafsi yake bado ipo hai, haijafa. Ndio maana anahangaika sana kujisafisha. Kibaya ni kuwa ktk kujisafisha anachafua wengine kwa uongo wake. Anasema mwalimu wa Math tulimpiga mangumi, si kweli kabisa, nilikuwepo na kilichotokea tulimfuata mpaka Math dpt. Mwalimu mwenzake aliposimamisha watu kwenye ngazi 1st floor, waliochini wakauliza mmesimamishwa na Profesa nani ?? Yule bwana alikuwa na Masters tu akachukia kweli kweli. AMA kuhusu mgogoro mzima wa G211 MAHAKAMA KUU ilikwishaamua, nani anamakosa na nani anahaki, namshauri asome hukumu ile, asiporidhika akate rufaa. Asipotezee watu muda.
Pia nimkumbushe kuwa hakukuwa na G72, kulikuwa na G211 na MATRAITOR. yeye alichagua upande kwa haki akiwa na akili timamu kama anavyotushuhudia.
Wengi wa waliokuwa MATRAITOR sasa hivi ni watu safi tunashirikiana sana mtaani na kwa kweli watatu niliwaonyesha hii post wanamshangaa.
 
AMA kuhusu mgogoro mzima wa G211 MAHAKAMA KUU ilikwishaamua, nani anamakosa na nani anahaki, namshauri asome hukumu ile, asiporidhika akate rufaa. Asipotezee watu muda.

Mlipokuwa mnatufukuza kusoma kule FOE kwangu ndilo ilikuwa harrasment kubwa kuliko chochote. Na hiyo harrasment ndiyo ilikuwa utetezi wangu na case yangu kwenu kuliko hata ile kesi yenu na Chuo au kesi yenu na Mutungirehi pale Nkrumah.
 
Ubondia wenu mwisho wake ilikuwa ni pale mwisho wa geti za FOE? Tuliukomesha na sasa umebaki kuwa history. Tuliweka history ya kuwaadabisha na mkaadabika. Mlikuwa meshashindikana na mabuti yenu kama wanamgambo.

Mimi nili-graduate FoE mwaka 1987, nadhani ni takribani miaka kumi mbele yako. Mazinigira mliyokuta nyie tuliyatengeneza sisi kwa umoja wetu, ikiwa ni pamoja na uwepo wa pay ya kutosha wakati wa practical training, kuwepo kwa vifaa vya kutosha kuendesha mafunzo ya engineering kama vile scientific calculators (wakati huo zikiwa hazipatikani kwa urahisi) access ya computer kwa wanafunzi (wakati huo computer zikiwa ni za kuhesabu), drawing equipement za kutosha ambazo ziliwasidia sana wanafunzi wa mechanical na civil Engineering ingawa zilikuwa ni kwa wanafunzi wote wa engineering na vitabu vya kiada vya kutosha zaidi ya vile vya kirusi vilivyokuwa vimetafsriwawakati mwingine kwa lugha yenye makosa. Iwapo sisi sote wakati wetu tungekuwa upande wa aina yako, ungeikuta FoE ikiwa ni kama shule ya kata tu.
 
Kichuguu na Muonambali, huyu jamaa amejitambulisha mwenyewe. Ni traitor, Msaliti mkubwa. Kizuri ni kwamba nafsi yake bado ipo hai, haijafa. Ndio maana anahangaika sana kujisafisha. Kibaya ni kuwa ktk kujisafisha anachafua wengine kwa uongo wake. Anasema mwalimu wa Math tulimpiga mangumi, si kweli kabisa, nilikuwepo na kilichotokea tulimfuata mpaka Math dpt. Mwalimu mwenzake aliposimamisha watu kwenye ngazi 1st floor, waliochini wakauliza mmesimamishwa na Profesa nani ?? Yule bwana alikuwa na Masters tu akachukia kweli kweli. AMA kuhusu mgogoro mzima wa G211 MAHAKAMA KUU ilikwishaamua, nani anamakosa na nani anahaki, namshauri asome hukumu ile, asiporidhika akate rufaa. Asipotezee watu muda.
Pia nimkumbushe kuwa hakukuwa na G72, kulikuwa na G211 na MATRAITOR. yeye alichagua upande kwa haki akiwa na akili timamu kama anavyotushuhudia.
Wengi wa waliokuwa MATRAITOR sasa hivi ni watu safi tunashirikiana sana mtaani na kwa kweli watatu niliwaonyesha hii post wanamshangaa.

Kwa vile mimi nilikuwa mwalimu wakati huo na pia nilikuwa na shughuli nzito za research kwa ajili ya Ph.D yangu tukiwa na Dr Msekela ambaye alikuwa akifanyia research yake kati ya FoE na Sweden, sikuwa nahangaika sana kufuatilia politics za wanafunzi. Niliwahi kuwa active sana miaka ya themanini na nikawa nimeshazistaafu. Kwa hiyo matukio halisi ya wanafunzi sikuwa nayajua, ila ninafahamu kuwa mgogoro ule ulitupunguzia msimamo wa kukaa na math department kujadiliana nao namna ya kuimarisha ufundishaji wa somo lile kwa wanafunzi wa engineering. Katika mgogoro ule waalimu wa engineering wasiweza ku-side na upande wowote wa wanafuni ambao walishakuwa fragmented. Ila kwa kufuatilia stori aliyaondika jamaa huyu, inaonekana kabisa kuwa yeye alikuwa ni sehemu ya tatizo.
 
Iwapo sisi sote wakati wetu tungekuwa upande wa aina yako, ungeikuta FoE ikiwa ni kama shule ya kata tu.

Nasikia hata enzi zenu walokole walipata shida sana na baadhi walitishiwa kila mnapopanga mikakati. Sikutaka kuyasema haya jinsi unavyong’ang’ania mimi kutoshangilia makonde, kutwangana viti au tabia ya kuchachana mitihani tena ukiihallaisha, basi sina jinsi ila kukumbusha hata kama nilisimuliwa tu.

Ningesoma enzi zenu mimi ningeangalia hoja zenu na method yenu. Mngekuwa ushawishi ningewaunga mkono. Lakini mngekuwa mnatumia vitisho kama hawa, basi hata kama mngeleta hoja ya mimi kupewa urais wa Tanzania ningeikataa kama Dr. Slaa alivyokataa kwa kusema “Siwezi kuingia Ikulu kwa kumwaga damu hata ya mtu mmoja”.
 
Mimi nili-graduate FoE mwaka 1987

Msalimie Dr. Peter Chitamu. Nasikia ameshakuwa Proffessor. Chronology yake ya ku-graduate na kukaa FOE muda mfupi, na time ya kupata PhD ina tofauti ndogo mno na yako.
 
Back
Top Bottom