Ndugu wana JF, tumeshuhudia Chadema wakitoa kauli kali na ngumu kuwa CCM imeamua kutumia umafia wake wote kuhujumu democrasia nchini, kuanzia vyombo vya dola, wakuu wa mikoa, wilaya na viongozi wa kata, tarafa na vijiji. Wako yatari kwa lolote, hata kama ni kuua, kujeruhi, kutishia, na kudhalilisha utu wa binadamu ili mradi waendelee kutuibia, kutunyonya, na kutukandamiza. Kama ni kweli taarifa iliyotolewa na viongozi wa Chadema kuhusu yaliyojiri kwenye kambi ya Singida, sasa uvumilivu wa watanzania utakuwa umefika ukingoni. Nimetafakari mambo haya ambayo yananiumiza sana, kiasi cha kushawishika kujiunga humu ili tuelimishane.
- Hela zinazotumika kugharimia kambi hizo kufundisha majangili na majambazi, fedha zinazotolewa kama rushwa, fedha zinazotumika kununua tindikali, madawa ya kulevya, sindano (ili mradi tuu kuwakomoa Chadema)n.k ni za sisi walipa kodi. Yaani natoa kodi yangu af ndo inatumika kuniua, kunijeruhi na kunitishia usalama wangu endapo sitaipigia kura CCM!!!!!! Mungu wangu!!!!!!!!
- Eti, Mwigulu, Nape au Mukama, "Hawa vijana mliowafundisha ujambazi baada ya uchaguzi mnaendelea kuwapa mishahara kama askari au? Au ndo wanaachwa solemba mpaka uchaguzi mwingine uje tena.? Kama ni hivyo, hatuoni kuwa baada ya uchaguzi wanabadilika kuwa majambazi kabisa? Maana wameshafundishwa mbinu.
- Je mtanzania kuwa mtumishi wa serikali maana yake ni kuwa mpambe wa CCM hata pale ambapo mtu hataki? CCM ya leo bado inadhani tuko kwenye mfumo wa chama kimoja enzi za Nyerere na Mwinyi? Mnataka watanzania waamini kuwa mmejisahau au ni kiburi chenu cha kujifanya miungu watu? Mtu kuwa mwalimu, mfanyakazi wa benki, au nafasi nyingine yoyote ya serikali ni dhamanana ya CCM? Ni fadhila? Msipotujibu maswali haya hakika yenu your count down imekuja.
- Ombi langu kwa Chadema, tuko nyuma yenu ila mtuambie mbinu mbadala za kutatua matatizo yafuatayo, tuko tayari kuchangia hata kwa gharama yoyote.
- Pawepo na movement ya kuwafikia wananchi wa vijijini na kuwaelimisha haki zao za msingi. Mikutano ya hadhara ya siku moja kukusanya watu maelfu haitatosha. Tunahitaji tuwe na watu watakaosambaa vijijini wakae kwa muda huko wawaeleweshe raia ambao wanateseka na vitisho vya CCM.
- Tunahitaji social media ambayo itakuwa na coverage kubwa zaidi ya kuwafikia watanzania wote (TV na magazeti). Wadau wengi hapa JF wako tayari kusapoti