Ukiwa shabiki wa Diamond raha sana

IKIRIRI

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
2,734
3,017
Yani kuna muda binadamu unahitaji refreshments. Kama ni kweli ni mpenda burudani kama unamshabikia Diamond raha sana, jamaa ana vibe kali.

Ipo sehemu tu katika mambo yake itakunogea na kukuvutia. Naangalia Wasafi TV live mapokezi anayopewa sitaki kuamini kama watu hawa wamenunuliwa; mji umesimama.

Wasanii wengine ukiwashabikia ni kama unashabikia Arsenal. Msanii full kuringa hakupi mtazamo chanya wa kupambana na shida.

Kiukweli Diamond ni mtaalamu wa burudani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasanii wengine ukiwashabikia ni km unashabikia Arsenal, msanii full kuringa hakupi mtazamo chanya wa kupambana na shida.
Kushabikia msanii inatokana na raha anayokupa moyoni kwako. Na kama mshabiki yeyote kuna wakati wa raha na wakati ambao unaweza kuhitaji faraja. Kama unamshabikia mringaji ni sawa tu, kama unamshabikia mondi ni sawa tu. Kumshabikia mmoja haina maana wengine hawafai.
 
mbona kama unapangia wengine cha kufanya mkuu!!

mond ni msanii mzuri sawa,ila sio kwamba atakuna kila mtu.
 
Naangalia hapa wasafi tv kwenye ile safari yake ya kwenda kigoma na treni kila baada ya mkoa anapata mapokezi makubwa sana alafu jamaa aringi anasimisha treni anaongea na raia utazani ni Raisi wa nchi.
 
Yani kuna muda binadamu unahitaji refreshments. Kama ni kweli ni mpenda burudani kama unamshabikia Diamond raha sana, jamaa ana vibe kali.

Ipo sehemu tu katika mambo yake itakunogea na kukuvutia. Naangalia Wasafi TV live mapokezi anayopewa sitaki kuamini kama watu hawa wamenunuliwa; mji umesimama.

Wasanii wengine ukiwashabikia ni kama unashabikia Arsenal. Msanii full kuringa hakupi mtazamo chanya wa kupambana na shida.

Kiukweli Diamond ni mtaalamu wa burudani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanamuziki mkubwa, Mwanamuziki anayependwa, Mwanamuziki maarufu na mwanamuziki tajiri Afrika Mashariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom