Ukosefu wa dawa hospitalini = Serikali imefilisika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukosefu wa dawa hospitalini = Serikali imefilisika?

Discussion in 'JF Doctor' started by QUALITY, Sep 29, 2011.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wana JF,

  Ninayo masikitiko makubwa kuwataarifu kuwa jana nilifanya utafiti mdogo wa hali ya upatikanaji wa dawa katika hospitali zetu za umma. Hospitali za serikali Kyela, Rungwe, Kinondoni, Temeke na Ilala, zaidi ya 70% hazikuwa na dawa.

  Nilienda hospitali iliyoko manispaa ya temeke physically iitwayo vijibweni ambapo hawakuwa na hata panado, hawana drip hata moja, dawa za malaria (mseto) hakuna, gloves hakuna, vifaa vya kujifungulia (kule matenity ward) hakuna!

  Nikaondoka nikaenda kituo cha afya cha Kigamboni karibu na kituo cha polisi. hawana dawa yoyote. wanacoweza kufanya ni kukuandikia karatasi tu na kukutuma uende kutafuta dawa mahali popote. Kwa taarifa yak0 hata vyeti (printed cards) hakuna kwa hiyo wanakata makaratasi ya kawaida ndiyo wanayotumia kuandikia.

  Nikatoka hadi hospitali ya Ilala, hakukuwa na dawa.

  swali: Je hii si dalili kuwa serikali yetu imefirisika?
  karibu kwa critical thinking

  Quality
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Mkuu hilo ni la kweli juzi tulikuwa na mgonjwa temeke hosp hatuweza kupata hata hiyo panadol hali inatisha !
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hamna dawa mkuu.utafiti wako upo sahihi.mi nimeenda pale kurasini hospital ya polisi pale baracks hawana dawa kabisa.wanakuandikia uendekununua mtaani.mtaani unakutana na madawa feki.safari hii tutakoma.mia
   
 4. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Utafiti wako ni batili, mimi nipo MSD Dodoma.
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  tuwekee picha hapa na utoe maelezo ya kusema utafiti ni batili.msd dar wanalia itakuwa huko dom.na wewe kuwepo msd dodoma sio kigezo cha kupatikana kwa dawa au wewe kuwepo huko kuna uhusiano gani na uwepo au ukosefu wa madawa?.hata ungesema upo msd makao makuu.mia
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu alijua mtatishika labda.. hivi kwanini hospitali nyingi mbele yake yaani kwenye milango mikuu kuna kuwa na maduka ya dawa sio ndio ile janja ya nyani..
   
 7. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ipo kazi
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Sasa naelewa kwa MSD wanachemsha...kumbe mmeja akina Mwita huko (utani huu umekaa kisiasa zaidi na sio kitaaluma!)..

  Pamoja na serikali kutokidhi mahitaji ya dawa kwa kila mtanzania...lakini nadhani kuna tatizo kubwa pale MSD, kubwa sana! Kuan kipindi nilikuwa na wafadhili katika vita dhidi ya malaria kwa kina mama wajawazito, tukapitia vituo kadhaa vya huduma za afya vya serikali Morogoro vijijini, hakukuwa hata na SP tu kwa ajili ya IPTp. Wafadhili wale wakajitolea wanunue dawa kibao (SP ni cheap sana), kasheshe tulipofika wizara ya afya wakatuuliza kwani mmeambiwa hatuna SP? Wakatupeleka MSD central store...SP zimejaa tani kwa tani...wakati mama zetu/wake zetu/dada zetu wanakufa kwa malaria in pregnancy! Mwita, play your part...acha kuchonga tuu kuhusu Chadema hapa JF kazi hamtaki kufanya!
   
 9. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MSD siyo hospitali. Kama mna dawa katika stoo zenu, wagonjwa waanakufa mahosptalini, basi ninyi hamfai. Bahati nzuri wengi waliofika katika hospitali zote hawakupata dawa. hata drip moja hakuna!!!!!!!
   
 10. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wamezidi longo longo. Wanafurahia kuwepo kwa dawa MSD hadi zitaexpire!
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Dawa zinaharibika bohari kuu dar.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Sasa kama Serikali imeshindwa kuziendeleza hizo Hospitali kwanini wasiwape watu Binafsi waka ziendeleza hizo Hospitali? Jamani Serikali inawauwa watu wake kidogo kidogo, bora waseme tu hospitali za bure hakuna kuna hospitali za kulipia tujuwe kuwa Serikali imeshindwa kuwahudumia wananchi wake ahhhh jamani tutafika kule tunakokwenda?
   
Loading...