Ukitaka kuoa au kuolewa usukumani, yajue haya

1. Wasukuma ni kabila kubwa kuliko yote Tanzania. Mikoa ya Simiyu, Tabora, Shinyanga, Geita, Mwanza kote huko ni usukumani.

2. Usukumani siyo lelemama, kuna Kazi nyingi kama kushinda shambani, uvuvi, kushinda machimboni ,ikiwemo kutunza maelfu ya mifugo hasa Ng'ombe etc

3. Wasukuma ni extended family, siyo ajabu mtoto wa shangazi akakulia kwa baba mdogo na akalipiwa ada bila ubaguzi wowote. Kwa hiyo jiandae kuwa na familia kubwa yenye upendo kutoka kwa ndugu wengine.

4. Wasukuma ,baba ndio head of the family, mama ni msaidizi tu na siyo lazima ushauri wake ufuatwe

5. Usukumani familia ni namba moja. Kwa hiyo hata kama ni tajiri lakini huna familia utadharaulika sana .
Hali hii huwalazimisha wanaume kujali familia zao. Matokeo yake wanaume wa kisukuma huonekana wanajua kupenda.

6. Mwanza linakopatikana ziwa la pili kwa ukubwa duniani (Ziwa Victoria) ilifikia hadhi ya jiji mwaka 2000 . Kwa hiyo Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa baada ya jiji la Dar.

7. Usukumani muoaji hupokelewa kifalme na mke hupokelewa kama malkia.
Kama siyo mchoyo na mwenye zarau, usukumani utaishi kwa raha sana

8. Usukumani amani ni namba moja.
Mtu yoyote au kikundi cha watu kinachotishia amani, huondolewa mara moja kupitia nguvu ya uma. Kama ni mkorofi mpenda fujo, utaishi kwa shida sana kwa sababu utatengwa na jamii nzima.

9.Wasukuma ni watu wenye msimamo na wasiopenda uongo.
Huwezi ukasema hili kesho ukasema lile alafu bado ukashangiliwa tu.
Ukienda usukumani unatakiwa unyooshe maelezo.

10 . Wadada weupe hawapati shida ya kupata wachumba.
Ukiwa mweupe hata uwe na tabia mbaya mbaya utanyooshwa tu na kuolewa.

Kama wewe ni mweusi alafu una tabia mbaya mbaya, sahau kuolewa, kwa hiyo kwa mweusi kuwa na tabia nzuri ni lazima.

11. 90% of Cotton grows in Sukuma land
Nimehongwa nyumba na msukuma nikakataa....
 
Vipi kuhusu kupenda uganga wa kienyeji na kushiriki mambo ya giza
Hujasema kabisa ilihali tunajua kuna sehemu huko Shinyanga inaitwa Gamboshi na tangu nikiwa mdogo nimepata simulizi nyingi za kutisha
 
Amesahau hili,wasukuma wengi wao huwa hawaflash baada ya kumaliza haja.na hili tatixo wanalo hta badhi ya wasomi wa kisukuma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom