Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

Sweke was a great leader. Allisimama katika kile alichokiamini.sijamuona siku nyingi lakini naambiwa aliweka rekodi ya kuwa consulting engineer miaka Sita tu baada ya ku graduate. Sina hakika huwa anapita huku JF.
Subirijibu anahitaji uponyaji wa nafsi. Sote binadamu tuna mwili, roho na nafsi. Uponyaji wa nafsi ni mgumu na muhimu kuliko ule wa mwili na Roho. Tuendelee kumuombea.

JF ni kiboko!

Mfano, ukiudunda mwili wa Benedict Mutungirehi kwa magumi, mateke, mieleka na pia kwa kumtwanga na viti, si tatizo kwa sababu uponyaji wa mwili wake ni rahisi.

Nakupongeza kwa phylosophy hii. Ni kweli Mutungirehi alikimbizwa hospitali, mwili wake ukapata uponyaji huo, akapona kirahisi akarudi kuwa President of DARUSO hadi January 1995 tulipomuondoa kwa referendum.
 
Subirijibu, wewe ni TRAITOR unayeumizwa na u-kunguru wako hadi sasa. Hebu angalia hizi post zako mbili ulivyowajibu wachangiaji tofauti, nimezitoa page ya pili... halafu zilinganishe na narration yako kwenye post yako kuu, kama hutagundua unavyojichanganya kwa sbb ya uchungu wa miaka kibao, utakuwa mtu wa ajabu sana: "UNASEMA KUWA MLIBAKI FOE KUJIANDAA NA MITIHANI MINGINE. HUU NI UONGO MKUBWA UNAOWEZA KUSADIKIWA NA ASIYEJUA MAZINGIRA YA PALE SIKU ILE..." Nyingine hii hapa; "SHERIA ILIYOTULINDA NI KWAMBA MTIHANI UKIANZA NDIPO SHERIA YA DAKIKA 30 INATUMIKA. KABLA YA KUANZA HAKUKUWA NA SHERIA ILIYOSEMA TUITUMIE IWE KAMA HAKI YETU"
 
Subirijibu, maelezo yako yamekuwa ya kuvutia na yana mtiririko ambao hauwezi ukawa wa kulazimisha yaani kujitetea. Ni maelezo yanayoongozwa na dhati ya ndani kabisa vinginevyo ujasiri huu ungekuwa na kikomo. Maana umeandika sio haba.

Maelezo yako na uchungu uliokuwa nao ni dhahiri ulikandamizwa kwa kutotendewa haki, na haukuwepo uwanja wa kutoa maelezo kama ulivyofanikiwa kufanya. Umekuwa na bahati umeutumia uwanja huu vizuri na imeonyesha wahusika wengi wamepata upande wa pili wa shilingi bila kujali wamekuliana na wewe. Wasiokubaliana nawe usiwajali labda watakubali kesho au hata siku chache kabla ya kufa kwao lakini ujumbe umefikishwa, hii ni bahati sana.

Funzo nililolipata ni kwamba Watanzania walio wengi wamekuwa katika mazingira kama yako, wamekamdamizwa na marafiki zao wenye nguvu, wafanyakazi wengi wameumizwa na wafayakazi wenzio wenye madaraka na ushawishi mkubwa. Kwenye vyama vya siasa mambo ni kama hayo, kwenye makanisa yetu hali sio tofauti. Unaweza kugundua siri ya watu kuwa na hasira na chuki. Mkandamizo wa hivi ndio unaoleta vurugu katika nchi na katika taasisi mbali mbali.

Tujitahidi kujifunza kusikiliza,kusema kwa kiasi, tuepuke ukandamizaji kwa maana sio rahisi kujua mwenzio atumizwa kwa kiasi gani. Kusema ukweli wakati wote na tuepuke kila aina ya udharirishaji uwe wa kijinsia,kikabila na kidini. Maana maeneo haya yanaigusa nafsi ya mtu na maumivu yake ni makali sana.

Jamii forum pamekuwa mahali pakusemea ukweli, kutolea malalamiko na mawasiliano kutoka upande moja kwenda upande mwingine. Udumu jamii forum.

Juzi rafiki yangu kanipigia simu na kunitania kwamba Jamii Forum ndiyo inaongoza nchi. Nikabaki nacheka utani huo.
 
SubiriJibu Traitor wangu.
Kwanini unalazimisha.
G211 hatukumpiga Mutungirehi, wala tukiwa wanafunzi hatukumpiga yeyote.
Tofauti yetu na wewe sisi
Tulisimamia kile tulichokiamini.
Tulisema waziwazi na hatukumsengenya mtu.
Hatukumsaliti mtu kwa kuandika barua au kumshtaki kwa watawala ili aadhibiwe pasipo haki.
Hatukufurahia mateso ya mtu hata kama mitazamo yetu ilitofautiana.
Kwa sababu hiyo hatufurahii mateso yako ambayo ni dhahiri sasa.
Piga "moyo konde" SubiriJibu, maisha huku mtaani ni tofauti na shuleni, lakini
FORMULA ni ZILEZILE, kushirikiana na kupendana kwa dhati na KUTOSALITIANA.
Naendelea kukuombea, nakusihi pia uendelee kutuombea.
 
Juzi rafiki yangu kanipigia simu na kunitania kwamba Jamii Forum ndiyo inaongoza nchi. Nikabaki nacheka utani huo.

Ni kweli JF inaogopwa sana. Hapa nyaraka nyeti zinapatikana kabla hao wapelekewa hawajazipata.
Let's get back to mgomo 'kunji'.
 
SubiriJibu Traitor wangu.
Kwanini unalazimisha.
G211 hatukumpiga Mutungirehi, wala tukiwa wanafunzi hatukumpiga yeyote.
Tofauti yetu na wewe sisi
Tulisimamia kile tulichokiamini.
Tulisema waziwazi na hatukumsengenya mtu.
Hatukumsaliti mtu kwa kuandika barua au kumshtaki kwa watawala ili aadhibiwe pasipo haki.
Hatukufurahia mateso ya mtu hata kama mitazamo yetu ilitofautiana.
Kwa sababu hiyo hatufurahii mateso yako ambayo ni dhahiri sasa.
Piga "moyo konde" SubiriJibu, maisha huku mtaani ni tofauti na shuleni, lakini
FORMULA ni ZILEZILE, kushirikiana na kupendana kwa dhati na KUTOSALITIANA.
Naendelea kukuombea, nakusihi pia uendelee kutuombea.

Mimi mlinifukuza nisisomee darasani kwa kauli TRAITOR HARUHUSIWI KUSOMA NIGHT STUDY. Ni kweli hili mlilisimamia vizuri na hamkunisengenya. Mliniambia waziwazi nitoke na nisisomee FOE.

Hili sikuhitaji ushahidi na hasa hili ndilo nililoeleza kwenye barua ile tuliyopewa tujieleze. Na nilimtaja aliyetoa kauli hii ya kunifukuza, na kikundi chake chote kilichokuwemo kwenye ile room, alikuwa ni yule mkurya aliyekuwa Chemical Engineering na wenzake.

Ni kweli alisimamishwa japo wenzake niliwaona hawakusimamishwa.

Usiwafanye Chuo kuwa walikuwa ni wajinga kusikiliza ushauri wangu kana kwamba wao na akili zao zote hawakujua jinsi ya kuuthibitisha.

Mimi toka mpate haki yenu yaani kuadhibiwa kwa kusimishwa mwaka mzima, wala sina habari tena na hilo. Na hata sasa ninaliandika kwa minajiri ya historia na si vinginevyo.

Halafu nimekuwa nikisema kwamba mjipange mnapokuwa humu JF. Sijui kimewakumba nini hadi hamsikii ushauri wangu.

Hebu soma post namba 32 ya G211 mwenzako anasema hivi:

Umenikumbusha mbali sana!!
FoE was a place to be!! Traitors hawakupewa nafasi... na kweli Ma traitor mlikoma!!!
 
Its true, JF kiboko. Nimeisoma hii "tamthilia" kwa siku tatu!! Nikarudia na kurudia,
SubiriJibu habari za siku nyingi mtu wangu, Ma TRAITOR wengine hawajambo,??
Msalimie sana chalii wangu Babu L. Nasikia amekuwa mtu mkubwa pale EWURA
siku hizi. Tabia na misimamo yake shuleni, mtaani anakoishi na kazini "zinafanana
mno" na zako!:israel::A S-baby:
 
Mkuu umenikumbusha juu ya NIPASHE. Huyu alikuwa Faculty of Education aliitwa nipashe kwa kuwa alikuwa na masikio makubwa kama kikatuni kimoja cha nipashe kilichokuwa kinatoka kwenye gazeti moja. Nilikutana naye akiwa ni mwalimu tukaliga mvinyo tukikumbuka hiyo hadithi. Sweke nilikutana naye akiwa ni mhandisi kwenye kampuni moja ya ushauri (consultancy). Enzi hizo bwana sijui kama bado zipo; rejected democratically!

Naaam, kuhusu Nipashe. Huyu siku moja kulikuwa na tatizo la maji. Chuo KILINUKA kila kona. Hakuna kuoga. Hakuna Kuflashi! Basi, kunji lilipoitishwa Luhanga akaitwa Nkrumah. Akamtuma Mzee Mkude. Akabembeleza watu warudi madarasani. Basi Nipashe akaibuka kusema kuwa Chuo Kifungwe kwa sababu Wanafunzi hawajaingia darasani siku 3. Ila yeye kwa kuwa kasoma muda mrefu, wampe Diploma akafundishe kwa sababu Digrii ilielekea kumshinda! Kauli hii ilibadilisha hali ya tensheni na Mzee Mkude akacheka na Chuo hakikufungwa!
 
Mimi mlinifukuza nisisomee darasani kwa kauli TRAITOR HARUHUSIWI KUSOMA NIGHT STUDY. Ni kweli hili mlilisimamia vizuri na hamkunisengenya. Mliniambia waziwazi nitoke na nisisomee FOE.

Hili sikuhitaji ushahidi na hasa hili ndilo nililoeleza kwenye barua ile tuliyopewa tujieleze. Na nilimtaja aliyetoa kauli hii ya kunifukuza, na kikundi chake chote kilichokuwemo kwenye ile room, alikuwa ni yule mkurya aliyekuwa Chemical Engineering na wenzake.

Ni kweli alisimamishwa japo wenzake niliwaona hawakusimamishwa.

Usiwafanye Chuo kuwa walikuwa ni wajinga kusikiliza ushauri wangu kana kwamba wao na akili zao zote hawakujua jinsi ya kuuthibitisha.

Mimi toka mpate haki yenu yaani kuadhibiwa kwa kusimishwa mwaka mzima, wala sina habari tena na hilo. Na hata sasa ninaliandika kwa minajiri ya historia na si vinginevyo.

Halafu nimekuwa nikisema kwamba mjipange mnapokuwa humu JF. Sijui kimewakumba nini hadi hamsikii ushauri wangu.

Hebu soma post namba 32 ya G211 mwenzako anasema hivi:

Nia yako yaweza kuwa mbaya vile vile! Pengine hapa kuna mtu unamtilia kauzibe!! Mhhh, yote yanawezekana ukizingatia historia ina tabia ya kujirudia!
 
Ladislaus Malima ni mjasiliamali sasa!!!

Sina uhakiaka kama hupitia humu!!!
 
Peele,

Sikutaja jina katika post yangu na hivyo usihadaike kudhani kwamba ninalikubaliana na nyinyi kwamba mlisalitiwa.

Nimesoma thread nzima hivyo sihitaji kufundishwa conlusion toka kwako (kwenu) au kwa SubiriJibu.

Hebu wapashe mkuu,

Wao wameshatoa maelezo ambayo kwetu ilikuwa ni habari kwa sababu hatukuwepo eneo la tukio. Tumeyasoma inatosha kwa sisi pia kutumia bongo zetu ku-conclude.

Vinginevyo, utazuka ubishi wa kipuuzi ambao thread kwanza imeshatuchosha, halafu haitaisha kwa ujinga wa kutaka kuonekana nani alikuwa sahihi wakati maelezo tumewapa muda wa kutosha na hatukumpendelea mtu tumesikiliza pande zote mbili.

SubirJibu, Peele na washabiki wenu, hili limetuchosha na tumeshalielewa. Haki yenu ni maelezo. Conclusion ni yetu mnaotusimulia. Tafuteni topic nyingine za kutuletea. Imetosha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hutaamini Kweli Siku hizi wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa ...watetezi wa system na uozo.....wanafunzi kunatakiwa kuwa motoooo.....hata Kina Sita walimkosoa Nyerere
 
mtirirko wako mzuri sana hadi unakupa hamu ya kuendelea kusoma hadi mwisho bila kuchoka, uandishi mzuri sana!!
 
traitor mkubwa wewe,,,watu kama wewe ni kama Kipara, Bush, na Kiswaga......,Big up to G211

SubiriJibu,

Hakika move ya Kumng'oa Mutungirehi ilikuwa sahihi sababu aligeuka kuwa TRAITOR na mtetezi wa Cost Sharing phase 2. Hasa baada ya ile safari ya kuosha macho aliyopewa na Serikali.

Pamoja na Ugumu wa ajira hasa kwa wale wa kozi za Unguin ni dhahiri alikuwa amenunuliwa sbb alipewa ajira na Masters ESAMI na kuwa Team member wa Campaign Team ya Ben Mkapa 1995.

Ni jambo la kawaida kwa Serikali ya CCM kuwanunua watu Militant ili kuzuia mabadiliko. In Connection to this point make reference katika uteuzi wa Ma DC wapya-je ni wagapi walikuwa DARUSO Leaders and sell-out wamepewa zawadi ya cheo hicho kuanzia kwa Mkirikiti na wengineo? Hii ndio Tanzania chini ya CCM>
Mfano Ali Hapi ingawa tulimkataa mara mbili kua rais DARUSO
 
Back
Top Bottom