Wadau, hasa vijana wenzangu,
Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi
Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu
haha utakua una gross ya laki 3!!
tafuta hela wewe mwanadamu!!!