Ukuaji wa uchumi unategemea sana hisia za watu, tuendepo hali ya uchumi itakuwa ngumu ikiwa watu watakuwa na hisia za kutishwa na vyombo vya serikali

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Habarini wakuu, Umuofia kwenu!!

Kuna matukio kadha wa kadha ambayo yametokea ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita, mengi yakihusiana na kesi mbalimbali za TRA dhidi ya raia na makampuni ya kitanzania. Issue kama ya shule ya St. Jude, Mobisol na kuna mtu wangu wa karibu anafanya kazi benki, ameniambia kuna request zaidi ya 20 mpaka 30 kutoka TRA dhidi ya baadhi ya wateja mbali mbali. Tumeona pia picha ya mkurugenzi wa bodi ya utalii na mkurugenzi wa TRA wakijadili kuleta kodi ya 'kitanda' kwenye mahoteli ya kitalii.

Nimejaribu kumulika hizi issue zinazotokea na nikajaribu kufanya utafiti wangu kidogo, nimejiridhisha na nna uhakika na mambo yafuatayo.

i) Tunachokiona TRA wakikifanya kwa sasa kitakuwa endelevu zaidi ndani ya miezi 12 inayokuja. Ukichambua mambo kwa three dimension, hutachelewa kugundua kwamba serikali ipo kwenye stress kubwa sana ya kupata pesa. Na stress imeongezeka baada ya kitisho cha kukosa misaada ya kusupport bajeti ambayo ilikuwa ni kiasi kama Tzs 1 Trillion kwa mwaka. Kwa hiyo serikali wanachofanya, ni kujitahidi kufukia hili shimo la Tzs 1 Trillioni ambazo wafadhili ni dhahiri wanaenda kupiga panga. Ubaya mngine na kinachowaogopesha serikali, ni kwamba kuna upungufu wa makusanyo ya kodi nje ya matarajio kwa mwaka 2019/20 na viashiria ni kwamba makusanyo ya kodi ya 2020/21 ni dhahiri pia yanaweza kuwa na upungufu maradufu.

Ni kitu kibaya sana serikali kuwa kwenye stress ya kukosa pesa, maana yake ni kwamba hata ile bajeti iliyopitishwa juzi mwezi wa sita haitaweza kutekelezeka kitu ambacho lazima kiathiri uchumi mzima kwa sababu matumizi ya serikali ni mojawapo ya kipande muhimu kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote. Na ubaya zaidi ni kwamba bajeti zetu sio balanced, kwa miaka kama kumi ilyopita, deficit imekuwa ni kama wastani wa Tzs 3 - 4 Trillioni kila mwaka. So unapoenda kunyimwa misaada ambayo ulikuwa unategemea ili kupunguza makali ya bajeti, maana yake hapo mipango yote ya matumizi uliyoipanga lazima uipige chini au u scale down au option ingine, TRA watie mbinyo wa kukusanya kodi kwa raia (ambacho tunakishuhudia kwa sasa na kitaendelea)

nakisi.JPG



ii) Matokeo ya wanachokifanya TRA, yatahatarisha kudondosha uchumi. hii point namba mbili ndo lengo haswa la uzi wangu, ambao nautumia kama uzi wa kuitahadharisha serikali kwamba matendo yanayofanywa na vyombo vyake kama mwitikio wa 'fiscal distress' inayoinyemelea serikali yenyewe yana hatari za kutumbukiza nchi kwenye mkwamo wa kiuchumi.

Kuna mwanauchumi gwiji wa Marekani, anaitwa Alan Greenspan, kwa faida ya wasomaji huyu alikuwa mwenyekiti wa banki kuu ya Marekani (Fed) kuanzia mwaka 1987 - 2006. Huyu mwamba kwenye kitabu chake cha 'The map and the territory' kuna madini mengi sana juu ya 'mtanziko wa hisia za watu na uhusiano wake kwenye kuanguka kwa shuhuli za kiuchumi' wasomaji mkakitafute ni kizuri sana.

Alan Greenspan kuna mahali aliongelea topic ya 'Risk aversion' ambayo ni tabia ya binadamu ambae anatawaliwa na 'Animal Spirits'. Kwa ufupi kabisa, binadamu huwa tunatabia ya kupenda kuchambua mazingira yanayotuzunguka kwa lengo la kuona kama kuna kitisho cha aina yoyote ili tuweze kuchukua hatua stahiki. Its a natural practice, na ni tabia ya binadamu kufanya hivo. Mfano mrahisi tu, mfano wa Risk Aversion ni tukio alilolifanya Godbless Lema, kama binadamu alikuwa na hisia maisha yake yapo hatarini, na mwisho wa siku alifanya decision ya kukimbia, tukio la kukimbia ndilo tunaliita risk aversion. Japo binadamu tunauwezo wa ku take risk, lakini naturally kuna level fulani ya risk mtu hutaweza kuichukua, na ndo hapo ni lazima uta make final decision.

Bila kwenda mbali sana, maono yangu kwa wanachofanya TRA ni kwamba yanaenda kutrigger 'Risk aversion' kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Na hii kitu inatokea naturally but gradually. Ukiangalia takwimu za capital flow in and out of Tanzania, unaweza uka trace hii propensity ya Risk aversion ambayo naizungumzia hapa. Watu wataogopa ku invest, watu wataogopa kufanya biashara kwa sababu wanakuwa na hisia kwamba kuna risk ambayo hawawezi kuibeba na inakuja.

Tutashuhudia biashara kufungwa, ama kama sio kufungwa kutakuwa na dis-investment. Yaani biashara zitakuwepo lakini zitakuwa zinaendeshwa below capacity ili tu waangalie kama hali itabadilika in the future.

Kuondoa hii 'Risk aversion' ambayo imeletwa vyombo vya serikali, Alan Greenspan kuna mahali aliandika 'The lessening or the end of uncertainty is like the lifting of the fog'. Ili hizi uncertainty zimalizwe unahitaji kuwa na stateman ambaye anaweza kuona mambo in three dimension, mwenye kuelewa vema, the cause and effect. Bado sioni hichi kiti kama kitatokea in next 5 years, which means sioni mabadiliko yoyote mapana zaidi ya kwamba tunanyemwelewa na msukosuko wa kiuchumi ambao unatengenezwa na government machinery.

Na N.Mushi
 
Ahasante kwa kutuelimisha,tuna utawala unaojua kila kitu bialashaka na hili wanalijua na watalishinda kama walivyoshinda vita vyote walivyopigana kwa mujibu wa mtoa macho wa mambo ya nchi za nje
 
Hii ni kweli biashara nyingi either zinafungwa au zinapunguza shughuliza operation.
Hiyo ndo naiita dis-investment ukitaka ku prove hicho kitu angalia balance sheet za makampuni mengi.. Wame scale down capital expenditure in recent years ikimaanisha kwamba kuna impending risk ambayo investors na wafanya biashara wanaiona Tanzania.

Ubaya wa analysis za kiuchumi ni kwamba zinakupa indicators, gradually ni kama ilivo 'time bomb'.. kuna viashiria vingi sana vipo mezani.. but surely mda unavokwenda mambo yanakuwa dhahiri.
 
Ahasante kwa kutuelimisha,tuna utawala unaojua kila kitu bialashaka na hili wanalijua na watalishinda kama walivyoshinda vita vyote walivyopigana kwa mujibu wa mtoa macho wa mambo ya nchi za nje

Binafsi nafanya biashara tena kubwa sana,lakini taratibu nimejikuta napunguza kwa kiasi kikubwa heka heka za biashara kwasababu Bwana mkusanya kodi tayari kanijeruhi pakubwa.Ninawafahamu wafanybiashara wengi wakubwa karibu wote wameumizwa na kodi kubwa ambazo zimewalazimisha kubadili au kuacha kabisa biashara.
 
Back
Top Bottom