Maafisa wa kijeshi wa Ukraine wamedai kuwa takriban wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa tangu Rais Vladimir Putin alipoanzisha uvamizi wake zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Katika sasisho lililotumwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wafanyikazi wakuu wa Ukraine, maafisa walisema kuwa wanajeshi 14,700 wa Urusi wameuawa katika siku 25 za mapigano.
Taarifa hiyo pia ilidai kuwa kiasi kikubwa cha vifaa vya kijeshi vya Urusi vimeharibiwa katika mzozo huo, vikiwemo takriban vifaru 476, zaidi ya ndege 200 za kivita, helikopta na ndege zisizo na rubani na karibu wabeba silaha 1,487.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai haya kibinafsi hili, ijapokuwa vyanzo vya Magharibi vinaamini kuwa Urusi imepata hasara kubwa na maafisa wa ulinzi wa Marekani wamekadiria kuwa takriban wanajeshi 7,000 wa Urusi wameuawa wakiwa vitani, huku wengine karibu 21,000 wakijeruhiwa.