Ndugu nimekuwa nafuatilia sana post zako na haina shaka wewe ni mwanachama wa CHADEMA. Takupa udhaifu mmoja hai mmoja unaokikumba chama chenu na amini kabisa ninachokuambia.
Unakumbuka katika mkoa wa Shinyanga halmashauri ya Msalala mlikuwa na diwani mmoja tu wa CHADEMA aliyekuwa kata ya BUGARAMA BULYANHULU, huyu pamoja na kuwa peke yake kukibeba chama chenu si Mbowe wala kiongozi yoyote aliyewahi kwenda japo kumsikiliza changamoto zake za kisiasa hata zile za kifamilia (uchumi) ukizingatia alikuwa peke yake na hivyo chama kingemuona kama mtu muhimu na sioni sababu hata kwa nini viongozi wote wangelikuja hata siku moja kumsalimia na kumtia nguvu lkn hakuna lolote lililofanyika hadi akazidiwa nguvu na kuamua kuunga juhudi za Jiwe. Si hivyo tu soon hata mwenyekiti wa kijiji cha Kakola ulipo mgodi wa Bulyanhulu atajiunga hivi karibuni maana hana msaada wowote wa chama isipokuwa viongozi wako Dar tu wanakula bata. CHADEMA ya sasa ni dhaifu mno na inaishi kwa kulalamika tu kwani kila siku napata updates za kinachoendelea. Amini Waitara atapita kwa kura nyingi tu kwani CCM haitegemei kura za majukwaani yenyewe inazifuata nyumba kwa nyumba kupitia mabalozi