Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu Benedict Mutungirehi na kundi la G211 pale UDSM mwaka 1994

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Jun 29, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280

  Thread hii inatofautiana na ile nyingine ya kuuliza kuhusu aliko Benedict Mutungirehi, aliyekuwa mbunge na sasa hatujui yuko wapi.

  {https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/272844-mutungirehi%3B-mwanasiasa-mahiri-kazimikia-wapi-3.html}


  Nimeamua kuweka thread mpya ili wengi wajue chanzo cha matukio yale kwa faida ya historia.

  Unajua hata wengi hawafahamu relation ya vijana wale wa Engineering (FOE) na kundi lililomtoa Mutungirehi pale stejini. Haya ni makundi mawili tofauti yaliyounganishwa na ile nia ya kumuondoa Mutungirehi.

  Sakata ya Mutungirehi ilitokea mwishoni mwa October 1994, lakini ili uielewe vizuri inabidi uanze na matukio ya tangu April 1994 yaani miezi sita nyuma. Mimi nilikuwa namalizia first year pale Engineering na hivyo ninalikumbuka suala hili vizuri sana.

  Kwa nini nianzie nyuma vile? Ni kwa sababu ninataka kuweka hisoria sawa kwani baadhi wanapotosha na wanajifanya siku hizi ni wapiganaji kwelikweli.

  Tuanze sasa maelezo. Mwezi April 1994 nikiwa first Year pale FOE tulikuwa na somo linaitwa Engineering Mathematics ambayo ilikuwa inafundishwa na walimu toka Mathematics depertment. Wakati huo ndiyo amemaliza kufunidha topics ngumu kichizi kama vile divergence, curl na kadhalika.

  Kisha yule lecture akatoa test ambayo ilikuwa ngumu haina mfano kwani mtu unafika mwisho wa time hujafanya swali hata moja. Lecture akatangaza kwamba muda wa paper umeisha. Mimi nilikuwa nachukua Civil Engineering nimekaa karibu na Bwana anaitwa Mziray. Mziray akaanzisha fujo kwa kumshika lecturer asikusanye zile paper.

  Mziray simkumbuki jina lake la kwanza ila najua alimaliza Kibaha High School, May 1993, akaenda JKT Oljoro na akaja UDSM. Pale Kibaha alikuwa PCM na aliondoka na Dv. One Point 5 yaani ABB.

  Kwa watu kama huyu kudhalilishwa kuibuka na zero kwenye Mathematics ilikuwa kejeli lakini ukweli ni kwamba test ilikuwa ni ngumu.

  Fujo ya Mziray zikaungwa mkono na wengi tu. Yule mwalimu akarudi Maths Dept. na huko akashitaki kwa mkuu wake yaani Prof. Masenge kwamba kafanyiwa fujo na vijana wa Engineering.

  Kumbuka ile test ndiyo ilikuwa ya mwisho wa mwaka. Si kama siku hizi nasikia wanasoma kwa semester, wakati ule test ile ilikuwa ya mwisho na kilichobaki ni tutorials chache kusubiri Unversity Exam. Vumilieni hadi mwisho maana hadi hapa hakuna connection yoyote na Mutungirehi.

  Hivyo, Prof. Masenge akato quotion kwamba Mathematics dept haitafundisha tena Engineering students hadi wa-apologise. Engineering tukakataa kuapologise.

  April ikaisha May ikaingia. May ndiyo ilikuwa mwezi wa University Exams. Tukafanya exams zingine lakini binafsi nilishapata dalili za kugoma kufanya Maths Exam. Hili niliambiwa na Marehemu Dr. Nzali ambaye nilienda kumfuata kuhusu ugonjwa wangu maana niliugua karibu niage dunia hivyo nikawa namtaarifu kuhusu unafuu wangu. Akaniambia nisijaribu kugoma.

  Kesho yake ikafika yaani siku ya Mathematics Exam. Tukaingia madarasani lakini walimu hawakuleta mitihani. Wakati huo sheria ya chuo inasema kuwa zikipita nusu saa basi unaweza kutoka nje ya chumba cha mtihani na hakuna mwingine kuingia.

  Nusu saa ikafika, tension ya wanafunzi ikaanza kupanda maana walimu hawakuja na hivyo tutaonekana first year wote hatukufanya paper na hivyo tumeji-ABSCOND.

  Tukakubaliana kuwa tutoke nje tujadili cha kufanya. Sasa hapa ndipo vurugu ya kwanza ilipoanzia. Class representatives wetu ninaowakumbuka walikuwa zaidi ya watatu yaani Lugiko Mpelwa karungubare (Chemical Engineering), Sweke (Civil Engieer), Hussein Kitilinga (Electrical Engineer). Wengine nimewasahau.

  Msiomjua Karungubare ni yule aliyegombea uenyekiti NCCR akapata kura moja na James Mbatia akashinda uenyekiti huo. Karungubare sasa hivi ni mwanachama mzuri tu wa CHADEMA.

  Wakati tumekaa pale chini hawa ma-class reps wakaitwa kujadili kwa Dean of faculty. Kumbe huko kwa Dean tayari Prof Masenge yuko huko na yule lecturer aliyefanyiwa vurugu. Binafsi sijui walifikaje kule.

  Pale chini tumeshajadili na kuamua kwamba sisi hatujagoma kufanya paper ila wao ndiyo wamekataa kuleta mtihani. Basi tukakaa tukiwa hatujui nini kitatokea. Mitihani huanza saa 3 lakini hadi wakati huo tayari ni saa 5 mchana.

  Ikafika mahala kila mmoja akaamua kuchukua uamuzi wake. Wapo walioamua kuondoka na kwenda mabwenini. Wakaulizwa “hivi nyinyi mnaondoka mtihani ukiletwa si mtakuwa mme-DISCO”. Wakajibu “fanyeni mtakavyoamua”!

  Wengine wakaamua kujiandaa na mtihani wa mchana au siku nyingine na hivyo wakabaki madarasani.

  Ilipofika nadhani saa 5:30 kumbe yale mazungumzo ya Prof. Masenge, Clas reps na daen yamemalizika na hivyo Prof. Masenge na timu yake wakaamua kugawa paper ili mtihani uanze. Wakaenda madarasani wakawakuta wale ambao walitulia kujiandaa na subjects zingine. Prof. na wenzake hawakujua kuwa kulikuwa na mtawanyiko wakagawa paper na waliomo wakaanza mtihani.

  Class reps wakaiona hali hii na waka-panic na kuja kwetu ambao tulikuwa nje. Ninayakumbuka vizuri maneno ya Karungubare kwamba “Jamani ingieni madarasani mkafanya paper maana tayari wenzetu wameshaana na zinasubiriwa tu dakika 30 milango ifungwe tusiingie tulioko nje”

  Hapa ndipo likaanza sokomoko la mwaka. Binafsi nikataka kuhakikisha maneno ya Karungebare na ma-class reps wenzake. Tukaenda vyumba kadhaa. Kweli bwana wenzetu walikuwa wanafanya paper taratibu. Ingekuwa wote hatufanyi paper kwangu isingekuwa tatizo. Lakini tatizo ni pale baadhi walikuwa wanaifanya.

  Nikapiga kelele na wenzangu kadhaa nikisema “Jamani, tufanye moja kati ya mawili, ama tuwatoe kwa nguvu hawa wanaofanya paper ama tuingie na sisi tufanye”.

  Hakuna aliyejisumbua na huu ushauri wetu kwa sababu tulikuwa kama wanne tu kati ya kundi la watu zaidi ya 220. Nilipoona huu ni upuuzi nikatangaza “ni ujinga kusubiri na hivyo napanda ngazi kwenda kufanya paper nisije nikafukuzwa”. Nikaanza kupanda ngazi. Kumbe huyu Ladislaus Malima kanisikia na kuniona.

  Akanifuata amefura ajabu na kunisukuma akisema “Unajua wewe unacheza na Maisha ya watu, wale walioondoka utawafanya nini, unataka wafukuzwe”. Mimi nikajibu bila kujua kauli yangu imevutia wengi, nikasema “Wamekwenda wapi, si tulikubaliana tusiondoke. Sasa na wewe unasemaje kuhusu wanaofanya mtihani na hujawazuia”. Malima nikamzidi hoja na tension ikawa inazidi.

  Kumbe hata kundini mmojammoja akawa anachomoka na kwenda kufanya mtihani. Mimi pia nikapata nafasi nikaenda kufanya mtihani. Kumbe mtihani wenyewe ulikuwa mrahisi maana ndani ya dakika 30 nikawa nimeshanya maswali ambayo nimeshavuka passmark yaani 40%.

  Kumbe wakati tunafanya, kule nje dakika 30 zikawa zimeshapita na wakakubaliana kwamba waingie kwa nguvu kwenye vyumba vya mitihani, huko watatukuta sisi ambao kuanzia dakika hiyo tukaitwa TRAITORS, lakini wakubaliana wasitudhuru bali waichanechane mitihani ile ili ushahidi ukosekane unaoonyesha kuwa tulifanya paper na wao hawakufanya.

  Wakafanya hivyo. Lakini hawakujua wlaichokosea. Nilisema mwanzoni mtu kama mimi nilishajua tangu jana yake kuwa kungekuwa na harufu ya mgomo. Hivyo mtu ulikuwa ukiingia tu kwenye chumba cha mtihani kitu cha kwanza ilikuwa ni kuandikisha jina lako na signature. Hivyo fujo ilipoanza wale walikimbilia mitihani hawakujua kama huo ni ushahidi mwingine.


  Masenge na wenzake walichofanya wakachukua majina yote wakatoa photocopy ya majina ya wote tuliosaini, wakaacha copy kwa Dean of Engineering na original akaondoka nayo Prof. Masenge mwenyewe.

  Wakati Pro. Masenge anapanda kuondoka FOE grounds, mmoja wale wanafunzi akapata wao kwamba ushahidi wa list ya waliosaini hawana na anayo Masenge. Hivyo, akiondoka nayo wamekwisha. Wakaondoka kundi lote wakamzingira Prof. Masenge, wakamnyang’anya ile list ya majina na wakichanachana mbele yake.

  Terrible mistake hawakujua kuwa tayari kopi ipo kule kwa Dean. Hapa ndipo hawa wanafunzi 211 walipokosea na sijui kama walikuja kuligundua hili.

  Baada ya siku mbili, ikatangazwa list ya watu 72 na 211. 72 walikuwa ni sisi ambao tulifanya mtihani na tulitakiwa kuendelea kuwepo chuoni. Na wale 211 ni wale waliofanya fujo zile wakatakiwa kuondoka chuoni kwani walifukuzwa.

  Ndipo yakazuka majina mawili maarufu yaani G211 na TRAITORS. G211 walijiita hivyo kwa sababu mwaka mmoja nyuma bungeni kulikuwa na kundi la G55 la wabunge waliotaka hoja ya serikali ya Tanganyika iliyozimwa na Nyerere.

  Mimi kama na wenzangu 72 tukaendelea na Maisha ya Chuo. Wale G211 wakafungua kesi Mahakamani. Kundi la G211 lilikuwa na watu wengi sana. Nimeshamtaja Karungubare (CHADEMA), Sweke, Kitilinga ambaye sijui yuko wapi lakini mara ya mwisho alikuwa OTIS kampuni inayoshughulika na lifts za majengo.

  Wengine ni Phenihas Magesa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mwanza na mwaka 2009 aligombea ubunge jimbo la Busanda akashindwa na Lorencia Bukwimba wa CCM. Phenihas alikuwa kinara mzuri

  Kesi ya hawa ilendelea hadi nadhani mwishoni mwa September 1994 na wakashinda na wakarudishwa Chuoni. Wakaja huku tunaanza second year na wako very enthusiastic kukishinda Chuo. Hakika walitamba. Wakanunu T-Shirt zimeandikwa G211 kama ambavyo sasa zimeenea zilizoandikwa DHAIFU. Kurudi kwao ilikuwa fahari kwao na huzuni kwetu. Si huzuni kuwa tulipenda, bali walikuwa ni kero kila tulipopita.

  Tukakaa tumenuaniana yaani TRAITORS na G211. Faculty of Engineering au FOE second year tukawa katika makundi hayo mawili. Ninakumbuka siku moja nimeenda kusoma prep darasa moja wakaja wakanifukuza kwa sababu TRAITORS tulipigwa marufuku hakuna ku-study kule FOE.

  Hali ikadumu hivyo kwa nusu mwezi. Ndipo likaja sakata la Mutungirehi. Maadui wa Mutungirehi wakaona kundi pekee lenye uamsho na zuri kulitumia ni hili la G211.

  Kuanzia hapa wengi mnajua yaliyotokea. Mutungirehi akavurumishwa stejini kama thread moja inavyosimuliwa humu. Lakini players wakuu walikuwa ni hawa G211 ingawa wanachuo wengi walidhani ni vijana wote wa engineering. Si kweli, sisi tulioitwa TRAITORS hatukufurahia vurugu kwa Mutungirehi. Kilichofuata ni kufungwa Chuo kwa mgomo uliosababishwa na fujo hizi.

  Tukiwa huko nyumbani tukaletewa barua zenye neon liitwalo INTIMIDATION. Mimi ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na neno hili na ikabidi nifungue dictionary kulielewa.

  Sitaki kutaja nilipokea barua nikiwa mkoa gani. Lakini G211 nao walikuwa wamejipanga posta zote za miji mikubwa. Wakiona mwanachuo kaenda kupokea barua basi wanakuja na kufanya kavurugu kadogo ili wajue ulichoandikiwa. Walikuwa wameji-organise kama usalama wa taifa.

  Mimi nikaenda posta. Natoka kuchukua barua nikazungukwa na vijana wanne, wote ni katika kundi la G211. Wakata kujua barua niliyopokea. Kwa sababu nilikuwa mkoani na hatuko chuoni na mimi nikapata kiburi sikutaka kuwaonyesha nikawapuuza na kuwatishia kuwaitia polisi wakaachana na mimi.

  Nyumbani nikafanya masharti ya barua ile, kwamba kama nilitishiwa (intimidation) basi ni nani au kikundi gani kilitutishia. Mimi nikaona Mungu akupe nini maana ule mnyanyaso wa kuitwa TRAITORS tangu May 1994 hadi October 1994 nilishauchoka nikataja waziwazi kuwepo kwa kundi la G211 na jinsi walivyokuwa wakitunyanyasa kutufukuza hata madarasani kujisomea usiku (prep).

  Lecturer mmoja alinipa live kwamba barua yangu walii-discus at length.

  Mwanzaoni mwa December 1994 tukaitwa kurudi Chuoni, lakini Mutungirehi akiwa bado President of DARUSO. Effect ni kwamba wanafunzi zaidi ya 200 walisimiamishwa mwaka mzima wengi wao wakiwa ni wale G211.

  Ikaitishwa referendum kuchagua kuendelea na Mutungirehi regime au la na wengi wakachagua kuwa asiendelee na ukaitishwa uchaguzi mwingine.

  Siku moja nimekutana na Lugiko Mpelwa Karungubare akiwa CHADEMA, nikamkumbusha ule woga wake hadi akatuita tuingine madarasani akakataa kabisa kukumbuka.

  Ladislaus Malima aliyekuwa jasiri kunisukuma nisiingie kwenye mtihani mmeeleza kwenye thread nyingine kwamba alipopigwa mkwara kwenye mgomo wa Mutungirehi akanywea na wale wenzake G211 naye wakamuita TRAITOR.


  Haya ndiyo ninayoyakumbuka kuhusiana na sakata lile la wanafunzi wa Engineering { G211} na Benedict Mutungirehi. Samahani kwa Makala ndefu lakini imenibidi niyaseme haya.
   
 2. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,445
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Hii hadithi inatufundisha nini?
   
 3. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  User Tag List?????
   
 4. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kimbunga njoo mjadiliane na Classmates wenzako. Sisi UDSM tulipita enzi za kina Mtatiro na Mwita Mwikwabe. Hatuna cha kuchangia hapa.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mkaidi hafaidi.........
   
 6. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  we kumbe kunguru? aka traitor..duh watu hatari sana nyie
   
 7. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Traitor unajianika hivi?!!
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  Viva UDSM ...nowhere else you can have a such finest history in the exclusion of UDSM!
   
 9. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu SubiriJibu,

  Umenikumbusha miaka ile ya Dhahabu UDSM! Mutungirehi alichaguliwa kwa Kishindo kuwa Rais wa DARUSO late 1993 na kuwa TRAITOR wa Magamba baada ya kupta safari ya Uholanzi au Hungary mwenye kumbukumbu sahihi atasaidia.

  Siku ile aliposhushwa High table kuna kijana mmoja alisimama akasema " you were elected democratically ....now you are also rejected democratically " Nakumbuka kijana huyo then aliitwa NIPASHE. Najua Wakuu wengine kama Eliakim Maswi na Sylvester Sweke watakumbuka vema tukio hili. Sijui wamo humu au wanapita hapa?
   
 10. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  i like udsm ila cjasoma hapo kwa sasa ni hewa t wote hakuna kit magamba matupu
   
 11. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Mimi nilidhani baada ya miaka mingi mngekumbuka kupottoka kwenu lakini hadi leo mnadhani mlikuwa sahihi. Nimeeleza kwa kirefu na mengine mnaweza kuongezea.

  Kwanza TRAITOR humaanisha MSALITI wa jambo fulani mlilokubaliana kuwa ni la manufaa kwenye umoja wenu. Sasa turejee na matukio ya G211 na lile la kumuangusha Mutungirehi.

  Tukianza na G211 nafurahi hata nyinyi mmesoma story yote lakini sioni mkisema kuwa ni uongo bali mnasema tulikuwa ma- TRAITOR. Issue ilianza na kitendo cha Prof. Masenge kugawa mitihani kwa waliokuwa madarasani nao wakaanza kufanya.

  Katika mfululizo huu ulioanza tangu mwezi mzima, hakukuwa na makubaliano kwamba tusifanye mtihani au la. Badala yake ile asubuhi tulikusanyika kwa kutafuta solution nini kifanyike baada ya Prof. Masenge kugoma kutuletea mitihani. Hivyo issue ilikuwa mgomo wa Mathematics Dept kutunyima mtihani.

  Kumbuka tulipotoka kwenye vyumba vya mtihani ilikuwa ni kutafuta unanimous solution kwa sababu tulikuwa tuko in dilemma yaani hatujui tuchukue uamuzi gani. Kwa sababu hiyo tukaacha maamuzi mikononi mwa clas representatives (class reps) yaani Sylvester Sweke, Hussein Kitilinga, Lugiko Mpelwa Karungubare na mwenzao wa Mechanical Engineering nimemsahau.

  Hivyo, makubaliano ndiyo yalikuwa kwamba tusubiri information toka kwa class reps ndipo tujenge unanimous resolution. Nimesema kwenye story kwamba class reps walipokuja statement yao ya kwanza wakiongozwa na Sweke na Karungubare tena kwa woga ilikuwa ni kwamba tusipoteze muda twende tukajiunge na wenzetu kufanya mtihani la sivyo zikipita 30 minutes tutakuwa DISCO.

  Tizama kwa makini kitendo hiki cha class reps. Hivyo, statement hii ndiyo ilikuwa resolution ya kwanza kabisa ya class reps. Kumbuka wanasema hivi baada ya kuwa na mazungumzo ya masaa mawili kati ya Mathematical Dept, Dean of Engineering na Uongozi wa Students yaani class reps. Hivyo hicho walichotoka nacho ndihco kilikuwa makubaliano.

  Hoja iliyojitokeza ghafla na hakuna aliyekuwa ameitarajia ni suala la kwamba wale walioondoka na kwenda mjini au vyumbani itakuwaje hatima yao?

  Nimesema binafsi niliipinga hoja hii kwa sababu wao wenyewe walifanya ujeuri kwa kutujibu kwamba liwalo na liwe, mtihani ukija tufanye tutakalojua. Namkumbuka mmoja wao aliitwa Amos. Kuna watu humu wanadhani jibu la liwalo na liwe kalianzisha Mizengo Pinda.

  Hebu ona jibu kama hili, maana yake ni nini? Mimi hawa walioondoka ndiyo huwa ninawaita TRAITORS maana walikiuka makubaliano yetu kwamba tuwasubiri class reps watakuja na resolution gani toka kwenye mazungumzo na kina Prof. Masenge na Dean.

  Hii hoja mpya ilimshinda kila mmoja maana hoja ya kwamba wengine wameondoka ilijibiwa na hoja nyingine kwamba mbona wengine wamo wanafanya mtihani. Hivyo kulikuwa na makundi matatu: 1: walioondoka na kurudi mabwenini au offcampus, 2: waliobaki kusubiri class reps lakini wako nje ya exam rooms, na 3: waliobaki kwenye exam rooms.

  Kibaya zaidi ni kwamba engineer unatakiwa uwe na maamuzi ya haraka. Katika state kama ile mtu alikuwa anaangalia na kuona wazi jinsi dakika zinavyokatika basi na ku-ABSCOD kunakaribia na hakuna solution.

  Hapa ndipo G211 walipokosea tena maana wengine tulipoleta hoja kwamba haitawezekana baadhi wafanye paper wengine tusifanye watu wakabaki wanapigizana kelele pale nje badala ya kuchukua uamuzi mapema.

  Nakumbuka kuna lecturer (Dr.) mmoja tulizoea kumuita Boggy akaja akaanza kutushangaa na kusema "nyinyi vipi kama mnaingia kufanya ingineni kama hamtaki acheni". Nilikubaliana naye maana ukweli ni kwamba dakika zilikuwa zinayoyoma na hakuna resolution yoyote watu wanapiga kele ovyo kama wako Kariakoo sokoni.

  Narudia, hadi hapa huwezi kumuita mtu TRAITOR kwa sababu kila mtu alikuwa anapima mwenyewe hatima yake. Kila mmoja alikuwa amechanganyikiwa kivyake na hakuna uamuzi wowote wa pamoja.

  Baada ya kufika 20 minutes mimi nikaona ni ujinga kuendelea kusikiliza zogo hapo nje wakati hakuna resolution yoyote.

  Tatizo ni kwamba wale G211 waliporudishwa chuoni na Mahakama hawakujihangaisha kuishi pamoja na sisi tulioitwa TRAITORS na sanasana wakawa na mkakati wa kututenga kimaisha na kimasomo. Hivyo hawakutaka kabisa kujua kwa nini tulifanya paper.

  Lakini binafsi nilipata nafasi ya kuwauliza hasa wale ambao tulikuwa nje halafu tukaingia kufanya paper. Mmoja niliyemuuliza aliitwa James Kivugo aliyekuwa Electrical Engineering maana Electrical ndiko ilisemekana kulikuwa na TRAITORS wengi.

  Yeye na wengine walijibu kwamba waliingia kwa sababu waliudhiwa na kitendo cha watu kupigizana kelele ovyo pale nje bila kuchukua uamuzi wowote wakati muda unakwenda na dakika 30 zinakaribia. Sababu ambayo hata mimi niliwaeleza wazi na kwa ujasiri nikaondoka mbele ya kila mmoja kwenda kufanya mtihani.

  Hadi hapa ninasema kwa ujasiri mkubwa kwamba G211 walijitakia wenyewe, maana hadi nusu saa ilipoisha na sisi tumeshaingiz ndani ya exam room, hawakuwa na uamuzi wowote kuwa kifanyika nini. Hivyo, kila mmoja wetu aliachwa achukue uamuzi wake binafsi.

  Hata kesi waliyomshitaki Prof. Masenge na Chuo haikuwa na msingi kwamba kwa nini sisi tuliingia. Prof. Masenge alilaumiwa kuwa alichukua hatua gani kwa kukuta wengine hawamo darasani. Kosa la Prof. Masenge ni kuchukulia mazingira kwamba wamesusa kuingia darasani kufanya paper. Masenge hakujua kwamba wako nje kwa sababu kuna wajeuri walikuwa wameondoka kabisa maeneo ya chuo hasa off-campus.

  Masenge alilaumiwa na mahakama kwa sababu hakujiridhisha na sababu za wengine kuwa nje maana kuwa nje kuna sababu nyingi ikiwemo hata ugonjwa wa ghafla na sikugoma pekee kama alivyidhani au alivyowasilisha maelezo.

  Nadhani nimemaliza kuhusu propoganda ya uongo ya kuitana TRAITOR wakati TRAITOR anafahamika ni nani. Propganda iliyoenea miaka mingi.

  Tuje kwenye suala la kumuangusha Benedict Mutungirehi, Rais wa DARUSO. Nalo ni kama lile la G211 na kama mnakumbuka siku hiyo hawa G211 walikuja kwa wingi pale Nkrumah na fulana zao zilitanda kule Balcon. Hebu tafakari, kama haikuwa imepangwa kumuangusha Mutungirehi kwa nini mfululizo wa matukio uwe vile?

  Tuje kwenye tukio lenyewe. Siku ile tulizoea kuiita Baraza maana ndipo kwa mara ya kwanza tunakutana all students kwa sababu Chuo ndiyo kimefunguliwa. Je, agenda ilikuwa ni nini?

  Hakukuwa na public agenda kwamba wote sasa tunaenda kumuondoa Benedict Mutungirehi.

  Ni kwamba zilipoanza kusoma agenda wakapewa sasa students waanze kuongea based on those agendas. Akaja huyo kijana mliyezoea kumuita Nipashe mwenye moustahce mrefu akasema kuwa "his intention was to change the agenda". Kwamba Agenda sasa si zile zilizoletwa na tulizozijua bali agenda sasa ni management ya Benedict Mutungirehi. Huku nyuma G211 wakashangilia sana kule juu walikokuwa huku ushangiliaji ukiongozwa na Phenihas Magesa na Ladislaus Malima. na Raymond Richmod aliyekuwa TBL Mwanza.

  Baada ya huyu NIPASHE akaja Harold Mushi naye akaongea huku akimlaumu sana na kumnyooshea kidole Mutungirehi. Harold akamaliza kisha akaja kumalizia mtu mwingine naye aitwaye Mushi, huyu akamalizia kwa kusema "Mutungrehi amekuwa na kiburi sana, tumemtafutia mke wa kumshauri lakini bado hajirekebishi".

  Ilipomalizika kauli hii akatokea kijana mmoja akapanda kwenye stage huku akiwaita wenzake waje pia. Akaenda mbele ya Mutungirehi na akamvuta ile tai na ngumi zikaanza pale kati ya Mutungirehi na wale waliomfuata. Achaneni na Mutungirehi, anajua kuzicheza karate na ule urefu wake! Aliriusha karate mbili tatu na wasingekuwa wengi anewato nje.

  Fujo zilipozidi akaotokea Gasper Tracers aliyekuwa 4[SUP]th[/SUP] year Electrical Engineering akaanza kwa kumrushia kiti Mutunigrehi aliyekuwa ameanguka chini. Gasper Tracers ni Engineer wa ITV kwenye mwaka 2007 sijui yuko wapi sasa.

  Viti vilipoanza kurushwa, pembeni ya Mutungirehi alikuwepo Katibu wa DARUSO wakati huo yaani Godwin Ngwilimi ambaye hadi mwaka jana alikuwa Mwanasheria wa Vodacom na sasa ni Mwanasheria wa TANESCO na aliwahi kujadiliwa humu kuwa inawezekana kaletwa TANESCO kwa influence ya Rostam Aziz.

  Ngwilimi alipoona bosi wake yaani Mutungirehi kaanza kutupwa viti na yeye akaanza vita ya kuwatupia viti wale wagomaji. Ndipo wale waleta fujo wakashindwa na Mutungirehi akapata watu wa kumtoa na kumpeleka hospitali.

  Sasa, tujadili tuko hili, kama hazikuwa fujo zisizo na msingi, ni wapi kulikuwa na maandalizi ya jumla kwa ajenda ya kumtoa Mutungirehi?

  Engineering ambao tulikuwa vinara wa kukusanyika Revolutionary Square mbona hawakukusanyika mapema ili tujue tuhuma kuhusu Mutungirehi ili tukiingia Nkrumah tumuondoe kwa demokrasia na si kwa vurugu kama vile.

  Naona humu kuna watu wanachangia kwa kusema eti aliondolewa pale Nkrumah kwa demokrasia. Nimesema waliochangia walikuwa ni wa tatu na hata yule wa tatu hakumaliza fujo zikaanza za kupigana na high table. Je, hiyo ndiyo demokrasia?

  Ukweli ni kwamba ilikuwa ni vurugu ya kihuni kama ilivyokuwa ile vurugu ya G211 maana zote msingi wake ni agenda ya iliyofichika inayojulikana na kikundi cha watu kadhaa bila ya makubaliano ya mapema.

  Ndiyo maana hadi leo ninasikia fahari kuwataja wale waliosababisha zile vurugu hadi waliohusika kumpiga Mutungirehi.

  Baadhi nimesema sasa ni wanachama kwenye vyama vyetu vya siasa. Phenihas Magesa ni Mwenyekiti wa CHADEMA pale Mwanza. Uchaguzi mdogo wa Busanda ile May 24, 2009 almanusura angeukwaa ubunge kama angemshinda Lorencia Bukwimba.

  Sikuwa najua kwamba Phenihas Magesa amekuwa mwanasiasa tena wa CHADEMA. Binafsi ninavyomjua kama bado ana tabia zilezile basi hakika hili bunge hawa akina John Mnyika, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Ezekiah Wenje wote naweza kusema ni cha mtoto. Naamini kungewaka moto na hii miongozo ya Anne Makinda.


  Lugiko Mpelwa Karungubare bado yuko CHADEMA kama Phenihas. Hivi huko waliko waheshimiwa hawa ni kweli bado wana character yao ya kutaka maamuzi yapitishwe kulingana na dhamira zao zinavyotaka au kulingana na uamuzi wa kidemokrasia uliokubaliwa na wengi?

  Ninavyoijua CHADEMA ilivyo makini sidhani kama wanapewa nafasi ya kuleta vurugu kama zile za UDSM mwaka 1994/95.

  Kama wamekuwa wanademokrasia basi ni wazi kila wanapokumbuka tukio la Mutungirehi na lile la G211 ni lazima walione kama ulikuwa ni utoto wa mawazo ambao Prince Bagenda aliwahi kuandika kwamba vyama vya upinzani vilivamiwa na siasa za vyuoni.

  Sina ushabiki na Bagenda lakini nilipmsoma kwenye comment hii huwa ninakumbuka utoto kwenye matukio ya G211 na lile la Benedict Mutungirehi.
   
 12. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Sweke anaendesha kampuni yake ya construction lakni ninavyomjua si mpenzi sana wa kupita humu JF au mitandaoni.
   
 13. Q

  Quick Senior Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  traitor mkubwa wewe,,,watu kama wewe ni kama Kipara, Bush, na Kiswaga......,Big up to G211
   
 14. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 15. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Ninachoshukuru hata jamii ya wanaoangalia hii thread wamejua wazi hamkuwa na point na inawezekana hamtakuja kuwa na point ya kueleza zile vurugu zenu za ki-ujana kama si ki-utoto.

  Nimeeleza kwa kirefu chanzo cha mzozo. Bahati nzuri si wewe hata waliochangia mwanzoni wanaopinga maelezo yangu.

  Wote mmekazania neno moja tu yaani TRAITOR lakini hadi sasa imepita miaka 18 na hata siku moja hamjaeleza ni nini kilichosalitiwa (TRAITED).
   
 16. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  SubiriJibu,

  Hakika move ya Kumng'oa Mutungirehi ilikuwa sahihi sababu aligeuka kuwa TRAITOR na mtetezi wa Cost Sharing phase 2. Hasa baada ya ile safari ya kuosha macho aliyopewa na Serikali.

  Pamoja na Ugumu wa ajira hasa kwa wale wa kozi za Unguin ni dhahiri alikuwa amenunuliwa sbb alipewa ajira na Masters ESAMI na kuwa Team member wa Campaign Team ya Ben Mkapa 1995.

  Ni jambo la kawaida kwa Serikali ya CCM kuwanunua watu Militant ili kuzuia mabadiliko. In Connection to this point make reference katika uteuzi wa Ma DC wapya-je ni wagapi walikuwa DARUSO Leaders and sell-out wamepewa zawadi ya cheo hicho kuanzia kwa Mkirikiti na wengineo? Hii ndio Tanzania chini ya CCM>
   
 17. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ndugu subirijibu.... Nimesikitishwa sana na ujasiri wa kutetea uwoga wako na utraitor wako... mimi ni miongoni mwa G211 na ni mmoja wa viongozi tuliongoza kundila G211 NA KUSHINDA KESI DHIDI YA CHUO... Naikumbuka sana historia hii na haitakuja kutoka kichwani pangu.... sina haja ya kurudia historia nzima hila napenda kukufahamisha haya machache kwa faida ya wana Jf na kuweka kumbukumbu sahihi..
  1. Tuna kila sababu ya kuwaita nyinyi matraitor kwa sababu .... sheria za chuo zilieleza wazi kwamba mtihani ukichelewa au mwanachuo akichelewa kufika kwenye chumba cha mtihani kwa zaidi ya dk 30 hataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na vilevile mtihani ukichelewa kwa dk 30 ... wanafunzi wanaweza kutoka kwenye chumba cha mtihani unless kuna taarifa za kuchelewa kwa mtihani... Tukio lilivyotokea ni kwamba mtihani ulichelewa zaidi ya masaa 2 na bila taarifa YOYOTE.
  2. SOTE tulikubaliana ya kwamba tusiendelee na mtihani hule na kwa vile wengine walikuwa na mitihani inayofuata muda wa mchana... sasa matraitor wachache kama wewe mliendelea kufanya mtihani hata baada ya kuletwa masaa ma 3 baadaye...
  3. Hata baada ya kuendelea na mtihani, tuliokuwa nje tuliwasihi mtoke ili tuwe na msimamo wa pamoja nanyi mliweka masilahi yenu mbele kama mafisadi na kusahau masilahi ya wengi..
  4. chuo kilitaka kutagawa nanyi mlivyo waoga kama kunguru mkagawanyika.... kweli nyinyi hamfai hata kuongoza ujumbe wa nyumba kumi kwani mnaweka masilahi yenu mbele na kusahau maslahi ya wengi... ndio nahisi mnaotuingiza taifa hili kwenye mikataba mibovu kwa faida yenu na familia zenu tu bila kujali mateso ya wa Tz wengi...
  5. Napenda kukutahadhalisha kutotaja majina ya watu ovyo humu JF, wakati wewe umejificha kwenye mwamvuli wa ID FEKI..
  6. Napenda kuwapongeza tena wana G211 kwa moyo wa kizalendo na wa kijasiri wa kuungana pamoja dhidi ya udhalimu wa chuo/serikali na kushinda ... nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu na mungu akipenda aweze kutuunganisha tena ili tushinde vita dhidi ya ufisadi kwani naamini bado mnaendeleza mapambano huko mliko...
  7. ALUTA CONTINUA NA HONGERA G211...
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,070
  Trophy Points: 280
  ..waliokosea ni viongozi/wawakilishi waliokubali mtihani uanze baada ya kuchelewa masaa 3++.

  ..pia lazima tukubali kwamba kuna mahusiano mabaya kati ya waalimu na wanafunzi hapo UDSM.

  ..hali ya kuogopana, kutishana, kuwindana, kupigana, haifai ktk mazingira ya kisomi.
   
 19. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kinachogomba ni utaratibu mliotumia wa kumng"oa Mutungirehi. Huwezi kuzitetea kwa sababu ulikuwa ni uhuni ambao wenzako bila aibu wanauita ni ushujaa.

  Kwani hakukuwa na njia ya kidemokrasia ya kumuondoa? Njia ilikuwepo na ndiyo iliyotumika baada ya nyinyi wengi kusimamishwa.

  Njia hiyo ilitumukaje? Kumbuka tulipoitwa kurudi Chuoni kitu cha kwanza tukapewa referendum au tuite vote of no confidence kama wote tunamtaka Mutungirehi abaki au la.

  Tukapiga kura na Mutungirehi akashindwa na ikabidi uchaguzi ufanyika upya kumpata rais mpya wa DARUSO. Sasa, mlishindwa nini kuieleza iwe namna hii na mbona aliondoka ndipo akarithiwa na Lenganasa.

  Kama alikuwa amenunuliwa hata kama ni kweli, mbona kununuliwa kwake hakukuzuia tumuondoe kwa kura kistaarabu. Hivyo, tatizo nisilolitetea ni ule uhuni uliotumika wa kumvamia wakati history imethibitisha tulimuondoa kwa kura na akaondoka.

  Mbona baada ya kumuondoa akabaki analalamika kwa kujificha jina halisi magazetini akiponda kuondolewa kwake magazetini.

  Hivyo, kile kitendo cha pale Nkrumah Hall huwezi kukabtiza jina jingine bali uhuni ambao unahitaji akili ya ajabu kuutetea eti kwa kuuita ujasiri. Ujasiri kwa nani?
   
 20. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Muonamambo ni kweli ndio maana mlishinda kesi kirahisi.
  Halafu pia sijapenda huyu bwana aka traitor anasema wazi majina ya watu huku lake lipo kapuni, mods huyu traitor anastahili ban walau ya siku 3, kwa kuwa bado analeta utraitor.
  All in all, well said Muonamambo.
   
Loading...