Ukubwa wa dunia ukilinganisha na galaxy yetu

Ukubwa wa dunia ukilinganisha na galaxy yetu

1743371573035.png
 
Ili Dunia ifanane kwa ukubwa na Jua, zaidi ya Dunia milioni moja zitahitajika kuungana ili kufikia saizi kamili ya Jua.

Ikiwa umelipunguza Jua kutoka kwenye saizi yake halisi hadi kufikia saizi ya jicho la binadamu, basi ukubwa wa Galaxy yetu, Milky Way, utakuwa sawa na Dunia.

Mwanga unaotoka kwenye galaxy iliyo karibu zaidi nasi, Andromeda, unachukua takriban miaka milioni 2.5 kufika duniani. Hii ina maana kwamba mwanga tunaouona leo kutoka Andromeda ulianza safari yake miaka milioni 2.5 iliyopita!

Kwa upande mwingine, mwanga unaotoka kwenye Jua unachukua takriban dakika 8 tu kufika duniani.

Pamoja na umbali wake mkubwa, Andromeda bado ni kubwa sana. Ikiwa utachukua saizi ya Jua jinsi linavyoonekana kwa jicho la kawaida angani, basi Galaxy ya Andromeda itqkuwa mara sita kubwa zaidi ya Jua! Galaxies ni kubwa sana!
Nani alienda huko kipima hiyo galaxy ndio akagundu kuwa ni kubwa kuliko Dunia? Acheni kuparamia nature msije potea kama Juma Nature
 
Wazungu wanatuongopea sana kuhusu Universe.

Milk way mara galaxies ,mara kwenye universe kuna galaxy kibao....sisi tupo kwenye milk way ,mara kuna majua kibao , mara nyota nazo ni jua...mara jua ni nyota.
Ni sahihi kuona hivyo kwa sababu Wazungu wameweza kutengeneza ndege, satellites na rockets na hata kufika mwezini wakati kuna Waafrika bado wanatumia punda kama usafiri.
 
Wazungu wanatuongopea sana kuhusu Universe.

Milk way mara galaxies ,mara kwenye universe kuna galaxy kibao....sisi tupo kwenye milk way ,mara kuna majua kibao , mara nyota nazo ni jua...mara jua ni nyota.
Inawezekana wanatuongopea ila kwa jinsi sisi africa tulivyo nyumbu na magoigoi ,utaweza vipi kujitetea?
 
Nimesikitika sana kwamba miaka yote nimefundishwa Pluto ni sayari, halafu leo wanangu wanafundishwa Pluto siyo sayari na sayari zinaishia 8 tu.

Nyie Wanasayansi uchwara mmesababisha wanangu watuone mimi na Walimu wangu ni vilaza. Pumbavu zenu sana.
 
Wanadanganya wanaenda mars kumbe wanaenda Namib desert na Kalahari desert huko Namibia/Botswana.
 
Ili Dunia ifanane kwa ukubwa na Jua, zaidi ya Dunia milioni moja zitahitajika kuungana ili kufikia saizi kamili ya Jua.

Ikiwa umelipunguza Jua kutoka kwenye saizi yake halisi hadi kufikia saizi ya jicho la binadamu, basi ukubwa wa Galaxy yetu, Milky Way, utakuwa sawa na Dunia.

Mwanga unaotoka kwenye galaxy iliyo karibu zaidi nasi, Andromeda, unachukua takriban miaka milioni 2.5 kufika duniani. Hii ina maana kwamba mwanga tunaouona leo kutoka Andromeda ulianza safari yake miaka milioni 2.5 iliyopita!

Kwa upande mwingine, mwanga unaotoka kwenye Jua unachukua takriban dakika 8 tu kufika duniani.

Pamoja na umbali wake mkubwa, Andromeda bado ni kubwa sana. Ikiwa utachukua saizi ya Jua jinsi linavyoonekana kwa jicho la kawaida angani, basi Galaxy ya Andromeda itqkuwa mara sita kubwa zaidi ya Jua! Galaxies ni kubwa sana!
Umeelezea kwa mifano mizuri sana. Njia sahihi ya kumfanya mtu aelewe anachoambiwa. Kuna kitabu nilisoma, profesa wa mahesabu alikwenda kijijini. Wananchi siyo wasomi na ukiwaambia ni profesa wa mahesabu hawawezi kujua ni mtu wa aina gani. Basi ikabidi aliyemtambulisha aseme ''huyu ni bingwa wa mahesabu, anaweza kuhesabu majani yote ya miembe iliyo hapa kijijini''. Watu wakashangaa 'wahaaa, kweli ni bingwa''
 
Sayansi ya anga ni ngumu sana. Kuna mambo ya kufikirika mengi.

ILa kadri miaka inavyoenda na technolojia kukua tunagundua baadhi ya mambo yaliyogunduliwa kale si sahii.

Katika zile sayari 7 nilizofundishwa miaka ile nadhani kuna baadhi zishatoka kwenye sifa ya sayari. Mf. Pluto.
 
Ulifundishwa sayari ziko 7?
 
Ivi hata kwa macho tu ya kawaida toka kesho nje alafu angalia jua... kweli lina ukubwa wa mamilioni ya size kuliko Dunia ?
Ndiyo jua ni kubwa kuliko dunia.maana Kwa umbali lilipo jua Hadi Dunia ni km150 milioni lakini Bado tunaliona ni kubwa.Tofauti na Dunia.Hili limedhibitishwa na wanaanga ambao wameweza kufika sayari ya mars pamoja na Mimi nitadhibitisha mwaka 2027 nitakapo enda huko mars.maana wao kadri wanavyopaa kwenda juu ndiyo Dunia Inaonekana ndogo zaidi Hadi kufikia kama kufanana na punje ya mchanga
 
Back
Top Bottom