Ukitaka kushangaa nenda Buza Tandika

Kwani halalbadri ni nini? nijuavyo mimi ni kuwa mtu afanyiwapo mambo ambayo humuudhi munga na mja huyo kwa kutambua uduni wake na utukufu wa mungu huamua kumshatakia yeye bwana wa viumbe wote [vengence is mine so said the lord] ili mungu amhukumie.
na madam ameiona mali iliyoiibiwa ninadhani hukumu imepita yeye anapaswa achukuwe kilichobakia kama atatengeneza au atauza ni juu yake.
Kama mwenye mali kweli yupo na haendi kuichukuwa basi kuna walakini aidha naye aliiba, alidhulumu au pengine alikwenda kwa mganga wa kienyeji na kufanya mambo yanayomchukiza mungu basi lana yake hata yeye mwenyewe anaogopa kuichukua
 
Pia kuna wale ng'ombe 4 pale Mtongani njia panda ya kwenda Bahari Beach,
Yasemekana mwenyewe akipita huwa anamwaga machoz,ila ndo hvo,hawezi kuwachukua,washasomewa Al Badri.
 
Discuss kwa mapana na marefu superstition an intergrating force in social cohesion. 10 marks.
 
Natamani ningeona kwenye kuran iwe inataja msamaha kwa watenda dhambi, hapo ningeupenda sana uislamu

ki kubwa ktk uislam kama umetenda kosa ni ww Kukiri kosa lako, then msamaha unafuata.
Tafakari kabla ya kutenda kosa uislam ni njia sahihi ya maisha yako na ime cover kila kitu ktk maisha yetu ya kila siku.
 
Hakuna kitu kama hicho,mi nielekezen vzur nkajichukulie kausafiri hako
 
hivi wale mbuzi waliokuwa wanashinda drive in kabla ubalozi kujenga nawaona kinondoni nao hawana mmiliki?
 
Hakuna cha Al badri wala nini ni imani hiyo.

Ile ni sala ambayo mtu anaomba kwa dhati katika kuombea jambo fulani baya limpate mtu.

Hata mimi Mkrsito Mkatoliki ninayejua BIBLE nikiamua kusoma Biblia naweza kukudhuru wewe. Na ushahidi ninao nilishakitumia kitabu hiki nikashindana nanguvu za Quran.

Katika BIBLE kuna kitabu cha ZABURI kunamaombi ya kila namna upendavyo ukiyaomba kwa kutumia zile sala na kwa dhati, Hakika majibu yatakuja. Nilishafanya hivyo mwisho jamaa akaamua kuniita mimi mchawi kumbe nimemmaliza nikafanikiwa na yeye akashindwa.

Ndugu zangu Wakristo tusibabaike na Al badri hicho ni kitabu na hiyo ni sala ambayo hata sisi tunaiweza tuwe na imani katika kumuomba Mungu wetu wakweli. Wao waache waombe mabaali kama enzi za nabii Eliya.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
viongozi wetu wa dini wamekuwa sawa na wana siasa tu sioni tofauti yao,maana ukitazama msingi wa siasa ni mzuri sana lakini wanaosimamia huo msingi mambo wanayofanya ni kinyume kabisa,
ni sawa na viongozi wetu wa dini tena hapa ni wa dini zote wamekuwa wao ndio vyanzo vya kila upuuzi,wamekosa maadili wamekosa hekma wamekuwa wapo wapo tu,wengi wao mafundisho ya dini zao wameyasahau zaidi wanafata matamanio yao tu,

ntawapa mfano wa kiongozi muadilifu ambae aliwahi kutokea baada ya mtume muhammad huyu bwana alikuwa anaitwa omar bin khatab,huyu bwana historia inasema alikuwa katika ujinga na hakuwa muislam na alikuwa adui mkubwa wa uislam na aliuwa sana waislam,lakini baada ya miaka mingi huyu bwana akaamini yaani akasilimu akamfuata mtume,

basi huyu bwana alimsoma mtume sana akasoma sana dini mpaka ikamwingia akawa ni mtu wa karibu sana na mtume,na huyu bwana alikuwa ni mtu tajiri sana pale makkah na alikuwa ni maaruf pia,
historia inasema huyu ndio katika viongozi waadilifu duniani ambao walipata kutokea basi omar alikuwemo,
omar ni khalifa wa mtume wa 3 yaani baada ya kufariki mtume aliefuata kuwa mtawala wa makkah alikuwa ni abubakar siddiq, wa pili othman bin affan,na wa 3 alikuwa ni omar bin khattab,
kuna siku jamaa mmoja alitembelea ofisini kwake omar ilikuwa muda wa usiku alikuwa ana maongezi nae wakati huo akiwa omar ndio kiongozi mkuu wa saudi arabia,basi huyu bwana alikuwa akimuuliza omar maswali mengi tu ya dini na family yake anachanganya maswali, basi omar alikuwa na mishumaa miwili pale ofisini kwake basi alikuwa anawasha mshumaa mmoja mara anazima mwingine,yule mgeni wake ikabidi amuulize mbona mara anazima huu anawasha huu?
Omar akamjibu wewe unaniuliza maswali mchanganyiko kuna maswali unaniuliza yanahusu family yangu ndio maana nazima mshumaa huu nawasha mwingine'kwa sababu mshumaa mmoja nimenunua kwa pesa ya kwangu na mwingine kwa pesa ya waislam ndio maana hapa naogopa kupata dhambi kila ukiniuliza swali la family yangu nazima mshumaa wa waislam nawasha wangu nakujibu,na ukiniuliza swali la waislam nazima wangu nawasha wa waislam pia sitaki kuwafanyia dhulma family yangu,
hebu jaribu kufikiria uadilifu gani huyu jamaa aliokuwa nao?

Na historia inatuambia huyu omar alikufa kwa maradhi ya tumbo kwa sababu alikuwa hataki kula vizuri licha ya yeye kuwa tajiri alikuwa akisema hawezi kula chochote kizuri wakati mitaani kuna watoto yatima wamejaa na wajane wasio na misaada ndio akaona badala ya kula yeye vizuri bora wengine wale,
je viongozi wetu wa leo hata robo ya uadilifu wanayo?

kwa vyovyote vile huo ni uadilifu wa hali ya juu ambao unapaswa kufuatwa hasa na viongozi wakuu wa nchi . Ikiwa hivyo hata kati na chini wataogopa na wataiga wakubwa wao. Viongozi wetu wanapaswa kufahamu kuwa hesho siku ya hesabu watahukumiwa mbele ya bwana wa viumbe wote kwani dhamana waliyobeba ni kubwa na kwa bahati mbaya ni kuwa wakati wanapoingia ofisini wanaapa kwa kutumia vitabu vyake na hivyo vitabu ndiyo vitawashitaki
 
naomba uelewe kwanza qur-an haina uhusiano na albadir, wala katika qur-an hakuna kitu kinaitwa albadir,na wala katika mafundisho ya uislam hakuna al badir sehem yeyote inapofundishwa,
kwanza hakuna ukweli kama al-badir ina madhara yeyote ila tunachoamini huwa kweli,kwa sababu huyo anaekusomea albadir anasoma kitabu cha majina ya watu ambao walipigana katika vita ya badri ndio maana kinaitwa al badir.ndani yake hakuna dua yeyote zaidi ya majina ya watu,ila kwa sababu tulishaamini toka enzi tunaumia kwa imani kuliko ukweli wenyewe


thank you
 
[QU="figganigga, post: 4889908, member: 28550"]unakua umeshavuka pale kwa mama kibonge? mimi nashinda zangu pale gaddaf lakini bado sijaona hiyo kitu. mia[/QUOTE]
Ni gossip hizo, pale temeke veterinary kuna pikipiki iliwahi andikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa mtu akiisogelea inajiwasha , nilienda pale nikaiona na nikauliza kwanini iko pale na haiondolewi: ukweli ni kuwa ile pkpk ni mali ya umoja wa madereva wa boda wanaopaki pale, waliamua kiweka pale cos kila aliyekuwa anapewa alikuwa hapeleki hesabu , hivyo wakaamua waiweke pale ili kila memba aione.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom