Ukurasa wa mbele wa Nipashe la 25/04/2018

Ukurasa wa mbele wa Nipashe la 25/04/2018

SueIsmael

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2013
Posts
932
Reaction score
1,283
Leo ukurasa wa mbele wa gazeti la Nipashe umebeba picha inayoonyesha watoto wakifanya mazoezi kwaajili ya sherehe za Muungano. Kiukweli hiyo picha imeniogopesha. Kumuona mtoto mdogo wakitanzania ameshika bunduki siyo jambo la kawaida na kamwe halitakiwi kuwa jambo la kawaida. Sielewi uongozi wa taasisi za usalama wameruhusu vipi jambo kama hili.

upload_2018-4-25_9-47-28.png
 
Mkuu hata kama ni ya mbao, sio jambo sahihi kumzoesha mtoto mdogo silaha za maangamizi. Binafsi, hata watoto chini ya umri wa miaka 17 kuruhusiwa video/computer games za mashambulizi siyo sahihi.
Guns.jpg

utotoni tumecheza sana, na ni michezo ya kawaida kwa watoto, Ila naungana na wewe kwenye mambo rasmi kama hayo haipendezi.
 
Guns.jpg

utotoni tumecheza sana, na ni michezo ya kawaida kwa watoto, Ila naungana na wewe kwenye mambo rasmi kama hayo haipendezi.

Ni kweli tulicheza hii michezo na kuunda vifaa vyetu vya kuchezea ila ukiangalia michezo mingi tuliyocheza kipindi hicho ilitokana na tulichokiona kwenye runinga au kufundishwa na wenzetu. Kwa sasa kuna ushawishi wa makusudi unaotumiwa na makampuni makubwa yanayolenga vipindi na michezo kama hii ilikuandaa soko la baadae. Ni bora kuwaweka watoto mbali na vipindi au michezo ya namna hii kabisa.

Kwa hili tukio, kama usemavyo, kurasimisha kitu kama hichi katika maadhimisho ya kitaifa ni jambo la kupinga na kukemea.
 
Leo ukurasa wa mbele wa gazeti la Nipashe umebeba picha inayoonyesha watoto wakifanya mazoezi kwaajili ya sherehe za Muungano. Kiukweli hiyo picha imeniogopesha. Kumuona mtoto mdogo wakitanzania ameshika bunduki siyo jambo la kawaida na kamwe halitakiwi kuwa jambo la kawaida. Sielewi uongozi wa taasisi za usalama wameruhusu vipi jambo kama hili.

View attachment 756142

Kwahiyo kumbe Tanzania ya sasa tunatengeneza Wapiganaji zaidi kuliko Wafanyakazi wa Viwanda tunavyovijenga?
 
Kwahiyo kumbe Tanzania ya sasa tunatengeneza Wapiganaji zaidi kuliko Wafanyakazi wa Viwanda tunavyovijenga?

Haijengi picha nzuri hata kidogo. Tumezoea kuona scouts na girl guides, lakini siyo watoto wakishikishwa bunduki.
 
Naungana na ww mtoa mada hiyo SMG dogo ameikamatia hapo
 
Yaani picha ya mtoto kushika bunduki,inatisha?
Wabongo VP aisee,yanatotakiwa kututisha,ni escrow,epa,meremeta,tangold,upotevu wa 1.5tillioni,
Sio kapicha ka mtoto aliyeshika bunduki
 
hapo naona inamaanisha kwamba wao ndo watahost hizo sherehe za muungano halafu wahusika wenyew watakua mtaani wanalinda nchi
 
Unashangaa!
Mtoto wa Rais wa Korea ya kaskazini,ana miaka 8 lakini kamaliza mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha luteni.
 
Tanzania inapelekwa kijeshi jeshi sasa hivi.

Rais anavaa kijeshi. Hakuna rais wa Tanzania aliyevaa kijeshi nje ya Vita. Hata Kikwete aliyekuwa mwanajeshi hakuvaa kijeshi kama rais.

Walinzi wa Rais wanabeba silaha kubwa kubwa wazi wazi kwa namna ambayo haikuwahi kufanyika hata enzi za kesi ya uhaini.

Tumeondoka kuchanganya siasa na jeshi tangu mfumonwa vyama vingi, lakininawamu hii ya tano wanajeshi wamerudishwa katika teuzi za kisiasa.

Rais anasema anatamani kuwa IGP.

Rais anahalalisha rushwa kwa askari trafiki kwa kusema ni hela ya kupiga brashi viatu tu.

Siwezi kushangaa hili. Kuna pattern inatokea. Si jambo la kutokea peke yake.
 
Back
Top Bottom