Uko wapi Dk Wilbroad Slaa? Njoo ushuhudie anguko la Mafisadi

Uko wapi Dk Wilbroad Slaa? Njoo ushuhudie anguko la Mafisadi

Chozi la Dr silaa haliwezi kudunda chini bure..only God knows..mi nilichawachinja mapema hao wapinzani uchwara..na uzuri nikajipatia wawili hapo hapo kituoni baada ya kuonekana hawajajua wampigie nani..nilivyoingizia ishu ya pombe kukesha kwenye madaraja usiku bila kuagizia watu wa chini yake nikajikuta nimekamata vichwa viwili fasta.
 
dr slaa ndio tumani pekee lililokuwa limebaki



Wanafiki wakubwa nie. Mbona 2010 muli mkataa kuwa rais. Mwaka huu ni Lowassa. Acheni unafiki wakuonyesha kama mna mpenda sana Slaa, nie ccm niwaongo wakubwa.
 
Kwa upepo ulivyo kwenye vituo ccm imeshaangukia pua..... vijana ndo wapiga kura leo na asilimia kubwa wana mabadiliko!!!

Na magoli ya mikono inanaswa vizuri kweli... kingine kibaya ni kuwa mawakala wengi wa fisiem ni wana cdm damudamu...

Imekula kwenu !!!!
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza,Kuna sehemu mafisiem walitaka wapigishe kura wanafunzi makamanda wakashtuka wakadakwa.Bao la mkono linakula kwao.
 
Gia ya angani leo inazimiwa ardhini kwa kura ....Bring back our Dr Slaa ....

Hujuma mnazofanya hazitafanikiwa kamwe tumedhibiti maeneo yote tata mliyojipanga kuiba na kuzuia ngome ya Mnyika Temboni stop over na Kimara. Zaidi ya watu elfu 12 hawajapiga kura tangu asubuhi lakini tumewabana na kesho watapiga kura mtashindwa vibaya
 
Hujuma mnazofanya hazitafanikiwa kamwe tumedhibiti maeneo yote tata mliyojipanga kuiba na kuzuia ngome ya Mnyika Temboni stop over na Kimara. Zaidi ya watu elfu 12 hawajapiga kura tangu asubuhi lakini tumewabana na kesho watapiga kura mtashindwa vibaya
Hujuma zipi! Hivi umemsikiliza vizuri alicho sema Mkurugenzi wa NEC?
 
Hujuma zipi! Hivi umemsikiliza vizuri alicho sema Mkurugenzi wa NEC?

Tuambie amesemaji wewe uliyemsikiliza, ulikuwepo Temboni bwaloni wakati msimamizi wa uchaguzi anakula kichapo baada ya kuficha daftari la wapiga kura alichokisema?
 
Wana ukawa wapo bize wanafanya mapinduzi kwenye sanduku la mpiga kura hawana time na propaganda zenu

No such a thing, wengi hamkujua kuwa lowassa alikuwa akitengeneza mafuriko ya kiini macho. lakini kwa ccm ni ushindi wa kishindo. lowassa alijaribu kutengeneza mafuriko tangu akiwa ccm na hata mpaka chadema, lakini kwenye masanduku ya kura hakuna mafuriko ya kutengenezwa
 
Unahisi kutekenywa kila utajapo chadema sio....nimeangalia mada zako zote humu ni kama upo na kazi maalum...kama mwanaume kamili weka id yako na sura yako kama wengine, unapojificha unaonekana kama wengine tu waropokaji...anxa na hilo kututhibitishia u'v got balls other wise dont waste othr people precious time.
 
Mzimu wa slaa na zitto utawatafuna wote waliohusika viva magufuli...
 
Mtandao Hatari wa JF waanza kupingana na Matamko ya serikali na kuacha members wake wakipost Matokeo ya uongo na Baadhi kutangaza washindi katika baadhi ya matokeo kinyume cha sheria.

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.

Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-

16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana. uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha usahihi wa matokeo yote yanayotangazwa.

16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.

Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 25/10/2015

Source: MICHUZI BLOG: KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU

Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhani sasa hivi akiongea live na ITV amesema kwamba Matokeo rasmi ya uchaguzi wa leo hayajatolewa kabisa infact hakuna hata kituo kimoja ambacho kimeshatoa matokeo, anasema kwamba ni Tume yake tu yenye mamlaka kisheria kutoa matokeo ya uchgauzi na wao hawajafanya hivyo bado, kwa hiyo matokeo yote yanayorushwa kwenye mitandao sasa hivi ni ya uongo na ni kinyume kabisa na Sheria.
 
Dr Slaa asingeweza kupambana na magufuli, Lowassa anamkimbiza vibaya gufuli.
 
Kwa matokeo yanayo endelea kutoka Edo ni Rais.

Kura yangu ipo salama [ mnvi= √]
 
[Unakosea sana ndugu, Slaa kaondoka mwenyewe kwa ulafi wa madaraka, Lowassa mnayemtuhumu fisadi mmeshindwa kuthibitisha ufisadi wake hivi " shut up"
 
Back
Top Bottom