Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Hapana hili halihusiani na magwanda wala magamba linatuhusu Watanzania wote. Hivi kweli dada wewe hili linakuingia akilini eti ktk kundi la watu milioni 45 hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kuwa Mkuu wa kaya ya Tanzania. Maana ndiyo hoja iliyopo mezani kuwa uondolewe ukomo wa kuwa madarakani.Hili ni rungu kwa magwanda.
mkuu naona katika wote , wewe ndio umechangia mada ya msingi katika uzi huu.Mkuu usishangae ambao wanachangia nje ya mada, nina uhakika mada wameielewa kuliko hata wewe mwenyewe unavyoielewa! watu wana mambo mengi kiasi kwamba wakati fulani yanagongana ndani ya vichwa vyao wenyewe.Tehe!Hapana hili halihusiani na magwanda wala magamba linatuhusu Watanzania wote. Hivi kweli dada wewe hili linakuingia akilini eti ktk kundi la watu milioni 45 hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kuwa Mkuu wa kaya ya Tanzania. Maana ndiyo hoja iliyopo mezani kuwa uondolewe ukomo wa kuwa madarakani.
Hoja hii kwangu mimi na haina mashiko, vinginevyo Watz watakuwa wameamua kuwatengeneza akina Museven, Mugabe Gaddaffi na Mubarak wa Tanzania. Tusiangalie makundi watanzania wote tutaonekana hatuna akili kabisa tukiruhusu hoja kama hii ipite na kuwa sheria!!!!!
Vipi chadema na vyama vingine unadhani watakubali na kama ndio kwa nini na kama sio kwa nini?Kwa watakaokubali au kukataa, unadhani itakuwa ni kwa maslahi ya taifa au yao wenyewe?Kwanza CCM kwenyewe hakuna atakayekubali hoja hii.
betlehem sio mjinga mnavyomfikiria ila najua hata yeye kichwani kwake anajua sio jambo jema katika nyanza ya demokrasia.Mwl Nyerere tulimuona kama malaiki na hata alivofariki wengine tulilia tukiona tutaishije? lakini ukweli bado tupo bila yeye na mungu anatusaidia.Mwenyewe alishakiri kuwa sisi binadamu sio malaika hata uwe mzuri vipi kuna makosa utatenda sababu sote tuna nyama na damu cha muhimu ni ku copy and paste mazuri na tunadelete mabaya.Tutashangawa hata na mataifa mengine sababu nchi yetu is not a monarch.betlehem hapa anajaribu tu kuwasha kijinga cha moto kuona moto utakavowaka na kuona mawazo ya watu msimpinge kwa wazo lakeMzee Mwinyi naye kaona umuhimu wa jambo hili
Kama tumefikia hatua ya kukosa mtu mwenye sifa ya kuwa rais basi tufanye marekebisho ili katiba ijayo iruhusu wanyama kama punda,nyani,ng'ombe na wengineo nao wagombee urais ili watuongoze sababu kuna uwezekano wakawa na akili,uwezo na uzalendo kutuzidi sie binadam 49ml kuliko kuongeza vipindi vya utawala kiongozi kama tuliye naye ambaye bila kupepesa macho hakuna ambaye hajui kuwa ni mzigo kwa taifa.
Mbona Mbowe anafanya hivyo CHADEMA huko haijatosha?Hatutaki kuanzisha monarch style. Mwalimu Nyerere alifanya hivyo imetosha.