Ukitaka kuoa au kuolewa usukumani, yajue haya

1. Wasukuma ni kabila kubwa kuliko yote Tanzania. Mikoa ya Simiyu, Tabora, Shinyanga, Geita, Mwanza kote huko ni usukumani.

2. Usukumani siyo lelemama, kuna Kazi nyingi kama kushinda shambani, uvuvi, kushinda machimboni ,ikiwemo kutunza maelfu ya mifugo hasa Ng'ombe etc

3. Wasukuma ni extended family, siyo ajabu mtoto wa shangazi akakulia kwa baba mdogo na akalipiwa ada bila ubaguzi wowote. Kwa hiyo jiandae kuwa na familia kubwa yenye upendo kutoka kwa ndugu wengine.

4. Wasukuma ,baba ndio head of the family, mama ni msaidizi tu na siyo lazima ushauri wake ufuatwe

5. Usukumani familia ni namba moja. Kwa hiyo hata kama ni tajiri lakini huna familia utadharaulika sana .
Hali hii huwalazimisha wanaume kujali familia zao. Matokeo yake wanaume wa kisukuma huonekana wanajua kupenda.

6. Mwanza linakopatikana ziwa la pili kwa ukubwa duniani (Ziwa Victoria) ilifikia hadhi ya jiji mwaka 2000 . Kwa hiyo Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa baada ya jiji la Dar.

7. Usukumani muoaji hupokelewa kifalme na mke hupokelewa kama malkia.
Kama siyo mchoyo na mwenye zarau, usukumani utaishi kwa raha sana

8. Usukumani amani ni namba moja.
Mtu yoyote au kikundi cha watu kinachotishia amani, huondolewa mara moja kupitia nguvu ya uma. Kama ni mkorofi mpenda fujo, utaishi kwa shida sana kwa sababu utatengwa na jamii nzima.

9.Wasukuma ni watu wenye msimamo na wasiopenda uongo.
Huwezi ukasema hili kesho ukasema lile alafu bado ukashangiliwa tu.
Ukienda usukumani unatakiwa unyooshe maelezo.

10 . Wadada weupe hawapati shida ya kupata wachumba.
Ukiwa mweupe hata uwe na tabia mbaya mbaya utanyooshwa tu na kuolewa.

Kama wewe ni mweusi alafu una tabia mbaya mbaya, sahau kuolewa, kwa hiyo kwa mweusi kuwa na tabia nzuri ni lazima.

11. 90% of Cotton grows in Sukuma land
Yote yaweza kuwa sawa, ila namba5 haswa aya ya pili ni uongo mtupu. Labda hawa wanyantuzu muwatenge na usukuma. Hawazijali familia zao, wakina mama ndo kila kitu. Akishaolewa, mwanaume anayavua majukumu yote kwa mkewe. Si chakula wala mavazi, mwanamke atajijua mwenyewe.

Mwanaume huku, haagi akitaka kuondoka, haulizwi alikokuweko, si lazima ale nyumbani, aoge au alale. Mwanamke ukiolewa huku ni kama tu uko kazini kuilea familia ya mume.
 
Hiyo Namba 8, nakuunga mkono mia kwa mia! Ndiyo maana kwaajili iyo wasukuma walikuwa wa kwanza kuanzisha jeshi lao la ulinzi (sungusungu) miaka ya 80! Na siku hizi ukienda kule Simiyu kuna kitu kinaitwa ''Fagilia!"
Au dagashida
 
This is BS. Tuongeleeni mambo ya maana yenye manufaa kwa nchi yetu. Tuongeleeni kuhusu uchumi wa nchi, nini kifanyike kukabliana na changamoto tunazokabiliana nazo, nk. Karne ya 21 unajadili kuhusu ukabila??? shame on you.

HUMU NI JAMII FORUM
tunaenda jukwaa kwa jukwaa.
usipende kuklpuka pasipo kupitia jukwaa mkuu, ustufanye tukatmia mda mwingi kukushangaa!!!!!!
be ye kind.
Shame on you
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom