GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,645
- 10,867
Hupaswi kumlazimisha mtu akuone wa thamani, lakini ni kosa kubwa sana kutokujithamini!
Imeandikwa, "Mpende jirani yako kama nafsi yako". Kutokujipenda ni kosa.
Ukijithamini, na wengine watakuthamini. Na hata wasipokuthamini itakupungizia nini ikiwa unajithamini?
Kijana mmoja, Yusufu, aliuzwa na ndugu zake na kujikuta mtumwani Misri. Lakini alikuwa na kitu cha thamani ndani yake. Nduguze hawakukikubali, lakini Wamisri walipokigundua, walikitumia kwa usahihi na ikawa msaada kwao na mataifa mengine. Kama nduguze wasingemwuza, wasingelazimika kufuata chakula Misri. Lakini kwa kuwa walimwuza mtatuzi wa njaa, iliwalazimu kumfuata huko alikoenda kutimiza ndoto yake, Misri.
Kwenye video iitwayo STREET UNIVERSITY, kuna ushuhuda wa kijana mmoja aliyefukuzwa kazi na bosi wake kwa sababu bosi alimwona kama ni "much know". Miaka mingi baadaye, bosi aliyemfukuza kazi alienda kupanga kwenye jengo la huyo kijana. Ni baada ya kampuni ya huyo "bosi" kuyumba kibiashara na kulazimika kuhama kwenye jengo la awali baada ya kushindwa kulipa kodi. Ajabu ni kwamba hilo jengo lilitokana na wazo lilikuwa limekataliwa na huyo bosi. Alipolipendekeza hilo wazo kwa bosi wake, siyo kwamba alilikataa tu, Ila pia alimfukuza na kazi.
Akiwa nje ya ajira, alilifanyisha kazi hilo wazo lililokataliwa na Mwajiri wake na hatimaye likamzalia jengo kubwa la kisasa, jengo ambalo baadaye aliyekuwa Mwajiri wake alikuja kupanga.
Ninamfahamu mtu mmoja, lakini simtaji jina. Alipokuwa akifanya kazi kwenye taasisi fulani, alikuwa na kawaida ya kumshauri bosi wake mambo anayoamini yangefanya management ya taasisi kuwa bora. Lakini bosi wake alimtafsiri isivyo. Alifikiri anamkosoa kuwa hawezi uongozi. Huyo mtu alipoacha kazi hapo, watu fulani walimwita na kumpa kazi kwenye kampuni yao. Hakuomba ajira, alitafutwa na wenye kampuni baada ya kusikia sifa zake.
Matokeo yake? Aliwaendeshea kampuni kwa viwango ambavyo viliwafanya wamiliki wake wakiri kuwa wamelamba dume. Wazo lililokataliwa na aliyekuwa Mwajiri wake kabla hajajiunga na hiyo kampuni, lilienda kufaa sana kwenye kampuni yake mpya ambayo alipewa jukumu la kuwa Meneja.
Mama mmoja mkoani Tanga alisimulia jinsi alivyokuwa akitamani aolewe na mwanaume fulani. Alikuwa anafahamiana naye, lakini hakuwa akifikiri kuwa angepata bahati ya kuwa mke wake.
Mwanaume mwenyewe alikuwa na ulemavu. Mguu wake mmoja ulikuwa mfupi, kwa hiyo mwendo wake ulikuwa ni tofauti na WA watu wengine. Najua unajua mwendo ulivyo wa mtu ambaye mguu mmoja ni mfupi.
Lakini wakati mabinti wengine wakitafsiri tembea ya huyo mtu kama kituko, kwa huyo mwanamke ilikuwa tofauti kabisa. Kwake ilikuwa ni burudani murua. Alikuwa akiona anavyotembea, moyo wake "unadundadunda". Alivyo na bahati, huyo mwanaume aliishia kumwoa, na hivyo wakati nasimuliwa hayo mwaka 2009, walikuwa mume na mke wa miaka mingi huko Tanga.
Ruth Graham, mke wa aliyekuwa muhubiri maarufu nchini Marekani, Billy Graham, anahusisha mafanikio yake ya ndoa na kukataliwa mara saba na vijana waliomchumbia. Kabla Billy hajamchumbia, alishachumbiwa na vijana saba lakini wote wakaishia kumtosa kabla ya ndoa. Ulikuwa ni uzoefu unaoumiza sana. Ilifikia hatua akahisi kukata tamaa ya kuolewa.
Lakini alipokutana na Billy Graham na hatimaye kufunga naye ndoa, alishukuru kwamba mahusiano yake saba ya awali hayakufanikiwa. Kama yangefanikiwa, asingeweza kuwa mke wa Billy Graham ambaye mpaka wanatenganishwa na kifo uzeeni mwao, walikuwa wangali wapenzi wa kupigiwa mfano kuanzia kwa watoto wao, wajukuu, majirani na watu wa Mataifa mengine.
Kwa maelezo yote hayo, ninalenga kusema jambo moja tu! Ukikataliwa usijikatae!
Wanaokukataa wanafanya hivyo kwa sababu tu hawajui thamani yako. Lakini kama wewe unaijua thamani yako, ipo siku na wao wataijua bila kuwaambia.
Iwe ni kazini, kwenye ndoa, kwenye familia, na hata kwa majirani zako! Kama wamekukataa usijikatae. Wana uhuru wa kukukataa, lakini utafanya kosa kubwa sana endapo na wewe utajikataa.
Huna "wewe" mwingine! Mjali "wewe" kwa usahihi na wengine watakuunga mkono kumjali, kumheshimu, na kumthamini "wewe"!