Ukweli kuhusu alama ya mnyama

Ukweli kuhusu alama ya mnyama

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,720
Je alama ya mnyama ni nini? Kuna maelezo mengi yaliyotolewa na baadhi ya watu juu ya alama ya mnyama, wengine hudhani kuwa alama ya mnyama ni “chip” ya computa, au kadi, au kitu halisi kinachoweza kubebeka! Lakini Je Biblia inaelezea vipi kuhusu alama ya mnyama? Ngoja tuangalie Mungu anachokisema juu ya alama ya mnyama.

(NB: maneno “alama”, “muhuri”, “ishara” au “dalili” ni visawe).

Ufunuo 13:16-17 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Kwanini alama hii ni ya muhimu kuelewa? Kama ukitaka kuthibitisha kwamba kitu flani ni chako, au ukitaka kuonyesha kuwa wewe ni mmiliki wa kitu flani, au ukitaka kutia alama kitu flani kuwa chako, siku zote kutakuwa na vitu vitatu tofauti.

*. Jina lako.
*. Cheo chako.
*. Mahali unapomiliki.

Hivyo, kama raisi wa Tanzania akitaka kuthibitisha kwamba kitu flani kimetoka kwake lazima athibitishe kama hivi:

*. Jina = Jakaya M. Kikwete
*. Cheo = raisi
*. Anapomiliki = Tanzania

Kuna serikali mbinguni (Isa. 9:6), na alama au muhuri wa Mungu ni sheria yake. Angalia katikati ya amri kumi na utaona muhuri wa Mungu, “Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba;…” Kut. 20:11

JINA LAKE = BWANA (“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu…” Isa. 42:8).CHEO CHAKE = MUUMBA (…BWANA…yeye aliyeziumba mbingu, na…nchi…” Isa. 42:5).ANAPOMILIKI = MBINGU NA NCHI (“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA…” Zab. 24:1).

Hivyo, BWANA alipoziumba mbingu na nchi kwa siku sita, siku ya saba alipumzika ili kuweka alama au muhuri kwamba yeye ndiye aliyeziumba mbingu na nchi, kwa hiyo Sabato ni muhuri unaothibitisha kwamba BWANA:

Aliziumba mbingu na nchi.Alituumba sisi pamoja na vitu vingine vyote.Anamiliki mbingu na nchi, pamoja na vitu vyote vilivyomo.

Kwanini shetani anafanya bidii sana kuwaongoza watu wasiitambue Sabato? Ni kwa sababu shetani anataka kujifanya yeye kuwa kama muumba wa mbingu na nchi, hivyo anainaingiza alama yake ambayo ni kinyume na alama ya kweli ya Mungu. Sabato ni alama au muhuri wa Mungu, kwa hakika Mungu mwenye anathibitisha ukweli huu kwa kusema, “…Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote;…” Kut. 31:13. (Kumbuka! maneno ishara, muhuri, alama ni visawe, na yanaweza kutumika kwa kuyachanganya-changanya).

Njia rahisi na nyepesi ya kugundua alama ya mnyama, ni kutafuta kujua kwanza alama ya Mungu., harafu utaona kwamba alama ya mnyama ni kinyume na alama ya Mungu.

Ufunuo 7:2-3 “Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka mawio ya jua, mwenye mhuri wa Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.”

Kama tulivyoona huko nyuma kwamba muhuri na alama ni visawe! Hivyo watumwa wa Mungu wanawekwa alama katika vipaji vyao vya nyuso, kipaji cha uso hapa humaanisha akili, mawazo, au nia.

Wabrania 10:16 “Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika…”

Pia Wanafisikolojia hutuambia kuwa ubongo wa mbele wa cerebrum [paji la uso] ndipo shughuri kama uamuzi, hukumu, na uhuru wa kutaka vinapofanyikia. Hivyo, Wakristo wanawekwa alama katika vipaji vya nyuso zao, pale tu wanapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wao na kutunza amri kumi zote kwa kuhiari, au kutaka wao wenyewe bila kulazimishwa. Hii ndiyo maana muhuri au alama ya Mungu haiwekwi mkononi, kwa sababu Yesu hatawalazimisha watu kumwabudu na kuzitii amri zake. Mkono humaanisha kulazimishwa kufanya kitu furani kinyume na nia zetu.

Jeremia 38:23 “Na watawatoa wake zako, na watoto wako wote, na kuwachukua kwa Wakaldayo; wala wewe hutapona na mikono yao, bali utakamatwa kwa mkono wa mfalme wa Babeli, nawe utakuwa sababu ya kuteketezwa kwa mji huu.”

Yesu kamwe hatatulazimisha sisi kumwabudu, kwani anapendezwa kama tutamwabudu na kutunza sheria zake zote, kwa hiari yetu bila kulazimishwa.

Ufunuo 13:15-17 “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Alama ya mnyama inawekwa katika kipaji cha uso na kwenye mkono. Hivyo wale wote wanaokubali kwa hiari yao wenyewe kumfuata mnyama na kutii amri zake, hawa wamewekwa alama kwenye paji la uso; maana wamehiari wao wenyewe bila kulazimishwa. Na wale wanaopokea alama kwenye mkono, ni wale watakaotii amri za mnyama kwa kulazimishwa bila ridhaa yao. Kwa hofu ya kifo na kushindwa kununua wala kuuza, wanaamua kumtii mnyama ili wasipoteze vitu walivyovifanyia juhudi nyingi katika maisha yao na hili ni bonge la kosa.

Kwa sababu tumeelewa kwamba kuamua kumkubali Yesu kama Mwokozi wetu na kutunza mafundisho na amri zake zote, ni sawa na kupokea alama au muhuri wa Mungu. Tunatakiwa pia tuelewe kuwa kukubali amri, mafundisho, au mapokeo ya kanisa la Romani Katoliki au kanisa lingine lolote linalofuata imani ile ile na kufundisha mapokeo yake, inamaanisha tumepokea alama ya mnyama. Pia elewa kuwa kutakuwa na wengine ambao sio Wakatoliki lakini wanafanya kila kitu ambacho mnyama anaamru kwa kuogopa kufa, au kupoteza mahitaji ya kawaida kwa kuzuiliwa kuuza wala kununua, kitu ambacho kitapelekea kukubali kufuata matakwa ya mnyama. Hawa watapokea alama ya mnyama kwenye mkono kwa sababu wamelazimishwa kinyume na matakwa yao. Wakatoliki na Wakristo wengine ambao hukubali haya “mafundisho ya wanadamu” watakuwa wamepokea alama ya mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao kwa sababu wamekubali kwa hiari kuwa kanisa lao liko sawa kwa kubadili maandiko na kuingiza “mapokeo” au “mafundisho ya wanadamu.” Na hii ilionywa katika unabii.

Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.”

Hivyo, kama ukipokea “alama” kwa kuchagua mwenyewe, hii inamaanisha umewekwa alama kwenye kipaji cha uso. Na kama ukipokea “alama” kwa kulazimisha, hii inamaanisha umewekwa alama kenye mkono wa kulia. Lakini kumbuka.

Mathayo 16:25 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.”

Mathayo 10:39 “Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.”

Yohana 12:25 “Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.”

Tukirudi kwenye alama ya mnyama kanisa la Romani Katoliki bila ya kutambua linatimiza unabii huu kwa maelezo yafuatayo.

“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

Kama unabii uko sawa unaposema jumapili ni alama ya mnyama, na Mungu anasema wazi wazi.

Kutoka 31:13 “…Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.”

Ezekieli 20:12, 20 “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua yakuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye…zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua yakuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.”

Maneno ishara, muhuri, na alama ni visawe, na yanaweza kutumika popote kwa kuyabadilisha-badilisha.

Hivyo, tuna uhakika wa ukweli wa Biblia kwamba Sabato ni ishara, muhuri, au alama ya Mungu. Na jumapili ni ishara, muhuri, au alama ya mnyama.

FB_IMG_1541242311357.jpeg
 
Hivi wewe ina maana huwaoni kabisa wale wenye alama ya kama kovu lililopona kwenye paji la uso na mkononi ambao wanasujudu usiku na mchana
Kama kitabu cha ufunuo kinavyo sema ?
Mbona hilo kovu linaonekana waziwazi kabisa, au hadi nikuwekee picha ya paji la uso wa jilani yangu hapa...!
Tatizo lako wewe unawaza Sabato tu, hutoki nje ya Boksi la fuvu lako.
Elleni amekupumbaza kabisa.
 
1541295270304.png
 
Aliyekwambia WAISLAMU ndio wanahusika na huo unabii nani?

Kwann usijenge hoja ukaonesha ni kwajinsi gan wanahusika ,huku ukiweka aya
 
Aliyekwambia WAISLAMU ndio wanahusika na huo unabii nani?

Kwann usijenge hoja ukaonesha ni kwajinsi gan wanahusika ,huku ukiweka aya
Wewe unamatatizo sana ya kukisiakisia mambo.
Mimi wapi nimewataja watu na dini zao ?
Wewe dunia hii unayemwona anayesujudu ni Mwislamu pekee ?
Tatizo lako hujui mambo mengi zaidi ya Sabato.
Unazijua imani mbalimbali za hii dunia ?
Unazijua Secret Society mbalimbali na mambo wanayoyafanya yanayoambatana na kusujudia miungu yao.
Unawajua Wabudha na Wahindu ambao hadi wanachora kidoti kwenye paji la uso wao ambayo ni alama yao ya Ibada ?

Soma kijana usiishie kumnukuu Elleni G White na kuona ndio unajua mambo.

Kitabu cha Ufunuo kipo wazi kabisa, wewe aliyekuambia Chapa ni Sabato nini kama sio kuishia kumnukuu Elleni.

Hebu soma hapa ona Ufunuo inavyosema

" 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."

Umeelewa kilichoandikwa hapo ?
Au ni lazima kwanza umsikilize Elleni anavyosema ?
 
Acha kupaniki

Hakuna sehemu nimemnukuu ELLEN.WHITE unaweza kunionesha?

Mbona unaweweseka hivo?

Kanisa katoliki haliwez kujinasua na unabii wa mnyama ,na Alama ya mnyama

Naona unataka kuamisha magoli,

Hapa sijamnukuu ellen nimenukuu BIBLIA NA KUJENGEA HOJA

shida umejawa na chuki kwa ellen g white maana ALIELEZA UKWELI MTUPU JUU YENU
FB_IMG_1540964211457.jpeg
FB_IMG_1540964205378.jpeg
 
Wewe unamatatizo sana ya kukisiakisia mambo.
Mimi wapi nimewataja watu na dini zao ?
Wewe dunia hii unayemwona anayesujudu ni Mwislamu pekee ?
Tatizo lako hujui mambo mengi zaidi ya Sabato.
Unazijua imani mbalimbali za hii dunia ?
Unazijua Secret Society mbalimbali na mambo wanayoyafanya yanayoambatana na kusujudia miungu yao.
Unawajua Wabudha na Wahindu ambao hadi wanachora kidoti kwenye paji la uso wao ambayo ni alama yao ya Ibada ?

Soma kijana usiishie kumnukuu Elleni G White na kuona ndio unajua mambo.

Kitabu cha Ufunuo kipo wazi kabisa, wewe aliyekuambia Chapa ni Sabato nini kama sio kuishia kumnukuu Elleni.

Hebu soma hapa ona Ufunuo inavyosema

" 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."

Umeelewa kilichoandikwa hapo ?
Au ni lazima kwanza umsikilize Elleni anavyosema ?
Tuambie hiyo alama ni nini?

Je kila mtu duniani atakayepigwa ALAMA kama usemayo tayari huyo ni washetani? Hata kama matendo yake ni mazuri?

Usitafsiri biblia kama Katekisimu
 
Hebu soma hapa ona Ufunuo inavyosema

" 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake."

[/QUOTE]

KWANZA UNAELEWA HUYO MNYAMA ANAYEZUNGUMZWA HAPO NI NANI?

JE SANAMU YA MNYAMA NI NANI?
 
JE SANAMU YA MNYAMA NI NANI?[/QUOTE]Lete Aya ya kwenye Biblia inayosema alama ya Chapa katika Paji la uso na mkononi ni SABATO.
 
Tuambie hiyo alama ni nini?

Je kila mtu duniani atakayepigwa ALAMA kama usemayo tayari huyo ni washetani? Hata kama matendo yake ni mazuri?

Usitafsiri biblia kama Katekisimu
Naomba unukuu Aya katika Biblia inayosema Alama ya Chapa ya kwenye Paji la Uso na Mkononi ni SABATO
 
Elleni ameharibu kabisa kichwa chako.
Unachowaza kila siku ni Ukatoriki na Sabato.
Wakatoriki watatubu na kwenda Mbinguni wewe unabaki na picha ya Katoriki na Sabato hadi unakupata umauti.
 
Elleni ameharibu kabisa kichwa chako.
Unachowaza kila siku ni Ukatoriki na Sabato.
Wakatoriki watatubu na kwenda Mbinguni wewe unabaki na picha ya Katoriki na Sabato hadi unakupata umauti.
Mbona unalalamika tu?

Wakatoliki mtatubu lini na kuyavunjilia mbali haya maashera ili muende mbinguni kama unavyodai?
FB_IMG_1540797464209.jpeg
 
Wala haihitaji elimu kubwa ya theology, kwa kuangalia na kuchunguza kwa makini tu hata sisi wa upande mwingine tusiofungamana tunajua kabisa alama ya mnyama ni jumapili, kwahiyo kanisa katoliki ni baba wa alama ya mnyama na matawi yake ni watoto wake
 
Naomba unukuu Aya katika Biblia inayosema Alama ya Chapa ya kwenye Paji la Uso na Mkononi ni SABATO
Maswali nimekuuliza umeyakimbia, wewe jamaa bhana

Halafu hakuna sehemu nimesema alama ya mnyama ni sabato

Bali MUNGU MWENYEWE ANAKILI SABATO NI ISHARA AU ALAMA AU MUHURU WAKE

NA NIMEELEZA

NA KINYUME CHA SABATO NI IBADA YA JUMAPILI NA KANISA LA ROMA LINAKILI IBADA YA JUMAPILI NI ALAMA YAKE

NA MNYAMA NI KANISA LA ROMA

HIVYO ALAMA YA MNYAMA NI IBADA YA JUMAPILI

ndio maana nilikuuliza kabla hujakurupuka ,je unamjua MNYAMA NI NANI?

KABLA HAUJAJUA ALAMA YAKE
FB_IMG_1540529670203.jpeg
 
Mbona unalalamika tu?

Wakatoliki mtatubu lini na kuyavunjilia mbali haya maashera ili muende mbinguni kama unavyodai?View attachment 920645
Aliyekuambia mimi ni Mkatoriki ni nani ?
Wewe unaakili sana tatizo lako ni moja tu la kupenda kukopi na kupesti maandiko ya watu wengine.
Soma na fanya utafiti mwenyewe.
Badala yake umekuwa hakimu wa Wakatoriki.
Saa ya kutubu wanaijua wakatoriki wenyewe kama walivyojua makosa yao.
Wewe tubu zambi zako na ufuate maagizo ya mwalimu wako Yesu Kristo, na sio huyo dada yako Elleni G White atakupotosha tu.
Yesu Kristo ndiye Alfa na Omega achana na habari za Hellena.
 
Tuambie hiyo alama ni nini?

Je kila mtu duniani atakayepigwa ALAMA kama usemayo tayari huyo ni washetani? Hata kama matendo yake ni mazuri?

Usitafsiri biblia kama Katekisimu
Ushaambiwa wanao fanya haya matendo.
1. Kusujudia miungu wengine yaani sanamu au mnyama.
2. Kuwa na Chapa, kwenye Paji la Uso na Mkononi.
Wewe hapo usichoelewa ninini ?
-Hulijui paji la Uso ?
-Huujui Mkono ?
-Huijui alama ya Chapa kama kovu lililo pona ?
Au unataka kutuaminisha kuwa kila kitu kilichoandikwa kwenye Biblia lazima kwanza tukitafsiri toka kwenye nadharia ya siku ya Jumapili na Jumamosi ?
 
Back
Top Bottom