Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 6,289
- 10,993
Poleni na kazi wajameni,
Leo hii nimekaa na vijana wangu kwenye banda letu tunapouziaga majeneza niko na kasimu kangu ka tecno M3 kale kakizamani (vile vya promosheni ya wale jamaa) sasa niko katika kuperuzi mitandaoni nakutana na haka kajamaa "Dr Shikamoo" eti kila siku kanaibuka na ishu mpya halafu naona kama kuna watu wanakatumia kufanikisha mambo yao maana wanajua kamepata umaarufu wa ghafla na kuwafunika kina Homo Rapa na Ebitoke.
Sasa juzi nilisoma habari sehemu eti Dr shika yuko Kahama ameahidi msaada wa bilioni 2 nikashangaa leo tena nakutana na habari moja eti Dr shika yuko kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa ccm yaani nimejikuta nacheka sana mpaka watu wanashangaa!
Nilichogundua haka kajamaa kakitumia vizuri huu umaarufu wake katika kipindi hiki kigumu katapiga hela ya kueleweka na mwisho kanaweza hata kununua mjengo na usafiri aisee!
Hii inaonyesha jinsi gani kuna wabongo wanajua kutumia fursa! Mzee huyu amenifanya nimkumbuke babu wa Loliondo alivyotumia fursa na akapiga hela na wajanja pia walitumia fursa hiyo kupiga hela kupitia biashara mbalimbali ikiwemo usafirishaji.
Hapa nawaza kumfuata babu yangu kijijini maana tangu astaafu jeshi mwaka 1985 mpaka leo yupo tu analinda shule ya kijiji bure nimlete mjini tukae chini nasi tutafute kiki pengine mzee wangu naye akawa maarufu kama Dr. Shika.