mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 892
- 1,709
Siungi mkono ushoga wala uvutaji shisha ama sigara hadharani,lakini nafikiri kuna taasisi kama ustawi wa jamii ndio wanaotakiwa kudeal na hivi vitu wao wako wapi ? Mkuu wa mkoa una mambo mengi ya kufanya matatizo ya barabara,madawa,gharama kubwa ya sukari maisha magumu hayawezi kumalizwa kwa kuacha kuvuta shisha au kuacha kuvuta sigara.Ukuu wako wa mkoa haupimwi kwa hivyo vitu,kuna matatizo mengi na makubwa ya kutatua kuliko hayo!! We mwenyewe mbona unapiga picha na mashoga ?? Mbona unawatag instagram ?? Au mpaka utajiwe shoga ni nani ??? Mimi nikuombe utoe amri ama tamko kwa Ustawi wa jamii katika mkoa wako,wape mda kuhakikisha hayo mambo hayapo katika mkoa wako na wewe uendelee na mambo mengine ya msingi kuhusu kero za wananchi,bado ziko nyingi sana hazijatatuliwa !