KINGA'asti,
Mtoto wangu wa "ujanani" amezaliwa 1997...! Yupo hapa Bunju ninavyoandika hii post...! 1988 nilikuwa naangaika kutafuta elimu mkoani Kilimanjaro na sikuwa shabiki wa "soft centre" by then..!
Familia ya "Rugangila" ni majirani zangu...!
KINGA'asti,
Mtoto wangu wa "ujanani" amezaliwa 1997...! Yupo hapa Bunju ninavyoandika hii post...! 1988 nilikuwa naangaika kutafuta elimu mkoani Kilimanjaro na sikuwa shabiki wa "soft centre" by then..!
Familia ya "Rugangila" ni majirani zangu...!
I second you MtamaMchungu..kweli mwiba uliopo mguuni pa mwenzio haujui maumivu yake.
Mimi nimeishi na ndugu ambaye baba yake alimkataa kabisaaa. Akasoma akamaliza shule akawa daktari. Ndipo akaanza kumtafuta baba yake. Good for him baba yake alikubali kumuomba msamaha na sasa hivi wako vizuri JAPO hata mama yake alikataa kumsaidia kumweleza ukweli.
Guess what baba yake naye ni daktari.
Kuna something about identity ya mtu anaijua anapowafahamu wazazi wake. Si vizuri kwa mama (pamoja na kumshukuru kwa kumlea...which was her responsibility btw..so dont make a big deal out of it) kumficha mtoto ukweli juu ya baba yake. HATA akienda na bado akakataliwa ni better kuliko kuishi maisha yote bila kujua what really hapenned to mzazi wake mmoja.
Umri wa huyu binti sasa (25yrs) ni umri wa kuanza mahusiano. Huwezi kuwa na mahusiano mazuri kama ww mwenyewe nafsi yako haijatulia about ur identity.
I think ninamuelewa.
My dear endelea kumtafuta baba yako ujue kama kweli alikufa kwenye ajali ya mv bukoba au vipi.
I think chukua ushauri wa kuwatafuta marafiki wa mama yako. Au mahali ambapo baba alifanya kazi mara ya mwisho kabla ya kupotea.
Usikate tamaa....
Kujitambua hakuji kwa kuangalia nje. Bali kwa kuangalia ndani.
Kuna human elements za kujisikia incomplete hapa, ambazo ni the opposite of kujitambua.
Baba ambaye hana habari na mtoto hana haki ya kujua habari za mtoto.
For all we know kakaa raha mustarehe na mke na watoto wake. Kwa nini kumpelekea unwanted dramatic intrusions into his life kama mwenyewe hataki kumtafuta mtoto?
I could easily see the stepma drama, the precarious position the father will be in, all the hazards of a mixed family in our settings.
I only raise these points, brutal as they may seem, because they are very pertinent.
Kuna tofauti kati ya aliyepoteza mzazi na asiyemjua kabisa. Wa kwanza anaelewa fate ya wazazi wake, either walikufa au hata kama walimkataa, at least anelewa the state of their "relationship" be it bad or good. Sasa mtu asiye jua chochote kuhusu mzazi wake anakuwa na maswali yasiyoisha hata siku moja, alikufa??, yupo hai??, yupo wapi??
Huwezi kujua maumivu ya mwiba kwenye mguu wa mwenzako.
Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!
Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!
You sound like a pessimist to me--on account of your overlooking one extremely important human quality: the ability to forgive.
Inawezekana kabisa mtoto alikuwa accidental conception, which might complicate the picture a little bit. Lakini kama haikuwa accidental, ambayo ndiyo assumption tunayokwenda nayo hapa, sioni ubaya mtoto kumjua baba yake.
Sijakusoma vizuri unaposema "Kujitambua hakuji kwa kuangalia nje. Bali kwa kuangalia ndani." Ni kujitambua gani huko ambako ni selective ya mahali pa kujitambua. Najua kiswahili chetu kina madhaifu mengi katika kuelezea fikra complex. Hili la kujitambua halina complexity yoyote hapa, kwani sioni ugumu unakujaje katika kukubali mtu anao utu wa ndani, ambao hatimaye unazaa utu wa nje, lakini pia kwamba katika sura hizi za utu wa mtu, yapo ambayo yamepatikana katika shule za aina mbalimbali, na yale ambayo ni kurithi.
Maana yangu ilikuwa kwamba mtoto hajafanya kosa kutaka kumjua baba yake kupata justification ya mambo ya kurithi. Hii ni jitihada ya kujitambua.
Nimeongelea habari ya pessimism. Unaelekea kudhani mtoto akifanikiwa kumpata baba yake jambo hili litaleta shida. Now that assumes huko aliko hakuna watu wenye huruma, hakuna watu wenye uwezo wa kusamehe. That is very pessimistic. Akipokelewa utasemaje? Kwa sababu hilo linawezekana pia.... Kuna wanawake kibao wakimpenda Mume wapo tayari kumbeba kama kesha likiwana matakataka yake yote kwa kusamehe vurugu za ujana.
Mi naona jitihada ya kumtafuta huyu baba mpotevu iendelee.
Forgiveness is for those who ask for it.
Hata wanaoamini dini kuna kutubu kwanza na kumuomba mungu msamaha, then unasamehewa.
Sasa kwa nini huyu baba asamehewe na kupewa nafasi ya kumuona mwanawe hata kabla ya kumtafuta na kumuomba msamaha?
The whole thing is spanning from a sense of incompleness. Mtu anajisikia hajakamilika mpaka amjue baba yake. Kujitambua kutatokanaje na kumtafuta baba asiyekutafuta? This is losing focus in the quest for kujitambua.
This so called father is a stranger in all senses but biological. Hujitambui kwa kukumbatia strangers. Don't confuse a craving for what is not there, a real father, for a quest for kujitambua. Mtu anayetafuta kujitambua angejenga identity around kutokuwa na a biological father . This is the reality. Kujitambua ni kutambua reality. Sio kuota ndoto kwamba unaweza kujenga uhusiano wa maana na baba ambaye hana habari nawe kwa miaka 20.
Unaangalia upande wa mtoto. Tuangalie upande wa baba. Does the father deserve to know the offspring?
Kuna kanuni moja ya maisha mnataka kuvunja hapa.
Usiende kule ambako hujaalikwa na watu hawataki uende.
Kama baba angetaka mtoto amtafute angeonyesha hilo.
Hakuonyesha. Heshimuni matakwa yake.
Kiranga, nikiri hapa kwamba Ni kweli nipo upande wa huyu mtoto. Ila katika hoja zako tatizo ninaloliona ni kwamba
wewe unanielekeza kwenye kesi hapa; na mimi sikutaka kujihangaisha na kesi.
Chukua scenario hii: umesafiri kuto Dar hadi Kigoma katika treni ya reli ya kati. Upo Daraja la Tatu mnakokaa watu sita kuzunguka meza. Watatu kila upande mnatazamana. Wewe kiranga ni mwanamume wa ule umri mbaya wa foolish age.
Mbela yako kuna Msichana ana sura nzuri sana unatazamana njia nzima kutoka Dar hadi Kigoma. Yeye pia yupo Foolish age. Unaujua ule umri 18 - 25. Inatokea bahati mbaya treni imechelewa kufika Kigoma. Tufanye imefika saa 12 jioni na kila mmoja wenu ana safari ya ziada kuelekea Kasulu na Kibondo.
Kutokana na kufahamiana sana katika safari na kutamaniana, mnachagua kuendelea kuonana, na mnajikuta mnapata Chumba cha wageni kimoja Mwanga Guest House ambacho kina kitanda kimoja tu. Hii hadithi ni Riwaya tu yenye lengo la kukusaidia kuona upande wa pili. Majina yote ni ya kutunga.
Kinachotokea katika kile chumba usiku mzima siwezi kusimulia. Mtoto wa kiume katoa jina lake na anuani ya Dar. Binti katoa jina la uongo na maelezo ya uongo anaenda chuo cha ualimu kasulu kwa sababu ana mchumba au mume kabisa mahali. Itokee yule kijana alikuwa lijali vibaya sana mimba ilitunga usiku ule na yule binti kutokana na kumpenda sana yule kijana alichagua kutunza ile mimba ili hali akijua si ya mchumba wake au pengine mume. Wenyewe wanaita kuchanganya.
Zinapita siku yule mchumba au mume anastuka mimba si ya kwake. Na yule binti anataka ulimwengu uendelee kujua ile mimba ni ya mume yule kulinda mstakabali wa heshima katika ukoo, kanisa au jamii yoyote kwani dunia nzima inaelekeza mwanamke asizae nje ya ndoa. Mtoto anakuja kutambua mama alizaa na mtu ambaye haishi naye.
Kosa nipo kwa mama hapo. Lakini inasaidia nini kumlaumu mama. Atarudisha mimba tumboni? na kuitoa? No....
Tungekuwa na uwezo wa kuongea na mama wa huyu binti na tukajiridhisha kuwa atatuelewa, tungemshauri amwambie mwanae huyu ukweli wote bila kuficha na wasaidiane kumtafuta baba. Mtoto huyu ana haja na haki vinavyokubalika kumjua baba yake ni nani hasa.
Kama kuna tatizo hapa ni mama yake.
Mfano wako mbovu kwani ni hadithi iliyo tofauti na kisa hiki.
Katika kisa hiki baba anamjua mama na anajua kuna mtoto. Lakini hakumtafuta mwanawe yeye mwenyewe wala kwa proxy.
Kama unataka tuendelee kujadili kisa hiki tuendelee kujadili habari tulizoletewa. Sio kutunga hadithi zisizokuwepo kwenye habari hii.
Kama unataka kujadili hadithi tofauti anzisha thread.
pamoja na yoooote binti nakutakia kumtafuta kwema baba yako..... Hilo janga unalolitafuta likupe fanaka........ Mama yako kakulea kwa shida na raha bafo unasema haupo ćomplete´ huyo baba alokutelejeza atakucomplite nini????
Don't get emotional Kiranga. Hadithi yangu inao uhusiano na kisa hiki kwa tafakuri ya mahusiano yaliyokuwapo kati ya baba na mama wa mtoto huyu. Kwa kutafakari tu huoni kuna uwezekano mmoja wapo kati ya wazazi hawa anaweza kuwa anahisi mtoto si wa kwake? Mi ninavyoona dilema ya huyu mtoto ni kwamba mtu anayetajwa kuwa baba yake anaweza akawa siye, na hiyo ndiyo mantiki haswaa ya hadithi yangu. Tatizo la huyu mtoto ni mama yake si baba yake.
Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!
Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!
Mimi sioni ubaya wowote ule kwa mtoto kutaka kumjua na kumuona baba yake.
Pengine mtoto ana kiu ya walau kutaka kujua huyo baba yake anafananaje.
Huenda mtoto labda ana maswali ya kumuuliza huyo baba yake.
Hata ingekuwa mimi ningekuwa najiuliza maswali mengi sana kama ningekua bila kumjua baba yangu.
Na kama asingekuwepo kabisa kwenye maisha yangu basi ningependa kujua kwa nini ilikuwa hivyo na ningependa kusikia toka kwake yeye mwenyewe.
Kati yangu ninayeheshimu the cold fact kwamba baba hajataka contact na wewe unayeendekeza ndoto za a deadbeat dad kum complete mtoto nani emotional hapa?
Hadithi yako hsihusiani vilivyo na kisa hiki kea sababu baba wa kisa hiki anajua kuna mtoto.