Ukitaka kuoa au kuolewa usukumani, yajue haya

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,903
2,580
1. Wasukuma ni kabila kubwa kuliko yote Tanzania. Mikoa ya Simiyu, Tabora, Shinyanga, Geita, Mwanza kote huko ni usukumani.

2. Usukumani siyo lelemama, kuna Kazi nyingi kama kushinda shambani, uvuvi, kushinda machimboni ,ikiwemo kutunza maelfu ya mifugo hasa Ng'ombe etc

3. Wasukuma ni extended family, siyo ajabu mtoto wa shangazi akakulia kwa baba mdogo na akalipiwa ada bila ubaguzi wowote. Kwa hiyo jiandae kuwa na familia kubwa yenye upendo kutoka kwa ndugu wengine.

4. Wasukuma ,baba ndio head of the family, mama ni msaidizi tu na siyo lazima ushauri wake ufuatwe

5. Usukumani familia ni namba moja. Kwa hiyo hata kama ni tajiri lakini huna familia utadharaulika sana .
Hali hii huwalazimisha wanaume kujali familia zao. Matokeo yake wanaume wa kisukuma huonekana wanajua kupenda.

6. Mwanza linakopatikana ziwa la pili kwa ukubwa duniani (Ziwa Victoria) ilifikia hadhi ya jiji mwaka 2000 . Kwa hiyo Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa baada ya jiji la Dar.

7. Usukumani muoaji hupokelewa kifalme na mke hupokelewa kama malkia.
Kama siyo mchoyo na mwenye zarau, usukumani utaishi kwa raha sana

8. Usukumani amani ni namba moja.
Mtu yoyote au kikundi cha watu kinachotishia amani, huondolewa mara moja kupitia nguvu ya uma. Kama ni mkorofi mpenda fujo, utaishi kwa shida sana kwa sababu utatengwa na jamii nzima.

9.Wasukuma ni watu wenye msimamo na wasiopenda uongo.
Huwezi ukasema hili kesho ukasema lile alafu bado ukashangiliwa tu.
Ukienda usukumani unatakiwa unyooshe maelezo.

10 . Wadada weupe hawapati shida ya kupata wachumba.
Ukiwa mweupe hata uwe na tabia mbaya mbaya utanyooshwa tu na kuolewa.

Kama wewe ni mweusi alafu una tabia mbaya mbaya, sahau kuolewa, kwa hiyo kwa mweusi kuwa na tabia nzuri ni lazima.

11. 90% of Cotton grows in Sukuma land
 
Kuna vingine muhimu hujaviweka kuhusu Kabila na utamaduni wa wasukuma, kwa mfano.
1/Ushamba
2/Ubishi.
3/Ujuaji.
4/Elimu duni.
5/Mfumo Dume.
6/Kuzaana bila mpango.
7/Kuoa wake wengi au kuzaa nje ya ndoa.

Ni vizuri kabla ya kuolewa kuyajua hayo.

Umesahau Visasi.Wasukuma wana tabia kubwa moja ya kulipiza kisasi hata kwa kuua aliyemkosea.
 
Hizo tabia zote ulizotaja km za asili zote hazipatikani usukumani zinapatikana kigoma na baadhi ya hizo mkoa wa kagera. Halafu dhana ya ushamba inayojengwa dhidi ya wasukuma ni wivu wa makabila mengine...!!
Wivu kivipi? Mimi natokea usukumani, nimezaliwa huko, nimekulia huko. Ninalijua kabila la Kisukuma kiundani kuliko kabila lingine lolote hapa Utanzania. Ushamba, Elimu duni, Mfumo dume, Ujuaji nk ni mambo ya kawaida kabisa usukumani, tena wasukuma huwa tunalinga nayo!


Msukuma huenda ndio binadamu pekee hapa Tanzania ambaye anaaminishwa toka akiwa mtoto kuwa "Nguvu zake ndio msingi wa yeye kufanikiwa na wala sio Akili yake". Msukuma(Kiasili) anaamini kwa nguvu zake anaweza kuoa msichana yoyote mzuri, akapata mafanikiwa, akaogopewa nk.
 
Wivu kivipi? Mimi natokea usukumani, nimezaliwa huko, nimekulia huko. Ninalijua kabila la Kisukuma kiundani kuliko kabila lingine lolote hapa Utanzania. Ushamba, Elimu duni, Mfumo dume, Ujuaji nk ni mambo ya kawaida kabisa usukumani, tena wasukuma huwa tunalinga nayo!


Msukuma huenda ndio binadamu pekee hapa Tanzania ambaye anaaminishwa toka akiwa mtoto kuwa "Nguvu zake ndio msingi wa yeye kufanikiwa na wala sio Akili yake". Msukuma(Kiasili) anaamini kwa nguvu zake anaweza kuoa msichana yoyote mzuri, akapata mafanikiwa, akaogopewa nk.
Kwa nini husemi kuwa amani ya nchi hii inashikiliwa na wasukuma sababu ya upole na mafundisho tunayoyapokea toka kwa mababu zetu. Ukiishi kwenye familia ya kisukuma kwa muda mrefu hata kama ni mkimbizi lazima upate stahiki sawa na watoto wa familia au ukoo huo.
 
This is BS. Tuongeleeni mambo ya maana yenye manufaa kwa nchi yetu. Tuongeleeni kuhusu uchumi wa nchi, nini kifanyike kukabliana na changamoto tunazokabiliana nazo, nk. Karne ya 21 unajadili kuhusu ukabila??? shame on you.
We jamaa VP.. Reasoning yako ndogo... Katika ulimwengu wa Leo ambapo interaction Kati ya jamii ni kubwa na ya spidi... Kueleza juu ya tamaduni ya jamii fulani ni muhimu kwa ajili ya kutoa mwanga kwa Mtu yeyote apendae kufanya shughuli au makaz yake katka jamii hizo.
Mfano, Hata watalii wanaoingia Tanzania huwa wanapewa darasa juu ya tamaduni zetu Kama nchi na jamii ambazo watatembelea.. Kuepusha migogoro na kuchochea maelewano.
 
Back
Top Bottom