Ukomo wa Rais kugombea uondolewe. Maadam atakuwa na sifa, agombee bila kikomo

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Wadau inaonekana tunafanya jambo moja katika level ya vyama lakini katika level ya taifa hatujatilia manani jambo hilo.


Nadhani ipo haja ya kuondoa kipengele cha Rais wa Jamuhuhuri ya muungano kugombea kwa vipindi viwili tu!, na kinyume chake rais aruhusiwe kugombea urais bila kikomo.

-Kwa kuwa jambo hili tumeliona linafaa katika level ya vyama vyetu, nadhani vile vile linafaa katika level ya nchi kwa kuwa ni zuri.

-Kwa kuwa jambo hili tumeweza kulifanikisha katika level za vyama, bila shaka vile vile tuna uwezo wa kulikamilisha katika level ya nchi.

-Kwa kuwa jambo hili tumeliunga mkono kwa nguvu moja katika level za vyama, bila shaka tutalikunga mkono katika level ya nchi vile vile kwa kuwa vyama hivi hivi ndio vinavyoongaza/vinavyotaraji kuongoza nchi.

===========
Update 2017
============
Mzee Mwinyi naye kaona umuhimu wa jambo hili
 
Kama tumefikia hatua ya kukosa mtu mwenye sifa ya kuwa rais basi tufanye marekebisho ili katiba ijayo iruhusu wanyama kama punda,nyani,ng'ombe na wengineo nao wagombee urais ili watuongoze sababu kuna uwezekano wakawa na akili,uwezo na uzalendo kutuzidi sie binadam 49ml kuliko kuongeza vipindi vya utawala kiongozi kama tuliye naye ambaye bila kupepesa macho hakuna ambaye hajui kuwa ni mzigo kwa taifa.
 
Ni wazo zuri hasa kwa nyakati za usiku ila mchana ni moja ya wazo bovu kabisa. Ndg mleta mada hebu jaribu kufikiri jinsi watu wanavyopigana vikumbo ili kuipata hiyo nafasi. Kwa hakika ikitokea tukapata rais mbovu, basi ina maana huyu atatutawala hata kwa miaka mia na kisha atamrithisha mwanawe kiti maana atatumia pesa kuwanunua watu kama tunavyoona sasa ktk chama fulani jinsi watu wanavyonunuliwa, kisha wanaanza kuwasifu watu wao na kututangazia kuwa huyu ndiye anayefaa wakati hata rekord zao kiutendaji zimeoza. HILI SIO WAZO JEMA KWA NCHI
 
Hili ni rungu kwa magwanda.
Hapana hili halihusiani na magwanda wala magamba linatuhusu Watanzania wote. Hivi kweli dada wewe hili linakuingia akilini eti ktk kundi la watu milioni 45 hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kuwa Mkuu wa kaya ya Tanzania. Maana ndiyo hoja iliyopo mezani kuwa uondolewe ukomo wa kuwa madarakani.

Hoja hii kwangu mimi na haina mashiko, vinginevyo Watz watakuwa wameamua kuwatengeneza akina Museven, Mugabe Gaddaffi na Mubarak wa Tanzania. Tusiangalie makundi watanzania wote tutaonekana hatuna akili kabisa tukiruhusu hoja kama hii ipite na kuwa sheria!!!!!
 
Kwanza CCM kwenyewe hakuna atakayekubali hoja hii, kwa kuwa ndani ya CCM kuna watu wengi sana wanaoweza kuwa Rais, nje ya CCM kuna wengi wanaoweza kuwa Rais, hakuna ushahidi unaoonesha kuwa tunaweza kukosa Rais mwaka 2015 kutokana na system iliyopo sasa, kutokana na nchi ilivyokuwa wakati Mkapa anaondoka madarakani na alivyo sasa, hoja yako ya pili inakumbana na maswali mengi sana, kama unaona nchi hii ni changa na ni tepetepe basi kwa maana nyingine ni kuwa katika miaka 10 iliyopita huyu rais alieacha nchi iwe changa na tepetepe basi angeifanya ikue na isiwe tepetepe, kwa kuwa hajafanya hivyo basi tunahitaji mwingine.
 
Hapana hili halihusiani na magwanda wala magamba linatuhusu Watanzania wote. Hivi kweli dada wewe hili linakuingia akilini eti ktk kundi la watu milioni 45 hakuna mtu mwingine mwenye sifa za kuwa Mkuu wa kaya ya Tanzania. Maana ndiyo hoja iliyopo mezani kuwa uondolewe ukomo wa kuwa madarakani.

Hoja hii kwangu mimi na haina mashiko, vinginevyo Watz watakuwa wameamua kuwatengeneza akina Museven, Mugabe Gaddaffi na Mubarak wa Tanzania. Tusiangalie makundi watanzania wote tutaonekana hatuna akili kabisa tukiruhusu hoja kama hii ipite na kuwa sheria!!!!!
mkuu naona katika wote , wewe ndio umechangia mada ya msingi katika uzi huu.Mkuu usishangae ambao wanachangia nje ya mada, nina uhakika mada wameielewa kuliko hata wewe mwenyewe unavyoielewa! watu wana mambo mengi kiasi kwamba wakati fulani yanagongana ndani ya vichwa vyao wenyewe.Tehe!
 
Kwanza CCM kwenyewe hakuna atakayekubali hoja hii.
Vipi chadema na vyama vingine unadhani watakubali na kama ndio kwa nini na kama sio kwa nini?Kwa watakaokubali au kukataa, unadhani itakuwa ni kwa maslahi ya taifa au yao wenyewe?
 
Hatutaki kuanzisha monarch style. Mwalimu Nyerere alifanya hivyo imetosha.
 
Mzee Mwinyi naye kaona umuhimu wa jambo hili
betlehem sio mjinga mnavyomfikiria ila najua hata yeye kichwani kwake anajua sio jambo jema katika nyanza ya demokrasia.Mwl Nyerere tulimuona kama malaiki na hata alivofariki wengine tulilia tukiona tutaishije? lakini ukweli bado tupo bila yeye na mungu anatusaidia.Mwenyewe alishakiri kuwa sisi binadamu sio malaika hata uwe mzuri vipi kuna makosa utatenda sababu sote tuna nyama na damu cha muhimu ni ku copy and paste mazuri na tunadelete mabaya.Tutashangawa hata na mataifa mengine sababu nchi yetu is not a monarch.betlehem hapa anajaribu tu kuwasha kijinga cha moto kuona moto utakavowaka na kuona mawazo ya watu msimpinge kwa wazo lake
 
Kama tumefikia hatua ya kukosa mtu mwenye sifa ya kuwa rais basi tufanye marekebisho ili katiba ijayo iruhusu wanyama kama punda,nyani,ng'ombe na wengineo nao wagombee urais ili watuongoze sababu kuna uwezekano wakawa na akili,uwezo na uzalendo kutuzidi sie binadam 49ml kuliko kuongeza vipindi vya utawala kiongozi kama tuliye naye ambaye bila kupepesa macho hakuna ambaye hajui kuwa ni mzigo kwa taifa.

Ni mzigo kwa waliokuwa wakiliibia Taifa.Kwa wapenda haki MUNGU ametupa mtu sahihi wakati sahihi na kamweka mahali sahihi.Tunamshukuru MUNGU kwa wema wake.Pamoja na uzalendo uliotukuka wa Mh.Rais wetu JPM siafiki ndoto ya kubadili katiba.Ninauhakika uchaguzi ujao atapata kura nyingi zitakazomshangaza hata yeye na kuzima keleleza walalmikaji wa kuibiwa kura za ndotoni,lakini kipindi chake cha pili kikiisha tunategemea atakuwa ametengeneza misingi mizuri ya kudhibiti wanaomfuata na kuweka vizibo kwenye mianya yote ya rushwa.

Ninaungana na wanashauri kuwa katiba iliyopendekezwa na tume ya Waziri Mkuu mstaafu asiye na tone la wizi na ubadhirifu wa mali zetu Mzee Joseph Sinde Warioba ikamilishwe bila tone la hila kwa manufaa mapana ya nchi yetu.
 
Yeye kama anataka kuendelea akubali 2025 aingie rais mwingine yeye awe waziri mkuu halafu 2030 agombee aendelee hadi 2040 kama Mungu atakubaliana naye. Urusi walifanya hivo kwa Putin
 
Mimi nahisi kutokana na ufinyu wa demokrasi wizi wa kura na figisu figusi za uchaguzi katiba ingebadilishwa ili chama cha siasa kisiruhusiwe kuongoza nchi zaidi ya miaka 10 maana yake ukiongoza miaka 10 uchaguzi ufuatao usisimamishe mgombeawa urais hii itasaidia kuondoa chama kilichotawala miaka zaidi ya 50 bila Msaada wowote kwa wananchi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom