Ukomo wa ajira vyeti feki huu

Ukomo wa ajira vyeti feki huu

Waambie mbona Ile taasisi ya nyokanyoka[emoji61](magamba magamba) hawaendi kuhakiki?au wanaogopa dunia duara[emoji288]
 
Katibu Mkuu na Watendaji Wakuu; Eneo lingine ninalopenda kuligusia ni kuhusu kuwepo kwa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali wanaokaimu nafasi zao kwa sababu mbalimbali. Hali hii siyo nzuri kwani inazorotesha utendaji wa Wakala hasa katika kufanya maamuzi. Niagize Ofisi yangu kupitia Katibu Mkuu kufanya uchambuzi na kuniletea taarifa ya Watendaji Wakuu wote wanaokaimu, sababu za kukaimu na mapendekezo ili tuchukue hatua mara moja. Kama sababu zipo kwa Wizara mama tafadhali wakumbusheni wajibu wao na kama sababu ni ndani ya Ofisi yangu tafadhali Katibu Mkuu na Wataalam wako simamieni suala hili tumalize suala la watumishi kukaimu muda mrefu. Aidha, kwa nafasi za Wasaidizi wa Watendaji Wakuu wa Wakala wanaokaimu lipo chini yenu nyie Watendaji Wakuu. Ni vizuri kila Mtendaji Mkuu afuate taratibu husika ili kujaza nafasi hizo kwani kufanya hivyo kutawapunguzia mzigo ninyi wenyewe katika kuendesha na kusimamia Wakala zenu. Ndugu Katibu Mkuu na Watendaji Wakuu wa Wakala; Nafahamu kwamba moja ya changamoto kubwa inayozikabili

Wote tunafahamu kuwa Serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha zoezi la kuondoa Watumishi hewa. Ninafurahi kusema kuwa zoezi hilo limekwishafika ukingoni na hivi karibuni mtajulishwa kurudisha rasmi kwa ajira. Pamoja na hayo niwatake Watendaji Wakuu kuweka mikakati ya kusaidia tusirudi tulikotoka kuhusu suala la Watumishi hewa. Haingii akilini Mtendaji Mkuu unaongoza Wakala yenye watumishi wasiozidi 100 au 200 lakini unakuwa na Watumishi hewa. Simaanishi Wakala zenye watumishi wengi ziwe na Watumishi hewa bali matarajio yetu kwenu ni makubwa kwamba mtakuwa makini zaidi kama sehemu ya kujitofautisha na Idara na Taasisi zingine za Serikali zenye tatizo hili. Naomba kila mmoja alisimamie kwa dhati suala hili maana limetuumiza na kupoteza rasilimalifedha nyingi sana za Serikali. Sambamba na hilo, ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki. Yuko mtumishi mmoja katika Wakala fulani ambaye alikuwa na cheti ‘Fake’ cha Shahada ya Kwanza na Shahada ya Uzamili. Watakeni watumishi wenu wote wawasilishe vyeti vyao vya elimu na taaluma au ‘Index Number’ za mitihani yao ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Watumishi watakaoshindwa kufanya hivyo ifikapo tarehe 1 Machi, 2017 watakuwa wamejiondoa
 
Kwani umeambiwa miongoni mwa wenye vyeti feki watoto wa masikini hawamo?
Mtoto wa Masikini Cheti feki atakipatia wapi? Tunapohoji tuwe tunajaribu kufikiria kwanza. Kwanza Fake Certificate inategemea na Uchumi wa mtu. Maana Cheti hicho hununuliwa kwa gharama kubwa.
Upo wewe unayehoji?
 
[29/01 08:45: HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA...
Chief watu wengine tunatumia simu badala ya kuweka waraka wote utakaochosha, hebu leta vipengele ambavyo unaona vinafit kwenye huu uzi.
 
huyu mama kapata cheo kupitia jina lake tu ni fadhila
 
Najuta kuwa mtumishi wa serikali ya tz,later on i can think twice to surrander.
 
Chief watu wengine tunatumia simu badala ya kuweka waraka wote utakaochosha, hebu leta vipengele ambavyo unaona vinafit kwenye huu uzi.
kuhusu swala la ajira mtoa post amepotosha kairuki kasema vingine
 
Anajihakiki na yeye maana haamini vyeti vyake.
 
Kinacho nishangaza kuna watu hawana vyeti na wengine wana share vyeti na wengine wanvyo feki bado wapo na wanalamba salaries kama kawa sijui walikuwa wana hakiki nini maana hata siwaelewi hawa watu ,nguvu nyingi matokeo hakuna.
umesaidiaje kwenye hili wewe,umetoa tarifa takukuru au polisi?
 
Yaani hamna jipya, hizi zote ni kutafuta tu njia ya kujisitiri ili waendelee kutunyima haki zetu.Zoezi la kuwasilisha nakala za vyeti tumelifanya kama mara 3 hivi ndani ya miezi kama 2 sasa leo unakuja na mdomo maneno mengi.
Watumishi wa umma wanachowaza wanakijua wenyewe, si wote waoga kama mnavyofikiri.
Huu wimbo tumeuchoka
 
Kwa nini Mtu anakuwa na Vyeti feki?
Kwa nini mtu ashangae mwenye vyeti feki anapochukuliwa hatua?
Kwa nini mwenzako ahangaike kusoma wewe ukae tu baadae yeye akae nyumbani wewe ukae kwenye kiyoyozi?

Hii imesababisha watoto wa masikini KUCHUMIA JUANI NA KULIA JUANI.
Wafukuzwe tu, hakuna namna

kwa kauli yako nazani wewe ni mzee wa miaka si chini ya 72, no offence
 
Back
Top Bottom