Kila mtanzania atakubaliana na mimi kwamba katika kipindi cha muda mfupi ambapo Dr. Mwakyembe amekaa katika wizara ya uchukuzi amefanya kazi nzuri kuanzia bandari hadi uwanja wa ndege.
Zile kelele za Tanzania kuwa kinara wa madawa ya kulevya na JKN International Airport kuwa kitovu cha upitishaji wa madawa ya kulevya hivi sasa zimekwisha kutokana na kazi nzuri ya Mwakyembe. Sasa hivi ukiachilia mbali matatizo ya system utoaji wa mizigo bandarini umekuwa na unafuu sana, huku wakwepa kodi huko bandarini wakiwa katika wakati mgumu. Ni wazi na dhahiri kwamba waziri Mwakyembe amefanya mageuzi makubwa katika wizara aliyokuwa anasimamia.
Lakini inashangaza sana kuona kwamba baada ya ufanisi huu wote, Rais Kikwete, ameona vema kumtoa Mwakyembe katika wizara hii na kumpa Samwel Sitta ambaye kiujumla hata huko wizara ya Afrika Mashariki ame-underperform.
Ni nani asiyejua kelele za Sitta na kauli zake wakati wa mgogoro kati ya Kikwete na Kagame? Mtu asiye na uadilifu katika wizara isiyo na kazi kama ya Africa mashariki atawezaje kubeba mikoba ya Mwakyembe kuwakabili wauza Unga wenye nguvu na mtandao mkubwa? Napata taabu kuamini kwamba mabadiliko haya ni ya kawaida.
Nashawishika kuamini kwamba Mwakyembe amemvurugia Kikwete biashara zake za madawa ya Kulevya. Maana wote tunajua kwamba Kikwete alipoingia madarakani alituambia anayo majina ya wauza unga, na hadi leo hajawahi kuyaweka hadharani wala kuchukua hatua za kuwakamata hao wauza unga anaowafahamu kwa majina. Ni dhahiri kwamba watu hawa waliingia naye ubia. Na kitendo cha Mwakyembe kusimama kidedea dhidi ya biashara hiyo kinaweza kuwa kimewakera washirika wa Kikwete katika biashara ya madawa ya kulevya na kumshawishi amuondoa.