Ukraine yadai kuwaua wanajeshi 15,000 wa Urusi

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,274
15000.jpg

Maafisa wa kijeshi wa Ukraine wamedai kuwa takriban wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa tangu Rais Vladimir Putin alipoanzisha uvamizi wake zaidi ya wiki tatu zilizopita.

Katika sasisho lililotumwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wafanyikazi wakuu wa Ukraine, maafisa walisema kuwa wanajeshi 14,700 wa Urusi wameuawa katika siku 25 za mapigano.

Taarifa hiyo pia ilidai kuwa kiasi kikubwa cha vifaa vya kijeshi vya Urusi vimeharibiwa katika mzozo huo, vikiwemo takriban vifaru 476, zaidi ya ndege 200 za kivita, helikopta na ndege zisizo na rubani na karibu wabeba silaha 1,487.

BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai haya kibinafsi hili, ijapokuwa vyanzo vya Magharibi vinaamini kuwa Urusi imepata hasara kubwa na maafisa wa ulinzi wa Marekani wamekadiria kuwa takriban wanajeshi 7,000 wa Urusi wameuawa wakiwa vitani, huku wengine karibu 21,000 wakijeruhiwa.
 
Hapa sasa sawa habari zitakuwa zina balance mana niliposikia Mrusi kapiga Hypersonic bomb nilishaanza joto joto
 
Ha ha ha ha.mtu anapigika huko ,wao wameamua kuhamishia Vita mitandaoni wakiamini progamda huenda zitawafanya warusi wamgeuke Putin,na ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.siku Ukraine yote itakapokuwa chini ya russian ,Tena BBC watakuja na propaganda nyingine! marekani muoga Kama waoga wengine
 
Us aingie vitani kama nani?
Ukraine sio mshirika wa moja kwa moja wa Us.
 
Ha ha ha ha.mtu anapigika huko ,wao wameamua kuhamishia Vita mitandaoni wakiamini progamda huenda zitawafanya warusi wamgeuke Putin,na ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.siku Ukraine yote itakapokuwa chini ya russian ,Tena BBC watakuja na propaganda nyingine! marekani muoga Kama waoga wengine
Time will tell.
 
Kijeshi tia tia maji ilitakiwa kiwe chali mpk leo hii sijui Urusi wanakwama wapi, bila hata silaha kubwa kubwa wangekimaliza mapema nashangaa hadi leo wanakwama kwann lkn?
 
Anajiweza wakati Moscow wanapanga folen saiv kununu sukari
WaBelarus wanafanya nini Ukraine? Unafikiri wameenda kutalii?? La hasha bali wameenda kumsaidia baba yao baada ya maji kuzidi unga. Lakin bado haijasaidi na Sasa unahitajika msaada wa mchina lakin mchina naye kachomoa.
 
Back
Top Bottom