BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,124
Ukomo wa ajira vyeti feki huu
www.ippmedia.com/sw/habari/ukomo-wa-ajira-vyeti-feki-huu-0
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angella Kairuki, alisema wale ambao hawatawasilisha vyeti hivyo kwa ajili ya kuhakikiwa watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Waziri Kairuki alisema hayo wakati wa mkutano wa mwaka wa watendaji wakuu wa wakala 32 za serikali nchini kuwa watumishi hao wawe wamewasilisha vyeti vyao au ‘index’ namba kama hawana vyeti.
Alisisitiza kuwa maofisa watendaji wakuu wa wakala za serikali, idara, taasisi za umma na wakurugenzi wawahimize watumishi wao kufanya hivyo.
Kairuki alibainisha kwamba wengi watumishi wa umma wanaghushi vyeti, huku akitoa mfano kwamba kuna mtumishi mmoja wa umma amegundulika kughushi cheti cha shahada ya uzamili (masters).
Kwa mujibu wa Waziri, mtumishi huyo alighushi cheti hicho na kwamba alipata kazi ndani ya serikali huku akijua hajasoma na kufika ngazi hiyo ya elimu.
Alisema baada ya kumalizika kwa muda uliotolewa kwa wafanyakazi kujihakiki, alisema ajira za serikali zitaanza kufunguliwa na kwamba waraka maalum wa serikali umesambazwa kwa kila idara.
“Haiingii akilini mtendaji mkuu anaongoza wakala wenye watumishi 100 au 200, lakini unakuwa na watumishi hewa. Lazima muwe makini, kila mmoja alisimamie hili maana tumekwishapoteza rasilimali fedha kubwa ya serikali," alisema.
Alibainisha kuwa pamoja na mahitaji makubwa ya watumishi katika taasisi za umma, bado watendaji wakuu wanatakiwa wajiridhishe kwa kufanya uhakiki, tathmini iwapo watumishi wanahitajika kwa kuwa hakuna kumbukumbu rasmi zinazoonyesha idadi halisi ya mahitaji.
Kati ya maeneo ambayo yana ajira zinazotia shaka, alisema ni wakala za serikali na baadhi ya taasisi, hatua inayosababisha gharama kubwa kwa serikali katika kuajiri wafanyakazi wa muda walio na mikataba maalum.
Hadi Agosti, mwaka jana, serikali ilibaini kuwapo kwa watumishi hewa 16,127 nchini na kwamba ajira 71,496 zitatolewa katika mwaka wa fedha 2016/17 baada ya kumalizika uhakiki unaoendelea.
Kairuki aliwaagiza watendaji hao kujiweka vyema kwa kuwa na matumizi sahihi ya fedha za umma, kuandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji wao wizarani.
Alisema kumekuwa na matumizi ya fedha na rasilimali kinyume cha maadili, ikiwamo magari ya umma, kujilipa fedha kubwa kwa ajili ya likizo bila kufuata kanuni na kwamba wakala za serikali zitimize sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245, inayoainisha majukumu, ikiwamo kuzishauri wizara.
Sambamba na hilo, alisema kumekuwa na taarifa chafu za watumishi kuwa na matumizi mabaya ya madaraka na kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji wa kazi. Kutokana na hali hiyo, alisema serikali imejipanga kuondoa urasimu na kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi.
Kairuki alisema changamoto kubwa katika wakala ni mawasiliano duni kati ya wizara na wakala na kwamba baadhi ya taarifa zimekuwa hazifanyiwi uchambuzi na kutoa mrejesho.