Uko wapi baba?

Uko wapi baba?

With all due respect, mwiba uliopo mguuni kwa mwenzio huwezi kujua maumivu yake. Tatizo sio baba peke yake, kuna swala la identity hapa na kama ni mtoto wa kiume ni ngumu sana kuishi bila kujua your roots.

Inawezekana suluhisho ni ku move on. Mbona watu wanafiwa na wazazi wakiwa wadogo na wanastawi vizuri tu?

Kwa nini mtu awe tegemezi kwa baba ambaye hakumjali?

Identity yoyote utakayotafuta bila kujali values za uwajibikaji itakuwa haifai kwa hilo. Na huyu baba hajawajibika.

Halafu kwa nini mumuingilie maisha yake kama yeye hataki kumtafuta mwanawe?

Akimkataa si mtapata heartbreak zaidi?

Kama mtoto kaweza kuishi miaka 20 aendelee kivyake tu. Obviously baba hana time naye. Angekuwa na time naye angemtafuta.

Sasa kwa nini kuji impose kwa mtu hana time na wewe?
 
pole sana ndugu, jaribu pia kugoogle hilo jina uone utapata details gani ufananishe na maelezo ya mama yako
 
Inawezekana baba yako ni mwana JF, endelea kuingia humu mara kwa mara kuna siku mtaungana. Kila la kheri!
 
Inawezekana suluhisho ni ku move on. Mbona watu wanafiwa na wazazi wakiwa wadogo na wanastawi vizuri tu?

Kwa nini mtu awe tegemezi kwa baba ambaye hakumjali?

Identity yoyote utakayotafuta bila kujali values za uwajibikaji itakuwa haifai kwa hilo. Na huyu baba hajawajibika.

Halafu kwa nini mumuingilie maisha yake kama yeye hataki kumtafuta mwanawe?

Akimkataa si mtapata heartbreak zaidi?

Kama mtoto kaweza kuishi miaka 20 aendelee kivyake tu. Obviously baba hana time naye. Angekuwa na time naye angemtafuta.

Sasa kwa nini kuji impose kwa mtu hana time na wewe?

Waswahil husema usilolijua daima litakusumbua,na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake!
Haijalish matokeo baada ya kuonana na babake yakuaje km kwel yupo kuna umuhm wa kumfahamu kuepusha mambo km kuoa au kuolewa na ndgze.
Pia unawezaje kujiridhisha kwa kusikia story ya upande m1?ni waz haijakamilika ht km ni ukwel tupu.
Nafsi isiyorizika daima itasumbuka had kaburin muachen amjue baba ake ht km nikuona kabur lake nafs yake itarizka na kutulia,
hawez kujiweka ktt kund la waliopata kila ki2 maisha ili hal hajapata kumjua babaye mzaz!ni ngumu kumeza jaman!
 
pole kijana.baba yetu na yeye aliwahi kuzaa nje,mtoto alipokuwa alimuuliza baba yake yuko wapi,akaeleweshwa,akamtafuta mpaka akampata.na sisi tukafahamamishwa kuhusu ndugu yetu.nafiki kama mtoto bila ya kumuona mzazi mmoja wapo mfano kama unasoma,na watoto wenzako wanaelezea baba amenifanyia hivi au mama,deep down,huyo mtoto anakuwa na unyonge fulani,sikulaumu kijana ila be careful utakapoonana nae,maana anaweza akaku let down zaidi au ikawa furaha kwako
 
Waswahil husema usilolijua daima litakusumbua,na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake!
Haijalish matokeo baada ya kuonana na babake yakuaje km kwel yupo kuna umuhm wa kumfahamu kuepusha mambo km kuoa au kuolewa na ndgze.
Pia unawezaje kujiridhisha kwa kusikia story ya upande m1?ni waz haijakamilika ht km ni ukwel tupu.
Nafsi isiyorizika daima itasumbuka had kaburin muachen amjue baba ake ht km nikuona kabur lake nafs yake itarizka na kutulia,
hawez kujiweka ktt kund la waliopata kila ki2 maisha ili hal hajapata kumjua babaye mzaz!ni ngumu kumeza jaman!

Mimi ninayeheshimu privacy ya mtu nitaona baba hataki ijulikane na anataka kifanya siri.

Vinginevyo angetafuta mtoto wake.

Kama mtu unampenda baba yako, hata kama humjui, unafanya matakwa yake. Unabaki kivyako.

Vinginevyo utamtia doa kwamba alizaa nje ambalo kwake ni wazi halitaki. Aanze kazi ku explain kwa mke, kanisani, kwenye jamii etc. Mama wa kambo aanzishe beef. Ya nini awkward complications zote hizo?
 
HAbari wana Jamvi. Hope your weekend is great kama ambavyo yangu pia ingekuwa kama Hili lingetimia. Mniwie radhi kama hapa si mahala pake as nimeona pananifaa zaidi kuwasilisha hili niweze pata walau msaada toka kwenu.

Namtamtafuta Baba yangu Enock Rugangira niliyempoteza since nikiwa na umri wa kutoweza hata kumtambua (6 month)

Here is my Short Life Story
Naishi na mama pamoja na wadogo zangu wawili, Mmoja wa kike na wa mwisho wa Kiume. Nilizaliwa mwaka 1988 mkoani Arusha na mamayangu Marry Pascal Kundi wakiwa wakiishi na ambaye ni baba yangu mkoani Arusha, wakati huo Baba akiwa mfanyabiashara wa madini. Kwa maelezo ya mama yangu, Nilipofikisha umri wa miezi 6 baba yangu alitoweka akiwa katika mizunguko ya kibiashara. Mbaya zaidi tangu nilipojitambua nimekuwa nikikosa ushirikiano kwa mama yangu kila ninapotaka kujua kuhusu alipo baba yangu, jambo linaloashiria mazingira waliyopotezana naye hayakuwa mazuri kwa maana ya namna flani ya ugomvi. Majibu ninayoyapata mara nyingi toka kwake ni simply "baba yako amekufa kwenye ajali ya MV Bukoba" with no any narration jambo linalonipa mashaka kuwa ni majibu ya kunipotezea nisifuatilie zaidi kumhusu baba yangu.

Now am grown up na namhitaji Baba yangu kuliko kitu chochote, walau kumuona then i think my Life will be complete.
I know JF is wide and i believe somehow somewhere this can help.

Kwa yeyote baina yenu wana jamvi aliye walau na clue ya Hili jina "Enock Rugangira" anifunulie hili tafadhali.



Awali ya yote unapaswa kum respect sana mama yako kwakua kiukweli kina mama wana siri nyingi na huwa wanauvaa umama na kusimama upande wa watoto wao licha ya kua wapo baadhi wana matukio yakutelekeza watoto wao.Mazingira yanaonesha wazi bila ya msimamo wa mama yako pengine usingekuwepo.
HIKI NI KISA CHA KWELI KINACHOFANANA NA CHAKO.
Yuko kaka mmoja wakati anafanya tukio hilo alikua na umri wa miaka 27.Yeye alimpa ujauzito dada mmoja jirani yetu lakini kutokana na kukengeuka aliamua kukana mimba mbele ya vikao vilivyoitishwa na wazazi wa msichana kwani msichana alimtaja yeye na si hivyo tu mahusiano haya yalikua bayana.Lakini licha ya kaka hayu kukana kwenye vikao kwamba hakua na mahusiano na huyu dada alie muita malaya tena hafanani nae,alikua akimtafuta dada hayu nje pembeni na kumwambia yeye hana tena time na yeye hivyo alimpatia pesa ili aitoe mimba ile lakini dada yule alikataa jambo la kutoa mimba.Kaka huyu aliitwa vikaoni kwakubembelezwa zaidi ya mara tatu ila baada yakutoa msimamo wake kikao cha kwanza kilichoendelea ni matusi na maneno ya kashfa kwa dada yule na kwa wazazi wake .Mungu si Athumani dada mjamzito alijifungua salama lakini mtoto aliezaliwa na baba yake ni kama kajipiga picha mwenyewe yani amefanana sana na yule kaka ila msimamo wake ulikua ni uleule kwamba yeye hawezi kuzaa na malaya.Baada ya miaka michache kaka yule alitangaza ndoa na binti fulani hivyo maandalizi ya harusi yalifanyika.Lakini habari hizi kwakua zilikua wazi kaka huyu kabla ya ndoa aliitwa na jopo la wachungaji kikaoni wakimsihi kwamba kama yule ni mtoto wake anapaswa kumridhia na amchukue lakini alikana pia mbele ya wachungaji na hakukua na jinsi tena kwani aligoma kabisa.Basi maandalizi ya harusi yake yalikamilika na mwisho wa siku alioa.
MIUJIZA ILIODUMU HATA HIVI LEO.
Huu ni zaidi ya mwaka wa kumi sasa kaka huyu hapati mtoto,amemaliza mahospitali,mitishamba na Wachungaji kwa maombezi lakini mke wake mimba zimekua zikitoka zikiwa changa kabisa,inasemekana amefika hatua anajaribu kutoka nje ya ndoa akihisi tatizo ni mke bila ya mafanikio yoyote,binafsi huwa anazani amerogwa ila ukweli utabaki palepale Mungu hua anamiujiza yake.Miaka michache iliopita ilimbidi sasa atafute wazee ili sasa afuatile mtoto ambae alishamkana tena kwakubembelezwa sana.Wazee wamegoma kwani hawajui pakuanzia kwakua wanafahamu kisa chote.Wazazi kaka huyu nao ni ngumu kufanya lolote kwani walikua upande wa mwanao hapo awali.
MSIMAMO WA DADA MWENYE MTOTO.
Amegoma kumtoa mtoto kwani kwanza hana imani tena juu ya usalama wa mtoto yule kwani kama baba yake alikua tayari kuitoa mimba yake ni dhahiri kabisa leo anamuhitaji kisa tu amekosa mtoto,swali ni kwamba ni nini usalama wa mtoto huyu kama itatokea kaka huyu mke wake amebahatika kupata mtoto?kwakua ni dhahiri baba huyu hampendi mtoto yule ila anamuhitaji kwakua hana mtoto.Kiuhalisia ni kweli lolote linaweza tokea kama mke wa kaka huyu atabahatika kupata mtoto.Familia ya dada mwenye mtoto wapo tayari kumsomesha mtoto hata atakapo kua na umri wakujitambua labda elimu ya chuo,watamueleza mtoto juu ya muendeno mzima kuhusu maisha yake na uhalisia juu ya baba yake na alichokifanya kwake kisha anaweza kuwa na maamuzi aelekee wapi kwani mtoto akishakua huwezi kutumia mabavu kumzuia na lazma atahoji juu ya baba yake kama unavyo fanya wewe sasa.
Kimsingi hii ndio hofu ya yule kaka kwani alipostuka alitaka kumchukua mapema yule mtoto kabla hajakua kwani akikua akafahamu alichofanyiwa na baba yake kaka yule atakua na mazingira magumu kwa mtoto wake na huenda mtoto hata akamkataa kabisa.
Hivyo muheshem sana mama yako kwani kina mama upendo wao kwa watoto wao hakuna wakufanana nao.
Na inawezekana unamtafuta baba mnyama kama huyu ndio maana mama yako amekua akikuficha ili usije enda kwake.
Naamini kwa kisa hiki utakua umejifunza kitu.
asahnte!
 
anamtafuta baba yake ili awe complete katika maisha loh! Mshukuru Mungu pamoja na mama yako aliekulea hadi umekuwa unaanza kucomplain kuhusu baba yako, angejua maana ya kulea asingekimbia.
 
Hata ukishauriwa huwezi kuelewa -
ila kweli kama huyo baba yuko hai, anajua alkuacha na mama yako na hajakutafuta piga magoti kwa Mungu umshukuru mama kwa kukulea na umwombee azidi kuwa na afya njema
Utaumia sana utakapompata halafu ugundue kwamba hakuhitaji
 
Inawezekana suluhisho ni ku move on. Mbona watu wanafiwa na wazazi wakiwa wadogo na wanastawi vizuri tu?

Kwa nini mtu awe tegemezi kwa baba ambaye hakumjali?


Identity yoyote utakayotafuta bila kujali values za uwajibikaji itakuwa haifai kwa hilo. Na huyu baba hajawajibika.

Halafu kwa nini mumuingilie maisha yake kama yeye hataki kumtafuta mwanawe?

Akimkataa si mtapata heartbreak zaidi?

Kama mtoto kaweza kuishi miaka 20 aendelee kivyake tu. Obviously baba hana time naye. Angekuwa na time naye angemtafuta.

Sasa kwa nini kuji impose kwa mtu hana time na wewe?

Kuna tofauti kati ya aliyepoteza mzazi na asiyemjua kabisa. Wa kwanza anaelewa fate ya wazazi wake, either walikufa au hata kama walimkataa, at least anelewa the state of their "relationship" be it bad or good. Sasa mtu asiye jua chochote kuhusu mzazi wake anakuwa na maswali yasiyoisha hata siku moja, alikufa??, yupo hai??, yupo wapi??

Huwezi kujua maumivu ya mwiba kwenye mguu wa mwenzako.
 
Maneno yako ni kweli na hakika,ila hayatoi sababu ya msingi haswa kwa nini huyu ndugu asitamani kumjua japo kwa kumuona huyo baba yake.
Pia katika habari hii hatujajua bado chanzo cha kutengana baina ya wanandoa, chanzo cha matengano kimekua ni cha kusadikika na habari haiweki wazi sana kuwa Baba alikimbia au alifukuzwa(hili lawezekana).
Pia kuna mahali habari inabainisha kuwa, "Baba alitoweka katika mizunguko ya kibiashara". Hii inaweza kumtokea mtu yoyote, hii haitoi maana kuwa baba mtu alitoroka.
Hivyo basi mwacheni mwanakwetu aendelee kumsaka baba yake, kwani "Jini likujualo, halikuli ukakwisha".

Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!

Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!
 
Mimi ni victim wa hii kitu, usiombe ukutane na watu wa hivi.....mara amesusa, mara anashitaki ohh humjali, humheshimu.,,,duhh yani ni majanga! I even regret why nilikutana nae....

pole sana dear. Mie naogopa strangers. I dont wanna mess up my life. Na most of the time huwa wanataka kupata emotional attention ili wao ndo waonekane victims kuziba makosa yao. Kama hukunitaka wakati ule, unanitaka wa nini sasa? Kama nimetoboa hadi sasa, nakutaka wa kazi gani?

Kuna mama mtu mzima, rafiki yangu. Alioana na mwanaume aliekimbiwa na mke akaachiwa watoto 3. Kijana mmojawapo wakati anaoa akaanza ooh namsaka mamangu. Baba akamuelekeza akaenda songea. Yaani mama alimfuata gesti, akamuambia sikuwataka wakati ule na siwataki sasa. Alfajiri naomba uondoke na usinitafute teeena hata ukisikia nimekufa usijeeee! Mume wangu hajui kama nilishawahi kuzaa, usiniletee balaa. Kwani huyo mama aliewalea si ndo mamako, nendeni nae mkalipe mahari mie siwataki na uwaambie na ndugu zako.
Kaka alirudi mdogo kama piriton!
 

Namtamtafuta Baba yangu Enock Rugangira niliyempoteza since nikiwa na umri wa kutoweza hata kumtambua

Hii familia ya "Rugangila" note: siyo "ra" ni "la" ina historia fulani katika nchi ambayo Mwl. Nyerere hakupendezwa nayo! "Enock Rugangila" alishantangulia mbele ya haki siku nyingi sana...!(RIP), na wala hakuwa kwenye ajali ya Mv Bukoba.

Naomba uendelee na maisha yako na mama yako na nduguzo na mshukuru Mungu kuwa umeweza kufika hapo ulipo...!

Ameni
 
Ndo maana nikasema baba nikikutana nae kwa bahati mbaya, atahitaji kunishawishi kwa nini hatujakutana toka muda huo.
Kuna watu wanazuiwa kuwaona watoto wao. Wanaitisha vikao, wanaenda kwa wazee, wanaenda ustawi wa jamii. THEY FIGHT kuwa sehemu ya maisha ya watoto wao!

Rafiki yangu aliondoka kwenye abusive marriage akapokonywa watoto. Alijua mume ni hopeless. Japo walishajenga ghorofa. Lakini bi dada alienda kuona wanae shuleni kwa siri, na kuwalipia ada kwenye account ya shule ili wanae wasome. Alimpa wifi mtu hela na nguo za wanae. Na simu ili atumiwe picha. Tulienda wote ustawi wa jamii, KUPAMBANA! Na iliposhindikana, baada ya kuongea na watoto na kugundua baba anaingiza mwanamke mpya kila siku ba kuwatukana matusi na kuwapiga (hao wanawake), mpango umesukwa wa KUWAIBA watoto. This is a fighting parent, hata akikuambia nilifanya moja mbili tatu utamuelewa.

Ila huyo baba ambae hadi nazeeka hajaweza kuniandikia hata barua kwa boski la barua la shule! Hata walioko jela wanaandika barua uraiani. Sitamtafuta aisee, im better off without him! Kha!
Maneno yako ni kweli na hakika,ila hayatoi sababu ya msingi haswa kwa nini huyu ndugu asitamani kumjua japo kwa kumuona huyo baba yake.
Pia katika habari hii hatujajua bado chanzo cha kutengana baina ya wanandoa, chanzo cha matengano kimekua ni cha kusadikika na habari haiweki wazi sana kuwa Baba alikimbia au alifukuzwa(hili lawezekana).
Pia kuna mahali habari inabainisha kuwa, "Baba alitoweka katika mizunguko ya kibiashara". Hii inaweza kumtokea mtu yoyote, hii haitoi maana kuwa baba mtu alitoroka.
Hivyo basi mwacheni mwanakwetu aendelee kumsaka baba yake, kwani "Jini likujualo, halikuli ukakwisha".
 
Au ni wewe nini mkuu? Jitokeze bwana

kama uko serious, yatafuata masuala ya baba mdogo na bibi zake wako wapi! Its gonna be complicated. I assure you!!
Hii familia ya "Rugangila" note: siyo "ra" ni "la" ina historia fulani katika nchi ambayo Mwl. Nyerere hakupendezwa nayo! "Enock Rugangila" alishantangulia mbele ya haki siku nyingi sana...!(RIP), na wala hakuwa kwenye ajali ya Mv Bukoba.

Naomba uendelee na maisha yako na mama yako na nduguzo na mshukuru Mungu kuwa umeweza kufika hapo ulipo...!

Ameni
 
Au ni wewe nini mkuu? Jitokeze bwana

kama uko serious, yatafuata masuala ya baba mdogo na bibi zake wako wapi! Its gonna be complicated. I assure you!!
KINGA'asti,

Mtoto wangu wa "ujanani" amezaliwa 1997...! Yupo hapa Bunju ninavyoandika hii post...! 1988 nilikuwa naangaika kutafuta elimu mkoani Kilimanjaro na sikuwa shabiki wa "soft centre" by then..!

Familia ya "Rugangila" ni majirani zangu...!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom