Ukisoma 1 Timotheo 3: 1-10 utagundua kuwa kwa kugombea ubunge Dkt. Gwajima amepoteza sifa za uaskofu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,966
141,975
Hapa naongea kiimani zaidi na siyo kichama.

Sifa kuu ya mtu atamaniye kuwa askofu ni lazima awe na KIASI.

Kadhalika anapaswa kuwa ni mtu mpole, muafilifu, mwenye upendo, mwenye nidhamu, mume wa mke mmoja na asiyekuwa wa kulaumiwa.
Haya yote yameelexwa katika kitabu cha Timotheo wa kwanza, sura ya 3 mstari wa 1 hadi 10.

Kwa mtazamo wangu ni vema sasa Dr Gwajima akajulikana tu kama mchungaji Gwajima akiungana na mchungaji Msigwa kule bungeni.

Nawatakia Dominica yenye baraka hapo kesho.

Maendeleo hayana vyama!
 
Alishazipoteza siku nyingi sana, alivyoanza kuhusishwa na mambo yanayoenda kinyume na miiko ya uaskofu pekee pale alishapoteza uaminifu kiasi kikubwa kwa jamii, hili la kukimbilia siasa ndio limekuja kumuonesha vizuri yeye ni mtu wa aina gani.
 
Askofu Gwajina hakutakiwa kuingia kwenye siasa. Yeye angechagua moja kumtumikia Mungu. Kwake siasa ni ya nini?.
 
Mathayo 22:21: Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.

Imagine wewe ni mwanachama mtiifu wa CHAUMA ila Askofu wako Mkuu Kanisani ni Kada mtiifu na Mbunge wa CCM. Hata zile sadaka zisizo na idadi (sadaka, mbegu, mtembeo, sifa, sadaka ya kujitakasa, zaka, ujenzi, band etc etc..) unaweza acha kutoa
 
Hapa naongea kiimani zaidi na siyo kichama.

Sifa kuu ya mtu atamaniye kuwa askofu ni lazima awe na KIASI.

Kadhalika anapaswa kuwa ni mtu mpole, muafilifu, mwenye upendo, mwenye nidhamu, mume wa mke mmoja na asiyekuwa wa kulaumiwa.
Haya yote yameelexwa katika kitabu cha Timotheo wa kwanza, sura ya 3 mstari wa 1 hadi 10.

Kwa mtazamo wangu ni vema sasa Dr Gwajima akajulikana tu kama mchungaji Gwajima akiungana na mchungaji Msigwa kule bungeni.

Nawatakia Dominica yenye baraka hapo kesho.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani Gwajma ni askofu? nani alimpa huo Uaskofu? These are self proclaimed bishops, wahuni tu wanapeta kwa watanzania wajinga,isukule
 
Back
Top Bottom