Ukweli kwenye maisha kuna watu wanaumiza nafsi za watu!Kuna mtu anakuuuuuumiza, mwingine anaishia tu kusema sorry, mwingine anakuona ndio kwanza unacomplicate maisha, mwingine anakupotezea tu na kuendelea na hamsini zake, ili mradi tu, wewe ndiyo unakuwa umebaki na majeraha ya ndani.Siku zote nasisitiza shida siyo jambo linalokupata, shida ni vile unavyolichukulia au kupambana nalo.(The problem is not a problem, but rather the way you react to problems.)
Kila mwanadamu ni wa thamani sana, kwake mwenyewe, kwa jamii inayomzunguka na kwa Mungu. Watu wanapokuumiza wengine ni makusudi na wengine ni ubinadamu wao umepungua sana ndani hadi wanakosa utu kabisa na kitu twaita empathy.
Hivyo kukubali kulia sana, kuumia sana, kununa, kususa, kuzira ni kuendelea kujiumiza wewe, MAANA UKWELI NI KUWA UKIKASIRIKA HUMUUMIZI ULIYEMKASIRIKIA BALI NAFSI YAKO YA NDANI.
Na kwa kuruhusu uchungu na hasira unajiumiza mwili wako kwa kuzeeka kabla ya siku, kukomaza uso, kupata magonjwa tabia na kujipunguzia wema kwenye mahusiano mengine.