Ukiujua vyema Mpira Kiufundi hutomshangaa Kocha Robertino kutomuingiza jana Kipa Kakolanya katika Penati

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,119
Baada ya Kumsoma vyema Kocha Mkuu wa Simba SC Robertino Oliviera nimegundua kuwa Kocha Mwerevu ( Genius ) sana.

Kiufundi hakutaka Kumuingiza Kipa Beno Kakolanya aliyekuwa Nje ( Sub ) kama ambavyo Wengi tulitaka afanye hivyo kwa sababu Kuu hizi Mbili tu..

1. Kocha Robertino anataka Kumtengeneza Kipa Kinda Ally Salim ili aje kuwa Msaada mkubwa kwa Simba SC mbeleni hivyo anamtengenezea Confidence zaidi Golini na laiti ile Jana angemtoa angemuumiza mno Kisaikolojia na Kipa kujiona hana Thamani. ( GENTAMYCINE nimempongeza Kocha Robertino kwa hili )

2. Kiufundi hasa kwa Nafasi ya Kipa ili awe Mchezoni Kimwili anatakiwa awe ame warm up hata kwa dakika 15 hivyo kama Jana angeingizwa Kipa Beno Kakolanya ambaye najiuliza ni nani aliwahakikishia Mashabiki wa Simba SC kuwa angeingia angeokoa Penati.

Kuna Timu moja Kubwa tu hapa Tanzania ilicheza Mechi Moja ya Kimaamuzi Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar na kuwa na Kipa siyo Mzoefu ila alidaka Mechi yote na ilipofika tu katika Penati wakamtoa na Kumuingiza Kipa Mzoefu ambaye alifungwa na Kutolewa kisha baadae Lawama zote zikaangukia kwa Kocha Wao.

3. Kocha Mkuu Robertino alichokifanya Jana ni kutupa Somo Maalum la Mwanadamu Kujiamini kwa Unachokiamini na kuwa na Msimamo wako hata kama itakugharimu Kiutendaji.

Nimempongeza Kocha Robertino.
 
Kiuhalisia upo sawa kabisa ila kuna wale wanaoshabikia timu sasa wao wanachotaka timu isifungwe ilibwasichekwe na mtani😂😂😂
 
Back
Top Bottom