EMMYGUY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 11,094
- 25,336
Wabari Wakuu!
Maisha yetu yanazidi kubadilika kila kukicha, kuna mambo hapo mwanzoni hayakuwepo na kuna mengine pia yalikuwa yanatokea. Uolewaji wa wanawake katika jamii zetu kwa kipindi cha nyuma ulikuwa ni wa kufuata maadili na misingi ya jamii.
Kadri ya ulimwengu unavyozidi kwenda ndio na mambo yanazidi kubadilika, mfano uchumba wa siku hizi sio dili tena kama zamani. Watu wamekuwa wakitumia neno uchumba kwa lengo la kupata kile wanachokitaka, maana inaaminika uchumba ni hatua kubwa inayofikiwa na wapenzi kabla ya ndoa.
Siku hizi ukimtongoza mwanamke anakuwa mwepesi sana wa kuhalalisha mahusiano yenu yawe wazi, hata kama mwanaume huna mpango wa kumuoa tayari wao wanakuwa wanaonyesha dalili zote za kutaka kuolewa.
Wanaume wengi hata humu JF wamekuwa wakilalamika kuhusu hichi kitu. Sijajua hasa tatizo ni nini mpaka wanafikia katika hatua hiyo, ukimtongoza binti leo kesho tayari hata ndugu wameshajua.
Hebu tujadili hili jambo kwa pamoja.