Ukurasa wa mbele wa Nipashe la 25/04/2018

Ukurasa wa mbele wa Nipashe la 25/04/2018

Nilipitia uchipukizi miaka ya 80... sio jambo la kushangaza wala kuogopesha!
 
Yaani picha ya mtoto kushika bunduki,inatisha?
Wabongo VP aisee,yanatotakiwa kututisha,ni escrow,epa,meremeta,tangold,upotevu wa 1.5tillioni,
Sio kapicha ka mtoto aliyeshika bunduki

Ndugu yangu, kumuona mwanajeshi au polisi ameshika bunduki ni kitu cha kawaida kwa kuwa ni sehemu ya kazi yake - Ulinzi. Kumuona mwananchi wa kawaida ameshika bunduki inaweza kukufikirisha kidogo lakini ukapotezea. Ila ukikuta mtoto kashika bunduki lazima ushtuke kwa kuwa yeye hana jukumu hilo wala nafasi hiyo ya kulinda kwa silaha bali kulindwa. Utakapoona mtoto anatumia silaha za moto, lazima kuna tatizo kubwa na nchini mwetu hiyo siyo taswira yenyewe. Tafadhali tuache ubishi usio wa tija, ustawi wa mtoto ni muhimu sana na ndio maana ni kundi lililostahili idara yake kwenye wizara.

Maswala ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma yana umuhimu wake na nafasi yake ya kujadili. Hilo halituzuii kuzungumzia maswala mengine yenye umuhimu wake.
 
Guns.jpg

utotoni tumecheza sana, na ni michezo ya kawaida kwa watoto, Ila naungana na wewe kwenye mambo rasmi kama hayo haipendezi.
Hata utotoni haikupaswa. Hao watoto wanacheza hivyo kwa sababu tayari wameshaambukizwa fikra hizo kutokana na fikamu au michezo ya kompyuta
 
Unashangaa!
Mtoto wa Rais wa Korea ya kaskazini,ana miaka 8 lakini kamaliza mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha luteni.

Je Tanzania ni Korea Kaskazini? Mfumo wetu wa Utawala unafanana na wa Korea Kaskazini? Huo ndio mfano wa kuiga?
 
Mkuu hata kama ni ya mbao, sio jambo sahihi kumzoesha mtoto mdogo silaha za maangamizi. Binafsi, hata watoto chini ya umri wa miaka 17 kuruhusiwa video/computer games za mashambulizi siyo sahihi.
Mbona primary tulicheza gwaride Kutumia bunduki za mbao
 
Yaani dume na pu..mbu zako unatetemeka kuona hilo limbao akiwa nalo dogo?

Umepitia Skauti!? Kuna mafunzo sawia na jeshi, lakini hiyo siyo Ak47 real,

Hahaaa mnataka vurugu ilihali mnatishwa na mbao?

Mkuu, hunifahamu na hivyo huwezi kunisemea matakwa yangu. Hakuna mahali katika historia yote ya uandishi wangu wa JF nimetamka kuwa nataka vurugu. Jitahidi kuwa na heshima japo kidogo.

Ndio, nimepitia skauti na mafunzo ya jeshi, na katika vyote hivyo kuna madaraja ya mafunzo. Sijui mafunzo uliyopitia wewe, ila skauti kwa mtoto wa chini ya miaka kumi na saba haihusihi matumizi ya SMG. Kwa kiasi kikubwa, skauti inakufunza kutumikia jamii yako vyema na kukabiliana na mazingira yako katika hali mbalimbali.
 
Mbona primary tulicheza gwaride Kutumia bunduki za mbao

Mh! Labda kama ni miaka ya 70 au 80 mwanzoni. Sikumbuki enzi zangu kufanya gwaride kutumia silaha, iwe ya mbao au la.
 
Mkuu, hunifahamu na hivyo huwezi kunisemea matakwa yangu. Hakuna mahali katika historia yote ya uandishi wangu wa JF nimetamka kuwa nataka vurugu. Jitahidi kuwa na heshima japo kidogo.

Ndio, nimepitia skauti na mafunzo ya jeshi, na katika vyote hivyo kuna madaraja ya mafunzo. Sijui mafunzo uliyopitia wewe, ila skauti kwa mtoto wa chini ya miaka kumi na saba haihusihi matumizi ya SMG. Kwa kiasi kikubwa, skauti inakufunza kutumikia jamii yako vyema na kukabiliana na mazingira yako katika hali mbalimbali.
Kwa taarifa yako skauti wanafanya mpaka medani za komandoo na masuala ya ujanja porini ikiwemo usomaji wa ramani za kivita, wanapiga kambi msituni,

Mafunzo hayo yanakuwa basically kumjenga kijana awe na nidhamu na ukakamavu.
Kama ulipitia huko sikutegemea kama ungeshangaa kiivo.

Msikuze mambo madogo madogo kama haya.
 
Kwahiyo kumbe Tanzania ya sasa tunatengeneza Wapiganaji zaidi kuliko Wafanyakazi wa Viwanda tunavyovijenga?
Kati ya vitu vinavyonichanganya akili ni pale ninapojitahidi kujua ni nani "Think tank" wa serikali kwa sasa!! Hivi ni nani anayepitisha upuuzi kama huu uwekwe kwenye ratiba ya shughuli maalum ya Serikali?
 
Leo ukurasa wa mbele wa gazeti la Nipashe umebeba picha inayoonyesha watoto wakifanya mazoezi kwaajili ya sherehe za Muungano. Kiukweli hiyo picha imeniogopesha. Kumuona mtoto mdogo wakitanzania ameshika bunduki siyo jambo la kawaida na kamwe halitakiwi kuwa jambo la kawaida. Sielewi uongozi wa taasisi za usalama wameruhusu vipi jambo kama hili.

View attachment 756142
Sasa hapo polisi wasikie huko kibiti Kuna vijana kwenye uwanja wa msikitini wanajifunza sarakasi na mazoezi ya Judo uone kile watafanywa na FFU kutumwa kuweka doria
 
Mkuu hata kama ni ya mbao, sio jambo sahihi kumzoesha mtoto mdogo silaha za maangamizi. Binafsi, hata watoto chini ya umri wa miaka 17 kuruhusiwa video/computer games za mashambulizi siyo sahihi.
MIAKA 17? ANGALIA VIGEZO VYA DARASA LA SABA KUINGIA JKT
 
enzi hizo haya mambo ya sasa hayakuwepo labda chipukizi ya somalia
Kinachotisha ni kile wachezacho kwenye faragha na ni war video games ambazo wazazi wengi hajali hata age limit za game hizo! Na sio hii michezo ya halaiki
 
Mleta thread una umri gani?
Enzi zetu tulivyokuwa wadogo miaka ya 90 tulikuwa tunatengeneza bunduki
 
Kinachotisha ni kile wachezacho kwenye faragha na ni war video games ambazo wazazi wengi hajali hata age limit za game hizo! Na sio hii michezo ya halaiki

waache wanajitengenezea bomu litakalowalipukia wao wenyewe. maana hao watoto bado wanalishwa. wakikua wakajua ukweli wa umaskini wao, ndipo wanaowapa michezo hiyo watashika adabu.
 
Mbona ni kawaida kwenye maonyesho ya halaiki. Tuliocheza halaiki huwa kunakuwa na vikosi na maonyesho tofauti tofauti.

Vv
 
Back
Top Bottom