Ukiwa Kiongozi Soma Mithali!

Ukiwa Kiongozi Soma Mithali!

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
5 Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.
Mithali 16 :5

6 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha Bwana watu hujiepusha na maovu.
Mithali 16 :6

7 Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
Mithali 16 :7

8 Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
Mithali 16 :8

12 Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki.
Mithali 16 :12

13 Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa.
Mithali 16 :13

18 Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
Mithali 16 :18

21 Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu.
Mithali 16 :21

22 Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao.
Mithali 16 :22

23 Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.
Mithali 16 :23

24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
Mithali 16 :24

25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Mithali 16 :25

27 Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara; Katika midomo yake mna moto uteketezao.
Mithali 16 :27

29 Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema.
Mithali 16 :29
 
dah..hapa hapanihusu,njooni wakristo na waislam wenye dini zenu za waarabu na wazungu!!!!!!!
 
Hiyo 8 na 18 ningekuwa na account ya twitter ya Pengo ningempostia ili aweze kushea na swaiba wake wa magogoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom