Ukondefu unaninyima amani nifanyeje ili nipate walau vinyama kidogo

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
1,142
2,000
Aisee kumbe mawazo yangu yalikua sahihi bna .
Huwa naona kuna watu ni wembaba mnoo mpaka unajiuliza huyu upepo ukivuma haumbebi kweli!!?
Kumbe wengi wao hawaipend ile hali aisee daah .

Na kuna wanene pia aisee, yujitahidi tuwe wastani tu jama
 

mibiki mitali

Member
Feb 5, 2018
91
150
Yani unashindilia nyama na bia on a daily basis hunenepi? Kweli binadamu tunatofautiana.

Watu tuna 130kgs hapa. Hatukutumia mwezi kufika hapa. Inabidi ule heavily na ule vizuri (NYAMA) kila siku ya maisha yako. Hata kilo 200 utafika. Pia gonga sana sugary foods, soda, keki, mavitu ya supermarket yenye sukari.

Always kunenepa au kukonda hakutakiwi temporay adjustment in meal habits ila permanent one.
Au ukute mwamba Ana roho ya korosho, wivu kwa wenzake na vilawama vya hpa na pale. Tungemuuliza na tabia yke ikoje in society
 

mibiki mitali

Member
Feb 5, 2018
91
150
We kula vitu vya sukari na mafuta tu ila nyama ndio nzuri kwa kujaza misuli. Hakikisha hukosi bakuli ya supu ya ng'ombe deile.

Mchana ugali na nyama ya kitimoto roast.

Jioni kuku choma na chips zitakufaa sana mkuu. Huku ukisindikizia na malta.

Nakupa mwezi na nusu tu, ulete majibu hapa.
Penye mshahara Sasa,
 

kuuuu

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
463
500
Weee Jamaa acha kumkufuru Mungu unawajua vimbaumbau wewe???? Mamaee mpaka misuli naiona unataka Ubonge upeleke wapi????? Sasa huo ulionao ndo mwili wa kiume labda kama demu wako kasema usiponenepa anakuacha Ukapagawaa ukaja mbiombio huku kuomba ushauri kwa kitu cha kijinga..

UBONGE HAULIPI...huo ndo mwili wa kiume acha kuendeshwa na MWANAMKE.
big up bonge na advice babu,,,***** ka hatafuata huu ushaul bora amuache tu huyo anaemdanganya
 

Diego Maradona

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
507
500
Asante mkuu nimedandia huu ushauri, mi mwenyewe ni mwembamba hadi naogopa kupima uzito ingawa nachukulia poa tu sijawai kujishughurisha na hilo, ila ushauri wako nitaufanyia kazi na mimi nione.

Duh! Unapotezwa hivi hivi unajiona.. unashauriwa kutumia kilevi, kijana zinduka!

Ushauri wangu, tafuta mtaalam wa kuongeza uzito, atakushauri vyakula gani vya kutumia na visivyotakiwa kutumiwa..
 

nana_

Member
May 17, 2021
17
75
HABARI WAKUU.
Wakubwa kwa Wadogo salamu kwenu
Mimi ni kijana mwenye 28 years..!

Tatzo langu ni uwembamba uliopitiliza natamani walau na mimi niwe na vinyama kidogo. Nakumbuka mwaka jana niliwahi kupima uzito wangu nikawa 48kg uzito wa Jogoo la kienyeji iliniuma sana nilikaa wiki zima nikitafakari hatma ya afya yangu hadi hapo nilipoenda kupima magonjwa yote nikakutwa nipo smart sina tatzo la kiafya!

Nikaamua kujianzishia Dozi ya kula matunda kila baada ya chakula na mara kwa mara hali ambayo ilikuwa inanigalimu kila siku kutumia galama zaidi ya elfu kumi 10,000 kwa ajili ya Kuimalisha Afya yangu pia nilipata ushauri wa kula kitimoto na Bia moja kila siku! Hali ambayo sikuona shida nilikuwa nafanya hivyo hadi kujikuta nakuwa mlevi wa bia, Maana nilikuwa nakunywa bia moja kwa ajili ya Afya ila hatmae nikajikuta nakunywa bia zaidi ya 5 kwa siku maana tabia ya Bia nilikuwa nikinywa moja natamani kuongeza nyingine na nyingine hadi nikajikuta nakuwa mlevi pasipo kukusudia hali hii ilikuwa inanipelekea kukosana na watu wanaonizunguka kila nikinywa pombe nawatambia majirani zangu kuwa hawana hela na kusababisha fujo hadi nyumbani kwangu! Ikabidi nijishauri mwenyewe nakuacha dozi hii kwa sasa situmii tena.

Ila katika kumbukumbu zangu kipindi nafanya haya walau nilianza kuona mabadiliko kidogo ya afya mwilini mwangu nikaanza kutokeza kakitambi kwa mbali na kunenepa shavu na nilipopimwa uzito nilikuwa nimefikisha 60Kg hadi watu walianza kuniambia nimenenepa pasipokujua hiyo hali inaniingiza galama kiasi gani!

Nilikuwa nimeanza kunyanyua kakibanda kangu ila nilisimamisha shughuli ya ujenzi, pesa yote niliokuwa napata katika mihangaiko yangu ikawa inatumika kwa ajili ya kufanyia kile ninachokitamani, baada ya kuacha tena dozi hii kwa sasa nimepururuka vibaya mno jana nimepima uzito nakuta 52kg tu na kila kukicha nazidi kukonda tena!

Nimeamua kuja hapa ili wataalamu mnipe namna ambayo itakuwa si ghali sana ambayo nitatumia ili ninenepe huu ukondefu unaninyima michongo mingi sana!
Atakaeweza kunisaidia nipo tayari kumlipa!

khaaa mi nimecheka kama mazuri. Kwanza nikuulize…ushanenepa au bado? Mi hapa nawaza kukonda ww unawaza kunenepa…kweli life isn’t the same
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom