ukitolewa prostate unaweza kuzaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ukitolewa prostate unaweza kuzaa?

Discussion in 'JF Doctor' started by gambalanyoka, Nov 24, 2011.

 1. g

  gambalanyoka Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nauliza mimi nimefanyiwa TURP na ninapokutana na mwanamke sitoi shahawa kabisa nikiuliya naambiwa kuwa hiyo retrograde ejaculation,sasa nauliza je ukitolewa prostate unaweza kuzaa?
   
 2. O

  Obinna Senior Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuwasubiri wataalam i need to knw too!
   
 3. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,463
  Likes Received: 10,673
  Trophy Points: 280
  kwani nani alikwambia mwenye prostate anaweza kuzaa?
   
 4. o

  omholo Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TURP ni upasuaji wa kutoa prostate zilizovimba kupitia kwenye mrija wa mkojo(urethral).miongoni mwa kazi za prostate gland ni kusaidia kibofu cha mkojo(Bladder) kufunga wakati wa kumwaga mbegu(ejaculation). Kwa hiyo retrograde ejaculation inasababishwa na prostate kuondolea.

  Retrograde ejaculation ni kitendo cha shahawa kurudi/kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kwenda kwenye mirija ya kutolea mkojo wa uume. Wakati wa ejaculation bladder hufunga kuruhusu shahawa kupita moja kwa moja kupitia mrija na kutoka nje kwenye uume.

  Hivyo tatizo lako ni kwamba bladder haifungi sasa,hivyo ni ngumu kupata mtoto sababu shahawa hazitoki nje badala yake zinarudi kwenye kibofu.ni vema ukamwone doctor.aliyekufanyia operation hiyo atakupa ushauri zaidi.
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Nadhani unaweza kupata mtoto kwa kutumia "artificial insemination". madaktari watakuja kutoa msaada zaidi hapa hayo yangu ni mawazo tu na sina ujuzi sana katika hili zaidi ya kusomasoma kijuujuu tu kuhusu hili, sijaingia deep.
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ni vizuri ukawasiliana na Dr aliyekufanyia TURP kwa ushauri zaidi. Kukosekana kwa chachu zinazotoka kwenye tezi la Prostate hazizuii mbegu (sperm cells) kukomaa, tatizo hapo kama laivyokueleza Omholo ni kuwa mbegu hizo zinarudi kwenda kwenye kibofu badala ya uke. Sio lazima ukiwa na retrograde ejaculation shahawa yote irudi, sometimes kuna kiasi kinapita na kuingia ukeni, kwa hiyo kuna possibility ya kutungisha mimba, ila kama alivyoshauri FF, kama imeshindikana...basi waweza fanya In-Vitro Fertilization (IVF). Siku hizi Bongo kuna IVF clinic pale Mikocheni opposite na Cloude Entertainment, baada ya kuonana na Dr aliyekufanyia operation unaweza pia kwenda pale kwa ushauri juu ya IVF kama ni muhimu sana kuzaa.
   
 7. g

  gambalanyoka Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri huo,nitamwona dk,sasa jambo lingine ila linahusiana na hilo ni kwamba frequency za kukojoa ni kubwa yaani nakojoa mara kwa mara tena kwa gape ndogo sana,yaani nikienda kukojoa inachukua less than a minute naenda tena kukojoa sasa nashangaa sana maana nilitolewa prostete ili urine retention iondoke sasa bado ipo,nimepima kisukari lakini sina,je hii ni nini?
   
Loading...