Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,181
- 5,321
- Thread starter
- #101
Mpaka sasa tatizo la duniani ni kifo na kutokuwa na uwezo wa kutatua chamgamoto za magonjwa na matatizo mengine. Ila raha zipo na furaha ipo tena ya kutosha kwa mtu asiye na maradhi na mwenye uwezo wa kutatua chamgamoto za maisha.
Raha ya shida ni iwe na utatuzi. Raha ya njaa uwe na chakula au ujue pa kukipata chakula, raha ya changamoto yoyote ni iwe na utatuzi.
Mbinguni kama hakuna kusikia njaa, hakuna kiu, hakuna kuoa wala kuolewa, hakuna kujenga nyumba nzuri, hakuna viwanda vya magari ukanunua gari upendalo, unafahamu vipi kuwa kuna raha? Raha ni nn mbinguni?
Je binadamu wote wanataka hiyo aina ya raha? Au ni vile kama huitaki basi unachomwa hivyo unakuwa huna jinsi? Ts either raha ya kulazimishiwa au moto.
Unahisi raha ni kula na kunywa pombe, uzinzi, kuendesha vitu,kumiliki mali, kuagiza chochote unachokitaka na unakipata, kuwa na afya njema,kuwa na familia n.k
Siyo kweli hiyo siyo raha kamili kwa sababu utakubaliana nami kuwa hakuna raha duniani yakudumu kila kitu tunakipata duniani kwa limitation fulani na lazima penye raha kuwepo na uchungu fulani tukiachana na hilo la furaha ya kidunia ambayo kamwe hata ikiwa asilimia 100 bado ahikidhi kuitwa furaha kamili,
Hii ndiyo sababu ya baadhi ya watu ku-meditate kuitafuta hiyo furaha ya peponi isiyo na mfano wake yaani hali ya kujihisi kutoitaji kitu kingine cha ziada kukamilisha furaha yako mfano uraibu,hisia,pesa,nguvu,afya,mali,michezo,fahari nakadhalika,
Kuhusu kufikia mpaka kuchomwa moto siwezi lielezea zaidi maana siyo uonevu ni haki kabisa kwa kuwa mkaidi hiyo ndo adhabu ikufaayo,pia usijisaulishe kuwa huyo unayempinga ni kwa sababu yake upo na unaexist na kwa kuwa anakupenda anakutakia mema tu.