Ukiwa Rais wa nchi ni vema ukawa rafiki wa wapinzani, tenga hata muda wa kuongea nao

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Ukiwa Rais wa nchi yoyote ile ni vema ukawa rafiki au karibu na wapinzani wote hata muda wa kufanya nao mazungumzo jitahidi uupate, dunia ya sasa hivi sio dunia ya kuwa na maadui bali kuongeza marafiki ila usalama wako unakuwa ni mkubwa sana.

Inaweza ikatokea mmoja akamhitaji mwingine ili warekebishe hali au kitu flani hapo inakuwa rahisi kuwasiliana na kukubaliana tofauti na kukataa kabisa kuongea na kuwasiliana na mwingine. Tujifunze na tuwafundishe na tuwaelekeze vizazi vyetu viwe vizazi vyenye maadili na kuona kuna umuhimu wa kuwa na urafiki na wengine ambao ni wapinzani.

Kuwa rafiki wa mpinzani hakumuondolei mtu heshima, hakumpunguzii mtu chochote mwilini ni kuandaa maisha yenu ya baadae, ya vizazi vyenu na watoto wenu kukaa pamoja na si kutengeneza uadui, hakuna ajuaye kesho yake ni Mungu tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WAKAZI WAKE WOTE
 
Back
Top Bottom