Ukitoa toa bila kukumbuka

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
UKITOA TOA BILA KUKUMBUKA

Neno KUTOA lina herufi tano ambazo ni chache sana kuliko milioni, utajiri, na kufanikiwa lakini neno hilo ndilo linatengenezea watu maneno yote hayo yenye faida...

Jambo la kutoa ni moyo wala sio mali ulizo nazo au mafanikio yako uliyonayo......, unaweza ukawa huna mali lakini maneno yako kuyatoa kwa mtu yakawa na thamani zaidi ya mali..
Kutoa ni moyo naposema ni moyo namaanisha lazima uwe na moyo wa kuhifadhi ulichotoa yaani ulichotoa kibaki moyoni mwako usikumbuke ulichotoa..unapokumbusha ulichotoa au kusema kwa watu kuwa umemsaidia mtu fulani jua kuwa sio msaada bali ni deni unalitangaza na unataka fadhila zako ulipwe..
Toa msaada bila kukumbuka na uliemsaidia akifanikiwa hatasita kuelezea msaada wako kwa watu...

Benjamini Graham hakutangaza kumsaidia Warren Buffet lakini Buffet alipofanikiwa alitangaza kuwa kufanikiwa kwake mbali na jitihada zake lakini kuna mtu alieitwa Benjamini aliechangia yeye kufanikiwa zaidi...kumtangaza aliekusaidia sio mbaya ila kumtangaza unaemsaidia ndio mbaya hata kiimani dini zote zinakataza hilo..

Wewe amini kuwa Unapotoa msaada mfano kusaidia watu wa tano wafanikiwe jua kuwa umesaidia familia tano za kitanzania kufanikiwa na ndani ya familia hizo zitasaidia wengine wewe baki kuamini hivo lakini usiangalie nini kinaendelea..

Ishi kwa kuwa msaada wa jamii sio kwa vingi ulivyo navyo bali kwa moyo uliojaliwa na Mwenyezi Mungu nae Mungu atazidi kukujalia kila siku
.
.
.
.
.
.
.
.
By Jay Speed
 
Back
Top Bottom