Turudi kwenye mada. Kwa mtu yeyote mwenye uelewa kidogo wa mambo ya bajeti haitamuingia akilini eti NEC wamerudisha Sh 12bln/-. Budgeting for an election in our situation is an exercise of dealing with definite numbers. No variables. No guesswork! Idadi ya watu wanaotakiwa kuandikishwa inajulikana na inatolewa na Ofisi ya Takwimu (NBS). Idadi ya kupiga kura waliondikishwa inajulikana. Idadi ya vituo inajulikana. Jiografia ya nchi na miundombinu ya ushafirishaji vinajulikana. Sasa pesa yote hii Sh 12bln/- ilibakije? Lazima kuna omissions zilifanyika, tena kwa kiasi kikubwa, kwa lengo la kuvuruga mchakato wa uchaguzi. Kumbuka, kutokutumia fedha kwa mujibu wa bajeti ya uchaguzi ni njia mojawapo ya kuvuruga uchaguzi (poll rigging).