'Ukoloni wa Kifisadi' una athari kubwa kuliko ukoloni wa kigeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Ukoloni wa Kifisadi' una athari kubwa kuliko ukoloni wa kigeni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 18, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  [h=6]Unafikiri tunaweza kuelezea hali ya kisiasa nchini kuwa ni "ukoloni wa ufisadi"? Yaani tukitofautisha na kutawaliwa na wageni?[/h]Ukoloni wa ufisadi (colonialism of corruption) naweza kuelezea kuwa ni mfumo wa utawala ambao umekuwa imposed on the people na ambao watu hawakuuchagua wala kuukubali lakini unaonekana ukiendesha mifumo mbalimbali ya serikali na kuwanufaisha wachache. Ni mfumo ambao unaendesha karibu njia zote za maisha ya wananchi (kisheria, kiuchumi, na kijamii) huku ukitengeneza kati ya watu kundi la watu wachache wenye kunufaika na mfumo huo (mafisadi, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vya ufisadi) na mamilioni ya watu ambao wanajikuta wakiuhudumia mfumo huo (servicing the system) .

  Kama ukoloni wa kisiasa wa kigeni ambao ulikuwa imposed on the people na kuwanufaisha wananchi wachache wa ndani na wengi wa kigeni mfumo wa ukoloni wa kifisadi unaendelea kuwanufaisha wachache wa ndani na wengi wa kigeni. Mifumo yote miwili - ukoloni wa kisiasa na ukoloni wa kifisadi - msingi wake ni dhulma, unyonyaji, ukandamizaji na kutokujali matokeo (impunity)

  Kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni wa kisiasa mafanikio ya jamii kubwa ya watu wakati ule na ya mtu yeyote yule yalitegemea sana uhusiano wake na wakoloni. Wale waliokuwa karibu na wakoloni au waliopewa ajira na wakoloni walijikuta wananufaika na wengine kufikia mahali pa kujaribu kuutetea ukoloni na mafao yake kwao. Wale ambao hawakuwa na nafasi za kunufaika katika ukoloni walijikuta ni wahanga wa mfumo huo; hawakuwa na nafasi ya kubadilisha sheria, taratibu isipokuwa kulalamikia mfumo huo.

  Wapo kati yao ambao waliona njia bora ya kushughulikia mfumo wa ukoloni wa kisiasa ni kufanya nao mazungumzo ya kuona jinsi gani "wakoloni" wangeweza kuboresha hali ya maisha ya wananchi kwenye koloni. Hawa hawakuwa hasa na nia ya kuuondoa mfumo huo bali kuona jinsi gani wangeweza kustawisha maisha yao ndani ya mfumo huo. Leo hii hii chini ya utawala wa ukoloni wa ufisadi wapo ambao wananufaika na mfumo huu kiasi kwamba hawako tayari kuubomoa na kuumong'onyoa kabisa kwani ni kama kuukata mkono unaowalisha.

  Tofauti kubwa ni kwamba wakati wa kuukataa mfumo wa ukoloni wa kisiasa wananchi wetu walikuwa pamoja kwani walijua kabisa ni kwa pamoja tu wangeweza kuleta mabadiliko ya kweli. Leo hata hivyo tumegawanywa katika kuukataa mfumo wa ukoloni wa kifisadi. Nyerere alielezea vizuri kuwa wakati wa kupinga ukoloni TANU was the national movement ya kukataa mfumo ule na wananchi toka kila kona ya taifa letu walikuwa nyuma yake (Nyerere na TANU) kukataa ukoloni.

  Lakini wakoloni baada ya kuwakataa na kuung'oa mfumo wao waliondoka kurudi makwao; je mafisadi ambao ni wenzetu tunapowakataa na tukiwatoa wanaenda wapi? Na wale waliokuwa wananufaika na mfumo wao watakwenda wapi kama siyo kubakia in the background kusubiria zamu yao tena? Je, tunaweza vipi kuushinda mfumo huu tukiwa tumegawanyika, kugawanyika na kugawanyana? Je twawezi kweli kuungo'a ufisadi bila kujikuta kizazi fulani kinajenga chuki kama kizazi kilichonyang'anywa mirija wakati wa Mwalimu kilivyojenga chuki?
   
 2. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapi CCJ?
   
 3. l

  limited JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Lakini wakoloni baada ya kuwakataa na kuung'oa mfumo wao waliondoka kurudi makwao; je mafisadi ambao ni wenzetu tunapowakataa na tukiwatoa wanaenda wapi? Na wale waliokuwa wananufaika na mfumo wao watakwenda wapi kama siyo kubakia in the background kusubiria zamu yao tena? Je, tunaweza vipi kuushinda mfumo huu tukiwa tumegawanyika, kugawanyika na kugawanyana? Je twawezi kweli kuungo'a ufisadi bila kujikuta kizazi fulani kinajenga chuki kama kizazi kilichonyang'anywa mirija wakati wa Mwalimu kilivyojenga chuki?

  hapa itakuwa kasheshe kuwashinda hawa amabao wananufaika na ufisadi, wengi wanataka hali hii iendelee , kunahitajika uzalendo mkubwa sana na kuelimisha watanzania wengi sana nini hasa maana ya ufisadi, na sioni vyama siasa vya upinzani vikifanya hii kazi kwa kasi inayotakiwa. mafisadi wamepiga hatua mia mbele sie tuko ya kwanza
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Ukisikia kobe kainama....
   
 5. i

  ikhwan safaa Senior Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujue anaona aibu....lol
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Well put mzee mwanakijiji!, huu mfumo ni mbaya kwa sababu unaweza hatarisha amani kabisa, mfumo wa kifisadi umeenea kwa kasi kubwa hii Tanzania yetu toka utawala wa Mwinyi na ukabarikiwa na Mkapa. Wanachofanya wanatuibia wanagawana, wananunua wachache kuwaingiza katika mfumo huu na mtando wao, mtandao unavyokua wanaiba zaidi wanaongeza wafuasi kwa kuwaonjesha nguvu ya ufisadi na matunda ya ubepari hii inaongeza nguvu zao na utawala wa sheria na haki, uhuru wa habari, siasa za ushindani n.k vinaonekana ni adui wa mfumo huu inafika wakati wahusika wakuu wanakua hawana imani tena na kuachia madaraka kwa wengine nje ya mfumo huu na hapo watafanya kila wanaloweza, (ikiwa pamoja na kuua wapinzani) ili nguvu yao ya kisiasa na fedha walizochuma zibaki salama. ni hatari kweli kweli kwani kuwaondoa itataka mapinduzi ya kweli
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Ukoloni wa ufisadi unatishia uhuru wa wananchi zaidi kuliko ukoloni wa kigeni. Kwani katika ufisadi watu wanaaminishwa wako huru na wanacheza kama wako huru kumbe wako kama wanyama kwenye zoo! Wanakula, wanacheza, wanazaana na kuzalishana wakiamini kuwa wako huru.. kumbe kuna watu wananufaika na wao kuwepo hapo...
   
 8. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi nafanyia kazi kwanza hii thread yenye title "Kauli ya Kaburu Botha ni sahihi juu ya waafrika?" https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/182740-kauli-ya-kaburu-botha-ni-sahihi-juu-ya-waafrika.html  "By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulging in sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence

  And here is a creature that lacks foresight. There is a need for us to combat him in long term projections that he cannot suspect. The average Black does not plan his life beyond a year."

  Hypothesis nzuri kwa research yetu.

   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duuh, thread hii ya KABURU nimekua niiruka bila kuchungulia hata kidogo; mbona huyu baba ka-mnyambua sisi Wa-Afrika katika uhalisia wa madhaifu yanayotuangusha kila siku katika maisha hivi?

   
 10. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna bwana mmoja aliniambia wagombea wengi wa CCM (sijui kama ni wakoloni fisadi au vibaraka) walikuwa wanamwaga pesa kama Shetani katika kura za Maoni tu za CCM. Chukulia watu hawa walishinda ubunge. Miaka 5 itaisha bila kutokezea. Sasa 2015, majimbo yatakuwa na watu wengi zaidi, lakini tuchukulie wale wa Igunga 50,000 tu. Mwenye Billion moja akigawa sawia kila mtu atakula 20,000 tu kama malipo halisi ya miaka mitano ya Maendeleo. Hivi ndio vyanzo vya vilio vya DOWANS, UDA, na mengine mengi. Hivi wakibanwa kabisa kwenye wizi watapita wapi hawa? Kwa sababu hata kuchakachua kunahitaji pesa. Hivyo basi inawezekana kabisa kubadilisha mfumo kama waadilifu wengi watashika nafasi za kisiasa. Vitu kama miiko ya uongozi ni muhimu sana kwa nchi kama ya kwetu iliyokombolewa kwa nguvu za wakulima na wafanyakazi.

  Hata hivyo baada ya kusoma hotuba ya Millya akitumia jina la Nyerere kumshambulia Nnape, na kuangalia kipindi cha dakika 45 Mzee Sita pia akimtumia Nyerere pia kuwashambulia mafisadi, Nasema kazi bado kubwa sana. Kwa mawazo ya Millya ni kuwa Nyerere angekuwa hai leo angemnyanyua yeye Millya kama shujaa wa kupambana na ukoloni mamboleo, Na sio Nnape wala Sitta. Kazi kwelikweli.
   
 11. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ukoloni wa Kifisadi unaongozwa na Fisadi Papa Kikwete na Wenzake ni lazima tuuong'ewe
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  .kuna kila haja ya kubadilika sis wenyewe ndo tufanye mabadiliko ya nchi mana hadi sasa ni kama wananchi wenyewe hatujielewe na hatuelewi tunachofanyiwa.
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Afadhali Makaburu kulika mafisadi.
   
Loading...